Zimbabwe situation Live

-Juzi nilifurahi kweli pale finance minister wa Zimbabwe,Tendai Biti alipokata kutoa fedha kutoka hazina kwa ajili ya birthday ya Mugabe.safi sana
 
Anachofanya Mugabe kwa wazungu mimi namuunga mkono kwa 100% ila wengi hatujui what is happening in Zimbabwe, yeye amekataa kuwa Savimbi wa Zimbabwe wazungu walimtumia Savimbi kuivuruga Angola ili wavune madini ya shaba yalipokwisha wazungu wakamwona Savimbi kama takataka wakamtolea ulinzi

Mugabe alipoingia madarakani akakataa kuwa mshirika wa waingereza akawanyanganya mashamba wakakasirika wakaanza kumwekea vikwazo hadi Zimbabwe ikawa nothing from something

wazungu hao hao wakaanza propaganda kuwa mateso wanayopata wazimbabwe yanasababishwa na wao kuondolewa kuitawala Zimbabwe yanasababishwa na Mugabe wakaanza propaganda za kuinyima Zimbabwe opportunities za kimataifa kama misaada nk

Zimbabwe ikawa hohehahe wazungu leo ndio wameanza kusema tatizo ni Mugabe lakini ukiangalia kiundani source ni wao ukiachilia mbali matatizo ya viongozi wengi wa kiafrika.
 
Luteni,wananchi walimkataa kwenye kura,ndio tatizo lilipoanza.Look,Kaunda aliloose uchaguzi akakubali though alikuwa founding father of zambia.Mugabe anaona kuwa Zimbabwe ni kama mali yake.

Yes,Wazungu wana hypocricy,at the same time jiulize 30 yrs in power,unataka nini?????
 
hali ya EA (Kenya, Tanzania na Uganda), almost zinafanana au Tanzania imezidi kidogo in term of rushwa na ufisadi, lakini swali la kujiuliza mbona hao Waingereza hawaipigii kelele Tanzania au Uganda, Jibu la kenya ni sawasawa na la Zimbabwe, hizo nchi ni za masettler, kwa Africa Ukiigusa Zim na Kenya ni Kuigusa Uk moja kwa moja,
hivyo vikwazo walivyowekewa viongozi wa Kenya viliwapasa wakina Mkapa, Chenge na genge lao lote kwa sababu Waingereza ndio wenye kujua hizi issue za ufisadi wa Rada kuliko hata sisi, lakini wako kimya kabisa
WACHA1 ndugu yangu jitahidi sana kuijua siasa ya dunia na uwe makini sana na hivi vyombo vya habari vya Magharibi, vipo hapo kwa maslahi yao zaidi
 
Zimbabwe kitu gani, nyie watu mnaoishi mijini mnajifanya kusikitikia Majirani zenu wakati wapwa zenu wanakufa na njaa kama mbwa!!!! nani asiyeona maisha magumu wanayoishi watu wa Tanzania, Nani asiyejua kuwa ni asilimia 30 peke ya watanzania wenye uhakika wa Mlo wa mwaka mzima? Nani asiyejua kuwa kuna watanzania haawataki kuskia mtoto wake kafaulu shule? Tusiskitike moshi unaofuka kwa jirani wakati kwetu kunaawaka moto.
 
Kituko nakuunga mkono,Britain ni hypocritical sana.
Baada ya scandal ya RADAR,hawa watu nimedharau sana.Nimekaa na Waingereza na kuwaelewa vizuri.Ndio maana waliweza kuwa na empire kwa sababu ya double face.

Watu kama akina Blair ni modern colonialists,wanajidai kupenda afrika,but in real terms huwa maslahi ya nchi zao kwanza.Suala la RADAR mpaka leo linanikera sana.
Na serikali ya Uk inavyofanya siko zote ni kusupport budget za nchi yetu,maana wanajua watawawin viongozi wetu madarakani kwa contracts etc.

