Zimbabwe: The turmoil, reconciliation, and the future!


Ni kweli Mugabe sasa hivi saa kumi na mbili imetimia na hata yeye mwenyewe anaona hawezi tena kuwaburuza wananchi wake anatafuta mwanya wa kukimbia.

Kuhusu Zimbabwe kuja juu hilo halina ubishi nchi ni watu ambao wanafanya kazi ili kujikomboa na mafedhuli na vile vile wengi wao wanasoma hivi sasa nchi za nje na ukitilia maanani kwamba asilimia kubwa wanawasupport ndugu zao kwa pesa ambazo wanafanya kazi nje. Petrol ina nunuliwa kwa cupon in forex ambazo zinatumwa na Zimbabweans hivyo Mugabe akitoka utaona jinsi watakavyojikwamua.
Angalia hapa chini inflation inavyotesa ..............................................


Kuhusu kuwasaidia tumewasaidia vya kutosha, Zimbabwe ni sovereign state kama Mugabe mwenyewe anavyosema na suala la kuwa na currency moja au kuungana haliondoi ukweli kwamba nchi zote ulimwenguni madictator watatokea na kama wananchi hawako macho wataumia. Hii miungano ambayo ni ya siri mimi siiafiki, hawa wanaotaka miungano hivi sasa wanataka kutumia ujanja ujanja ili kutafuna pesa za walipa kodi. Miungano hii ingetokea wakati ule wa kupigania uhuru sio hivi sasa wakati kila mtu anakodolea mali ya mwenzake. Cooperation tunayotakiwa kuwa nayo ni ya biashara kuwa na msimamo moja kwenye rasilimali tunazouza nje i.e. madini, vyakula na mazao ya biashara n.k. Utakumbuka vizuri kwa mfano Airport tax Tanzania tulikuwa tunacharge USD 20.00 (miaka ya 1980's) wakati nchi zote majirani walikuwa wanacharge USD 10.00. watalii waliendelea kulalamika kwa kipindi fulani na baadaye wengine waliamua kuwa wanakuja Bongo kwa barabara n.k.

Afrika wote tusimame kidete kuwaondoa hawa mafedhuli.
 
Coalition Set Up to Back Ncube


Mugabe anatumia kila njia kutuliza mapigo.
 
Zimbabwe launches $200,000 note


Food shortages have become common in Zimbabwe

Soma Hapa

You want to be a millionare overnight come to Zimbabwe.

Hii hali inatisha jamani hata ungemchukua mtu ambaye hakwenda shule uchumi usingekuwa mbaya namna hii. Naona wataanza kula degree za bwana Mugabe.
 
Zimbabwe: 'Zim to Import Maize From Tanzania'

The Herald (Harare)
31 July 2007
Posted to the web 31 July 2007

Harare
ZIMBABWE will import about 200 000 tonnes of maize from Tanzania as part of drought mitigatory efforts, the Minister of Agriculture, Cde Rugare Gumbo, has said.
He said the country has been importing grain from friendly Sadc countries like Zambia and Malawi in the past few months.

He dismissed reports that the Government had rejected food offers from international food agencies.
"We have been importing maize from Zambia and Malawi. Right now, we are finalising the modalities to import maize from Tanzania," said Cde Gumbo in an interview last week.
"We are determined to feed the nation and we will do our best to achieve that."
He said most areas in Matabeleland and Masvingo had been severely affected by low rainfall and required food aid.
Cde Gumbo said it was not true that Government was spurning food offers from the Food and Agriculture Organisation, World Food Programme and other international donor organisations.
He said Government was still studying the extent to which the country had been affected and its food requirements.
"We are prepared to engage with anybody, but we are still to assess the amount of maize we can purchase locally and how much we require as imports.
"We can't just rush to the international community without concrete figures and proper statistics on the situation," he said.

The Government has since appointed a board of directors for the Grain Marketing Board and said their responsibility was to professionally market and distribute prescribed commodities, a role the minister described as critical at this time when the country was coming from a poor season and was resorting to imports.

GMB board chairman Mr Charles Chikaura said he would discharge the duty to the best of his ability.
"Right now it's too early for me to say much. I am still to consult with the current acting chief executive officer, and we will meet as a board to chart the way forward," said Mr Chikaura in an interview.

Government has declared 2007 a drought year, meaning that drought-prone areas should receive food relief from the State.
______________________________________________________________

What is the difference between Black Africans and White Africans? Its really a shame to see the same farms used to produce food for the whole Zimbabwe and for export!

This reminds me of us(Tanzania) after Arusha Declaration...

Where are we going wrong? Is it our attitude?
 
