Zimbabwe kununua Korosho za Tanzania

Zimbabwe kununua Korosho za Tanzania

View attachment 1114168
Baada ya Zimbabwe kuonyesha nia ya kununua mahindi na mazao mengine kiasi cha 800,000 kutoka Tanzania, taifa hilo la Kusini mwa Afrika linafikiria pia kuanza kununua mazao mengine kama korosho.

Ujumbe kutoka Serikali ya Zimbabwe utawasili nchini kuanzia siku ya Jumanne ya Tarehe 3 Juni na unatajiwa kuwa nchini mpaka tarehe 7 ya Mwezi Juni.

“Ujumbe huo unakuja kwa ajili ya kuangalia na kujiridhisha kuhusu mambo ya msingi kama ubora wa chakula na mambo mengine ya awali,” Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameyasima hayo jana wakati wa kikao cha dharura na wakurugenzi wa taasisi na idara mbalimbali za Wizara ya Kilimo.

“Zimbabwe imefikiria pia kuanza kununua mazao mengine kama korosho kwa kuwa imeona fursa ya kupata mazao yenye ubora na kwa bei nzuri ipo Tanzania. Baadae mazao mengine ya mbegu za mafuta, jamii ya mikunde, mboga na matunda yataanza kununuliwa na taifa hilo,” aliongeza Waziri Hasunga.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la kuanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kuiuzia nchi ya Zimbabwe mahindi na mazao mengine kiasi cha Tani 800,000.
Seriously Zimbabwe wanunue Korosho ya Tz wafanye nayo nini?
Is this a joke or what?
Wanashindwa kula milo mitatu kwa siku ndio wawe na pesa ya kununua Korosho kweli?
Hii serikali ina utani na wakulima wa Tz
 
Pole pole leo kasema tutagawana korosho zetu endapo hazitauzika...... Naomba Zimbabwe washindwe heri tupewe kg mbili zetu kila mmoja
Huyu Mzee kijana anaongea swala la Korosho yeye kama nani?
ccm mnacheza na maisha ya watu mjue
Mzee kijana kaa lumumba usituvuruge
Umeshakuwa mchumi mara hahahh Hii nchi ujinga kama wote
 
Itabidi ijengwe reli kwa ajili kusafirishia shehena ya hela toka zimbabwe
Taarifa nyingine zinasema kuwa msafara wa raisi umegundua viwanda vya kubangua korosho huko Zimbabwe.
 
Hivi kile kitabu cha Kusadikika bado kipoga, mwenye nacho aniazime nisome huu ukurasa wa kununua korosho zetu.
 
Itabidi ijengwe reli kwa ajili kusafirishia shehena ya hela toka zimbabwe
...hahahaaaa watatuma bombadia kusomba izo pesa za mauzo...au tutatuma maroli ya wajeda yakasombe izo noti. Nimeamini msemo wa babu yangu chizi ata ukimvalisha suti atajinyea humo humo sijui babu alikua anamaanisha nini kuniambia hivyo
 
India na Vietnam ni wanunuzi wakubwa wa korosho kutoka Africa,na wao ni global supplier s Ulaya ambako mahitaji ya korosho yanazidi kuongezeka kila siku.Brazil wao wanauza USA.Kuongezeka kwa matumizi ya Korosho Ulaya ni opportunity nzuri ya wakulima
Kutoka developing countries kuuza bidhaa hii kwenye hizo nnchi.Netherlands,German,UK,Central and Eastern Europe huko kote kuna fursa ya kuuza korosho kwa Sababu ya ongezeko ya matumizi yake.Kabudi ajimwage na Negotiations skills zake watu wapate tenda..Au akajifunze kwa wa Nigeria huko..Wauzaji wazuri wa Korosho.Zimbwabwe Mahindi yes,Wana exports Iwisa Unga wa Saza.(Ugali)
 
Yaani ningekuwa naweza ningeweka audio yake hapa kanitia hasira mno leo kaja mtwara kutwambia mambo meusi
Huyu Mzee kijana anaongea swala la Korosho yeye kama nani?
ccm mnacheza na maisha ya watu mjue
Mzee kijana kaa lumumba usituvuruge
Umeshakuwa mchumi mara hahahh Hii nchi ujinga kama wote
 
View attachment 1114168
Baada ya Zimbabwe kuonyesha nia ya kununua mahindi na mazao mengine kiasi cha 800,000 kutoka Tanzania, taifa hilo la Kusini mwa Afrika linafikiria pia kuanza kununua mazao mengine kama korosho.