Kama unavyosema ,CCM ni corrupt kuliko Zimbabwe,Kenya na Uganda.Yet Uk govt hailii foul hata siku moja.Magazeti tu ndio yanajitahidi kuandika,nakumbuka ktk ununuaji wa ndege
ya rais wakati ule gazeti la independent uk liliandika kashfa hii,hasa kuhusu mdosi Vithlani.

Nafikiri Ujerumani ilifanya mambo makubwa kuliko Uingerza pamoja na kukaa karibu kipindi sawa.hata jiji la Dar lilikuwa ni masterplan ya wajerumani.angalieni reli.Najiuliza kwa nini mpaka leo viongozi wetu wanawahusudu hawa waingereza?
 
yanayotokea zimbwabwe yanatokea india, brazil , kenya na kwingineko, hakuna jipya this is part of life propaganda tu za bbc
kabisa aisee ulaya mashariki kuna maisha ya dhiki mno, lakini hawaongelei ila kwa sababu ni africa ndo maana wanasema, huu ni ukoloni mamboleo siwezi kuukubhali, hata hapahapa tanzania maisha ni ya dhiki mno, tatizo siyo Comrade mgabe tatizo ni unyonyaji,
 
Fafanua,sijui unazungumza nchi gani ya ulaya mashariki?Huwezi kufananisha nchi yoyote poor ya East Europe na Afrika au India.
Get the facts right!
 
hali ya EA (Kenya, Tanzania na Uganda), almost zinafanana au Tanzania imezidi kidogo in term of rushwa na ufisadi, lakini swali la kujiuliza mbona hao Waingereza hawaipigii kelele Tanzania au Uganda, Jibu la kenya ni sawasawa na la Zimbabwe, hizo nchi ni za masettler, kwa Africa Ukiigusa Zim na Kenya ni Kuigusa Uk moja kwa moja,
hivyo vikwazo walivyowekewa viongozi wa Kenya viliwapasa wakina Mkapa, Chenge na genge lao lote kwa sababu Waingereza ndio wenye kujua hizi issue za ufisadi wa Rada kuliko hata sisi, lakini wako kimya kabisa
WACHA1 ndugu yangu jitahidi sana kuijua siasa ya dunia na uwe makini sana na hivi vyombo vya habari vya Magharibi, vipo hapo kwa maslahi yao zaidi

Naona wewe ndio hufahamu siasa za dunia na huko makini katika kuangalia issues kwa ujumla, ati unaongelea nchi kama Kenya, Uganda etc. Charity begins at home, hivi ulitegemea vyombo vya magharibi vikusaidie wewe uliye bongo au Zimbabwe let alone Africa for argument sake kwanza kuliko wao wenyewe?

Tanzania as a sovereign state kwa nini hatuwazuii mafisadi kusafiri nje kwa kuwanyang'anya hati zao za usafiri?Ati tunasubiri uncle wetu kule EU utufanyie hiyo kazi - I&d^io*t.

Kupanga ni kuchagua kama UK wameamua kupiga kelele kwa ufisadi unaotokea Zimbabwe hilo ni lao, huna uwezo wa kuwachagulia. Hata sisi wakati tuna-support ukombozi kusini mwa Afrika lilikuwa chaguo letu. Mbona Kenya hawakusaidia chochote katika jitihada za ukombozi? Wakati ule sisi Tanzania as a nation tuliwawekea vikwazo SA. Hatukuwauliza UK, USA au nchi yoyote nini cha kufanya?
 
Nafikiri Wacha1 huijui story ya Zimbabwe na UK propaganda ya BBC ni sawa na kutegemea RTD itangaze habari nzuri za vyama vya upinzani Tz ni sawa na kutegemea CNN itangaze habari nzuri za Irani

ni kweli sikatai watu wa Zimbabwe wanapata tabu lakini siwezi ku rely on BBC News kuhusu Zimbabwe hizo propaganda ni za masetra wanaodai kurudishiwa mashamba waliyonyang'anywa na kupewa wananchi wa Zimbabwe

masetra hao kwenye uchaguzi uliopita walichanga mabilioni ya pound kuuangusha utawala wa Mugabe unataarifa kuwa serikali ya Brown ilitoa £3Bil siyo shilingi kwa ajili hiyo na UK haijakanusha hadi leo sasa ulitegemea BBC watangaze nini sasa wakati ni chombo cha serikali

wote tunajua yanayotendeka Zimbabwe lakini ukitaka kujua habari zaidi sikiliza vituo mbalimbali try tu be careful na vyombo kama BBC, CNN,CBN, Sky News ni vya propaganda za nchi za Magharibi, balance na vyombo kama RussiaToday RT, Aljazeera, etc unaweza kupata mchanganyiko mzuri.

