Zimbabwe yasitisha matumizi ya sarafu ya kigeni

Zimbabwe yasitisha matumizi ya sarafu ya kigeni

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,378
Zimbabwe imetangaza leo kuwa itasitisha matumizi ya sarafu za kigeni ambazo zilichukua nafasi ya dola ya Zimbabwe iliyokabiliwa na anguko kubwa kabisa la thamani miaka 10 iliyopita.

Taifa hilo lililo kwenye mgogoro wa kiuchumi linakabiliwa hivi sasa na kupanda kwa bei za bidhaa ambapo takwimu rasmi zinaonesha mfumuko wa bei unafikia asilimia 100.

Benki kuu ya Zimbabwe imesema kwenye taarifa yake, kuwa fedha halali zitakuwa ni noti za hati fungani na sarafu mpya ya RTGS ambazo zilianzishwa baada ya kupungua kwa noti za dola za Marekani.

Tangazo la Benki Kuu limesema, dola ya Marekani, randi ya Afrika Kusini, sarafu nyingine za kigeni na dola ya Zimbabwe hazitotumika kama fedha halali katika malipo yoyote nchini humo.

Serikali ya Zimbabwe imeahidi kuchapisha sarafu mpya za nchi hiyo hivi karibuni.

Zim%20CURRENCY.jpeg
 
Naona wanapata ahueni baada ya Mugabe kuondoka madarakani
 
Labda wana weza kupata nafuu ya uchumi
 



Re-Introduction Of Zimbabwe Dollar and ‘Banning’ Of Foreign Currency

Zimbabwe has banned use of the United States dollar and other foreign currencies for local transactions.

This is with immediate effect, and means the RTGS dollar is currently the sole medium of exchange.

Statutory Instrument 142 of 2019 reads, in part, “The British Pound, United States Dollar, South African Rand, Botswana Pula and other foreign currencies whatsoever shall no longer be legal tender.
 
Labda ubebaji wa pesa kwenye matoroli utapungua
 
Back
Top Bottom