Ujumbe kutoka Serikali ya Zimbabwe utawasili nchini kuanzia siku ya Jumanne ya Tarehe 3 Juni na unatajiwa kuwa nchini mpaka tarehe 7 ya Mwezi Juni.

“Ujumbe huo unakuja kwa ajili ya kuangalia na kujiridhisha kuhusu mambo ya msingi kama ubora wa chakula na mambo mengine ya awali,” Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameyasima hayo jana wakati wa kikao cha dharura na wakurugenzi wa taasisi na idara mbalimbali za Wizara ya Kilimo.

“Zimbabwe imefikiria pia kuanza kununua mazao mengine kama korosho kwa kuwa imeona fursa ya kupata mazao yenye ubora na kwa bei nzuri ipo Tanzania. Baadae mazao mengine ya mbegu za mafuta, jamii ya mikunde, mboga na matunda yataanza kununuliwa na taifa hilo,” aliongeza Waziri Hasunga.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la kuanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kuiuzia nchi ya Zimbabwe mahindi na mazao mengine kiasi cha Tani 800,000.

Sina hata cha kusema
 
Hivi hawawezi kufanya mambo kimya kimya ili hata yakiharibika hakuna anayejua, hizi kiki, haziwafikishi popote, ni bora tu muendelee na maandalizi yenu ya kuiba kura na kupora ushindi, Ila mjue kuwa siku zinatofautiana na watu pia wanachoka.
 
Zimbabwe wanunue korosho wazipeleke wapi?kweli tunamawaziri wapuuzi kweli ambao hawajui hata wafanye nini.
Yaani muda wote wanakaa ofsini kujadili ZIM watanunua korosho kweli hii serikali iko mbioni kuanguka tena bila kusukumwa.
Zim hata wakinunua bado currency yao haina thamani
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hii ni sawa na mtoto mchanga kunyonyesha badala ya kunyonya!
 
Rais alisema korosho zote zitabanguliwa lazima tuuze zkiwa processed na alitumia nguvu kubwa kuuaminisha uma juu ya hili hapa je tutauza zkiwa zmebanguliwa Au la

Kitu kingne rais aache kutuongopea alisema Kuwa wahabeshi watatumia bandari yetu je hili suala limefikia wapi?

Mwisho watetezi wa rais kwa awamu hii mnakaz nzito Sana kutueleza sis wananchi juu ya matamshi ya rais ukweli n kwamba tuna hali ngumu sna huku mtaani mwambien ukweli hali n ngumu
 
Zimbabwe wanunue korosho wazipeleke wapi?kweli tunamawaziri wapuuzi kweli ambao hawajui hata wafanye nini.
Yaani muda wote wanakaa ofsini kujadili ZIM watanunua korosho kweli hii serikali iko mbioni kuanguka tena bila kusukumwa.
ni vyema kufanya biashara na nchi zenye rika letu, tunaweza kuwa na uhuru wa kuongea biashara na mazingira rafiki ya kibiashara, Zimbabwe tuwauzie Korosho Sembe mchele Ngano ya Bakhresa, mbaazi maharagwe Vitenge khanga samaki na bidhaa zozote rafiki. Tuangalie uwezekano wa CRDB EXIM bank kwenda kufungua matawi Zimbabwe na Namibia, ndege zetu ziweze kwenda Zimbabwe na Namibia, wanafunzi wa huko waje kusoma vyuo vikuu vyetu. Huu ni mwanzo mzuri wa kufungua fursa za kibiashara baina ya nchi za Africa.
 
Seriously Zimbabwe wanunue Korosho ya Tz wafanye nayo nini?
Is this a joke or what?
Wanashindwa kula milo mitatu kwa siku ndio wawe na pesa ya kununua Korosho kweli?
Hii serikali ina utani na wakulima wa Tz
Kwani wanaozinunua wao huzifanyia nini? tusiwe na mawazo mgando kudhani biashara ni lazima ufanye na china us uk india brazil, tunaweza fanya na congo Zimbabwe Uganda kenya angola. Hebu tu use Africa market to the maximum kabla ya kuwaza mambo mengine ya juu Zaidi.
 
Hii serikali ya awamu ya tano korosho zitawatesa sana. Korosho ni zao ambalo Zimbabwe hawana uwezo wa kununua ili watafute soko na wananchi wake ni masikini kifedha kuamua kula korosho kama kiburudisho au kujenga siha zao.

Zimbabwe
image

Market Shares in global exports
NaN%Ranked 142nd
Market Shares in global imports
0.0%Ranked 130th

Market Intelligence of Cashew Nut in Zimbabwe

Source : https://www.tridge.com/intelligences/cashew-nut/ZW
 
Back
Top Bottom