Unafikiri sijui story ya Zimbabwe kwa sababu nimekwambia uangalie hiyo documentary au vipi? I mean you become a great tinker and judge somebody because he/she has told you to watch a documentary?

Propaganda? Nini maana ya propaganda, kueneza maneno na vitu vya kizushi na kizandiki ambayo havipo, sasa with your clear mind ile documentary ni ya uongo? Na kila kitu ambacho BBC, CNN, CBN na Sky news ni propaganda. Tuhamie kuangalia Russia today RT ambao miaka ya nyuma walikuwa wanagawa magazeti ya bure ya Urusi Leo au Aljazeera wanao-support bombers na kila uharamia ambao wanapewa fweza za kuendesha kituo chao na BBC, au tubadilike tuwe kama Somalia.

Unaongelea fweza za uchaguzi uliopita ambao ulifanyika, nini £3 billion kwa UK wao si wanachapisha tu na kukwambia hiyo ndio value (refer to the on going recession), Mugabe alitumia ngapi? Mbona basi asiwagawie opposition ili kufanya fare election? Mbona husemi fweza walizotoa UK kwa ajili ya compensation kwa mashamba ya wazungu ili wapewe waafrika. Mbona husemi kwa nini Mugabe alishindwa ku-account billions of £'s alizopewa na UK kufuatia makubaliano ya Lancaster? Mbona husemi jinsi Gukurahundi ilivyowaua innocent civilian people of Zimbabwea? Mbona husemi jinsi 7th Brigade ilivyoua wananchi kule Bulawayo? Mbona husemi mamillioni ya Zimbabweans wanaovuka mpaka kila uchwao kwenda SA kujaribu japo kupata mlo wa uhakika japo moja? Huu ndio naita unafiki - Bob Mugabe juzi tu katumia fweza kibao kwa ajili ya nini kuzaliwa kwake who cares?

Tanzania tusitegemee UK kuwazuia mafisadi kusafiri au kuwachukulia hatua tufanye sisi wenyewe, funga jela Mkapa aliyechukua Kiwira na kufanya biashara Ikulu, weka ndani RA, EL, Chenge, Mramba waliokwiba BOT fweza za EPA au kurudisha na wahujumu wote wa uchumi. Whats happening in Zimbabwe can happen anywhere in the region. We are a sovereign State lets flush the mafisadi once and for all na sio kulialia tu kila siku or BBC, SKY et al hawatupendi? Sisi wenyewe hatujipendi.
 
Luteni,wananchi walimkataa kwenye kura,ndio tatizo lilipoanza.Look,Kaunda aliloose uchaguzi akakubali though alikuwa founding father of zambia.Mugabe anaona kuwa Zimbabwe ni kama mali yake.

Yes,Wazungu wana hypocricy,at the same time jiulize 30 yrs in power,unataka nini?????

Unauliza miaka 30 ya Zimbabwe in power mbona hujiulizi miaka 48 ya uhuru wa Tanzania tumefanya nini kuwazidi wazimbabwe

matatizo ya wazimbabwe hayakuanza juzi baada ya uchaguzi ni ya muda mrefu hayo unayoyaona ni baadhi tu ya matokeo ya siasa za nje za UK zilizopandikizwa na Blair towards Zimbabwe walichofanikiwa ni kuua uchumi wa Zimbabwe na kuanzisha chokochoko za kisiasa

walishindwa kuitawala Zimbabwe kisiasa miaka ya 80s badala yake wanataka waendelee kuitawala kiuchumi sababu UK inategemea sana mazao ya mashamba ya masetra hasa mahindi kutoka Zimbabwe
 
Unafikiri sijui story ya Zimbabwe kwa sababu nimekwambia uangalie hiyo documentary au vipi? I mean you become a great tinker and judge somebody because he/she has told you to watch a documentary?