Weep for Zimbabwe

Bofya hapa


Ndio viongozi wetu wanapotaka madaraka ahadi lukuki lakini wakishaingia joto ya jiwe inawapata walipakodi.
 
Mugabe Splashes Trillions On Cars


Bofya hapa


Wakati wananchi wanakufa kwa njaa. Ananunua magari ya anasa kwa kutoa ajira kwa wazungu na kutumia pesa ya walipa kodi bila huruma. - HUYU NDIYE MUGABE
 
Strange Twist in Pius Ncube Adultery Case


Soma hapa

Tutaona mengi kabla ya mabadiliko!
 
Hivi karibuni nchini Zimbabwe maofisa 15 wa juu wa jeshi wamefukuzwa kazi kutoka katika jeshi hilo. Hatua hio inafuatia jaribio la kumpindua raisi Robert Mugabe wan nchi hio huru ambae amekuwa madarakani tokea akabidhiwe nchi na wakoloni wa Kiingereza mwaka 1980.

Baaadhi ya maofisa hao wamefikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi, wengine rumande na wengine hawajulikani waliko! Jaribio la sasa linasemekana kuwa lilikuwa ni zito zaidi ya lile lililofanyika mwaka 1998 na sasa zaidi ya 40 wapo chini ya upelelezi wakifuatiliwa na vyombo vya usalama ambavyo ni moja ya vyombo bora katika bara la Afrika kwa uchapaji kazi!

Lakini matukio hayo yakiendelea, hali ya uchumi wa nchi hio inazidi kuwa mbaya. Benki kuu ina kazi kubwa kudhibiti mzunguko wa fwedha na “wafadhili”, “wahisani” na NGOs wanajitahidi kupenyeza pesa kupitia benki kuu kama sheria inavyotaka hata kama fwedha yenyewe itapungua sana kwa thamani ya Dolali ya Zimbawe.

Wananchi wa Zimbabwe ndio wanaoadhibika kwa hali hio kwani hawana chakula cha kutosha, gharama za maisha zimepanda na watu wamepata nafasi ya kwenda nje hasa Afrika kusini kama wakimbizi au wasomi wengi tu wamekimbilia nchi za magharibi na kusababisha kupungua kwa wazalishaji mali nchini humo.

Raisi mwenyewe mheshimiwa Robert Mugabe yeye anatupa lawama kwa mataifa ya nje zikiongozwa na Uingereza kwamba ndizo zinaharibu uchumi wa nchi hio, kwa makusudi ili wananchi wakasirike na hatimae wamchague bwana Morgan Tsvangirai awe raisi wa nchi hio na akaribishe makampuni ya kimataifa,wawekezaji na mabenki, waje na sera ambazo zitazidi kumkandamiza mkulima, mfugaji na yeyote yule anaeishi kijijini kusikopata habari ya nini kinaendelea pale Harare.

Pia Serikali ya Bwana Tsvangirai itakuwa na udhibiti wa jeshi nchi nzima, ndani ikiwa na wazungu ambao ndio wafadhili wa MDC kwa sasa wakiwa na mashamba makubwa.

Lakini ni nini kiini cha matatizo?

Kwa kuangalia matatizo ya nchi hio inabidi kuona jinsi wananchi wa taifa hilo wanavyotaabika kila kukicha. Umri wa kufariki umeshuka hadi kufikia miaka 37 kwa wanaume na 34 kwa wanawake na inawezekana ikashuka zaidi ya hapo.Kwa hio hapa kwa kiasi kikubwa wazalishaji mali ni wanazidi kupungua.

Halafu kuna Ukimwi,ukosefu wa chakula, ukame,ukosefu wa kazi na mfumuko wa bei ambao umefikia kiasi cha asilimia 1800.

Matatizo ya Zimbabwe hayawezi kuelelekezwa moja kwa moja kwa Mzee Mugabe, kama ambavyo watu watapenda kufanya hivo. Mugabe aliongoza harakati za kuikomboa Zimbabwe kutoka kwa ukoloni wa kiingereza.
Lakini kama kawaida ya viongozi wakti ule, siasa zake na tabia ya kijamaa ya kutaka wananchi nao wafaidi matunda ya uhuru, mzee Mugabe akaitwa London pale Lancaster House kuzungumza na mabepari. Baada ya kikao akaamua kuendeleza sera zake za kijamaa ili kupata kuungwa mkono na Wazimbabwe na wakati huohuo akiridhia matakwa ya mabepari (mashirika, makampuni na mabenki). Sera zote zilizoonesha kuzuia kazi ya mabepari ziliwekwa kapuni na hapo fwedha ikaanza kumwagwa na serikali ya mzee Mugabe ikawa na neema na kutumia fwedha ya misaada kwa kuendeleza Elimu na Afya, wakati huo ukienda Harare(nasikia) ilikuwa ikiitwa “Basket of Africa”.

Kama nchi zingine za Africa ikiwemo Tanzania, Zimbabwe ilikubali mpango wa IMF uitwao kwa Kiingereza “Enhanced Structural Adjustment Facility” mwanzoni mwa miaka ya tisini. Soko huria ikawa ndio kisingizio cha kuingiza zaidi fwedha za mikopo kwa hazina ya Zimbabwe kwa masharti kwamba irudishwe ikiwa na riba kubwa juu yake. Matumizi ya fwedha ya Serikali yakapungua kuanzia kwenye Afya, Ukimwi na hatimae deni la serikali (nchi) likaanza kukua kwa kasi na kutokana na masuala ya biashara huria kushika tama duniani na ushindani kuongezeka thamani ya bidhaa za Zimbabwe ikaporomoka na hata madini yakakosa soko na hapo ndipo sera za Mzee huyu zikaanza kuangaliwa kwa undani na wachambuzi.

Mzee Mugabe akaanza kupunguza urafiki na IMF na nchi za magharibi kwani utegemezi wa bajeti ya serikali ambao serikali ilipenda kwa sana ukaondoka. Kama kawaida wananchi huwa wananza kuhisi machungu na mfukoni kunakosa kitu,suluhishi- kuandamana.

Sasa mzee wa watu akachanganyikiwa, akaanza kutafuta watu wa kumuunga mkono na kama kawaida kwa sababu alikuwa kama amewaweka kwenye akaunti watu maskini wa vijijini wasio na ardhi akawaahidi kuwapa mashamba makubwa kwa kunyang’anya mashamba ya wazungu walowezi na kwa kuwa wazungu hawa waliruhusiwa kulima na kufanya shughuli zao bila shaka walikuwa hawakuwahi kusumbuliwa hapo kabla.

Lakini mzee Mugabe akasahau kwamba anahitaji fwedha ya kuwekeza kwenye mashamba mapya ya wazimbabwe asilia kwani palihitajika mashine,elimu na ujuzi wa kulima kuweza kuzalisha chakula kwa uchumi na ulaji.

Kwa pamoja sera za biashara huria za IMF na ushirikiano kutoka ZANU-PF na sera zake zisizoeleweka, Zimbabwe leo imefikia hapo ilipo, na nchi hiyo inatapatapa isijue nini cha kufanya.

Mzee Robert Mugabe bado anataka kuendelea kuwa Kamuzu Banda mwingine.

Mimi nafikiri Mzee Mugabe inabidi afikirie Zimbawe baada ya yeye.Je wewe unafikiriaje.
 
Richard,
Ya Zim kwa sasa inasikitisha- Wakubwa US na UK wasipokupenda hata ufanyeje you will go! Angalia Nkurumah 1966! Kwa hiyo sioni la ajabu Zim kwa sasa!
On a serious note, Mugabe amezeeka angewaachia tu vijana, miaka 27 madarakani kwa mtu mmoja at 83 years inatosha!
Hope mazungumzo ya sasa through SADC yataleta ahueni over matatizo ya Zim. SADC summit Lusaka this August will discuss Zim.
 
Zimbabwe sugar stampede kills two



Soma hapa

Kwa kweli hii ni laana sijui huko Lusaka kama mambo yatakuwa mazuri?
 
1. Halafu nimekuwa nasikiliza BBC J'borg Wazimbabwe wakimbizi kama 1,000 wanalala kanisani la Methodist na kila siku kanisa hupokea kama 20 new Zimbabweans!

2. SADC took so long to intervene- now it is too late! Hope something good will come out of Lusaka meeting!
 
....27 yrs in presidency/ huyu jamaa need to go no matter what, si aondoke tuu na asipoondoka watamwondoa kwa nguvu sasa,na sio kila kitu anatukumbushia eti alikuwa freedom fighter 40 yrs back wengine hata kuzaliwa ilikuwa bado,he screwed up big lakini still yupo tuu...kachanganyikiwa kama banda naona!
 
1. My problem ni kama ndani ya Zim wenyewe watamwondoa! Sijua hawa viongozi- if he feels unpopular sii tu angeachia ngazi mapema by 2000 yote haya yasingetokea! Huyu mzee bwana!

2. Sasa ukishakuwa na watu over 3 million ktk kipindi kifupi wamekimbia nchi yako- sii bora tu akahamua kuwaachia vijana? Tatizo mzee huyu haambiliki! Now he can not blame UK and US any longer- wakati wananchi wake wanateseka hivi!
 
Govt Splurges U.S. $1.5 Million to Defend Price Blitz

Zimbabwe Independent (Harare)
NEWS
17 August 2007
Posted to the web 17 August 2007





Resources diverted for the sake of outside world. We have got big problems with our leaders and a long way to go. They can only smile.
 
Australia bans 'Mugabe students'



Soma Hapa

Good action and a big YES for the Australians.
 

Mzee Koba, Bob si Baba wa taifa lao?, hata baba wa taifa letu alitutawala miaka kadhaa "tukaridhika"!... Wa Zim wanafuata nyayo zetu, ipo siku nao atatokea "Mzee Ruksa" wao!

Mzee Bob Mugabe si alikuwa anaishi pale Chang'ombe, na miaka yote ile mpaka walipojipatia uhuru 1980(?) alikuwa anatuona na maazimio yetu ya arusha, mara tunavyojifunga mikanda! ...

NASI KWA KUSAHAU!!! ha ha...
 
Do you think this can happen in Tanzania?

though not to the extent ya hawa watani!

Unakumbuka pale karibu na soko la kisutu miaka ile ya 1970's kulikuwa na biashara imeshamiri sana ya dada zetu toka kabila la kule magharibi walokuwa wanajiuza usiku? hata Morogoro nilipoishi miaka ya 1980's kulikuwa na shamba street!!!

Mbona nasi tushapanga sana foleni ya Sukari Gulu, Sembe la njano, nyumbani kwa balozi wa nyumba kumi, tena na daftari lako mkononi, ambalo limeorodheshwa nyote mnaoishi katika nyumba hiyo, Chakula kwa mgao, ukikosa zamu yako, ujue ndio mpaka wiki ijayo!!!

Mbona nasi tushapigana sana vikumbo kugombea kununua mkate tu, (Wa Siha), foleni inaanzia saa saba mchana, unakuja kununua mkatae kumi na moja jioni?...tena wala sio mbali, miaka ya 1980's tu hapo...

Mbona tushapanga sana foleni ya petroli na dizeli, tena unakadiriwa kwa wikilita zako 20 kwa mfano, tena jumapili baada ya saa nane usiendeshe gari lako mpaka jumatatu asubuhi!!!

Shopping ilikuwa duka la michezo Zanzibar, Nairobi au Mombasa, ndio unavaa BATA brand trainers, lasivyo Safari Boot ya Bora nawee wewe na Safari Boot!!! kama usipopigia mswaki jivu, unakuwa umeuchinja kwa ukiletewa zawadi ya Colgate moja, Imperial leather, lux na Omo,...tena unavificha kweli kweli pale Namanga au Airport, maana ukikamatwa navyo...!!!

Wakati huo ulifikia kuna baadhi ya wananchi Tanzania hii hii walivaa magunia!!! leo hii kwa sera za mzee Ruksa angalau utamkuta mtu angalau na tshirt-Mtumba ya Barcelona hata huko Mahuta Shimoni-Newala!!!

We've been there Mzee, na wala usiombee hali ile irudi tena maana....!!!

Uzuri wetu wadanganyika hatuchelewi kusahau!!!
 

Inanikumbusha enzi zile Vijana wa Kitanzania wana cross Boarder kwa Boarder kwenda kutafuta meli!!!.

au kina Kisoda waloteka ndege ya ATC kwa embe, ...hili embe embe, dodo!!!

Guys, hawa jamaa wapo katika kipindi cha mpito, they'll pass thru this period na watakuja inuka tena, si unakumbuka ule msemo wa
"Nyoka huyo, yu wapi na apite tu"?

TATIZO NI KUTOKUJIFUNZA KATIKA KIPINDI KAMA HIKI!
 
Unajua weakness ya baadhi yetu hasa tuliodanganywa na wanasiasa ni kuwa, Wazungu na wabaya na weusi ni wazuri. Najua hapa kwenye Jambo ukiuliza watu who is good for the people of Zimbabwe between Ian Smith and Bob, wengi wanaweza kusema Bob. Siwezi kushangaa, mimi napinga binafsi naweza kusema Ian was much much better in many respects compared to Bob. Angalia Bob alivyoivuruga nchi, sasa hivi Wazimbabwe wanakula Panya balada ya nyama ya ng'ombe ambayo hata watu wa Arusha tuliweza kuila.
Alichukua nchi kutoka kwa Smith ikiwa na heshima kubwa, unemployement was very low, economy was robust, watu walikuwa wanakimbilia kwenda Zim, sasa hivi watu wanakimbia nchi.
Sasa hivi hata ukimuona mwenyewe anavyoonekana unaweza kuona tu ni kweli yanamsubiri kama ya kamuzu Banda. Moja ya mambo yaliyonifanya nisimwelewe BWM ni kumuunga mkono Bob, i wonder what was in Ben mind? Bob hafai kwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…