Propaganda? Nini maana ya propaganda, kueneza maneno na vitu vya kizushi na kizandiki ambayo havipo, sasa with your clear mind ile documentary ni ya uongo? Na kila kitu ambacho BBC, CNN, CBN na Sky news ni propaganda. Tuhamie kuangalia Russia today RT ambao miaka ya nyuma walikuwa wanagawa magazeti ya bure ya Urusi Leo au Aljazeera wanao-support bombers na kila uharamia ambao wanapewa fweza za kuendesha kituo chao na BBC, au tubadilike tuwe kama Somalia.

Unaongelea fweza za uchaguzi uliopita ambao ulifanyika, nini £3 billion kwa UK wao si wanachapisha tu na kukwambia hiyo ndio value (refer to the on going recession), Mugabe alitumia ngapi? Mbona basi asiwagawie opposition ili kufanya fare election? Mbona husemi fweza walizotoa UK kwa ajili ya compensation kwa mashamba ya wazungu ili wapewe waafrika. Mbona husemi kwa nini Mugabe alishindwa ku-account billions of £'s alizopewa na UK kufuatia makubaliano ya Lancaster? Mbona husemi jinsi Gukurahundi ilivyowaua innocent civilian people of Zimbabwea? Mbona husemi jinsi 7th Brigade ilivyoua wananchi kule Bulawayo? Mbona husemi mamillioni ya Zimbabweans wanaovuka mpaka kila uchwao kwenda SA kujaribu japo kupata mlo wa uhakika japo moja? Huu ndio naita unafiki - Bob Mugabe juzi tu katumia fweza kibao kwa ajili ya nini kuzaliwa kwake who cares?

Tanzania tusitegemee UK kuwazuia mafisadi kusafiri au kuwachukulia hatua tufanye sisi wenyewe, funga jela Mkapa aliyechukua Kiwira na kufanya biashara Ikulu, weka ndani RA, EL, Chenge, Mramba waliokwiba BOT fweza za EPA au kurudisha na wahujumu wote wa uchumi. Whats happening in Zimbabwe can happen anywhere in the region. We are a sovereign State lets flush the mafisadi once and for all na sio kulialia tu kila siku or BBC, SKY et al hawatupendi? Sisi wenyewe hatujipendi.

Wacha1 nashukuru kwa kunisaidia kwenye hoja yangu kuwa tusiishie kuangalia habari na picha za BBC na CNN tu na kuchukulia walichosema ni cha ukweli ujue hizo documentary zinatengenezwa na watu kwa ajili ya biashara na maslahi yao hata wewe ukiwa na picha watakayoipenda watainunua na kuitumia kwenye documentary yao

hizo picha za watoto walionyong'onyea hata hapa Tanzania zipo kama wakitaka kutengeneza documentary kuhusu hali hiyo(kwa maslahi yao) kwamba inatokea Tanzania wanaweza elewa kuwa CNN na BBC ni vyombo vyao vya kufanyia propaganda za kimataifa ukitaka kuwafahamu zaidi sikiliza counterpart wao kama RT na Aljazeera nao vile vile si wakuwaamini kwa 100% vyombo vyote huvutia upande wao lakini kama uko makini utachambua usifyonze kila kitu kama dodoki

umesahau wakati wa vita vya Iraki CNN na BBC walivyokuwa wanasema Iraki ina WMD hadi vikafanikiwa kuiteka dunia na UN lakini hadi leo hizo WMD umeziona? leo Blair mwenyewe yuko kwenye heat aeleze kwa nini aliudanganya ulimwengu the same is happening for Zimbabwe lakini hawatakuja wafanikiwe sana sana ni kuwaumiza wananchi wa kawaida.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom