Kijakazi: inahitaji roho ya bata kutetea yale anayoyafanya Mugabe kwa watu wa Zimbabwe. Hata hivyo huhitaji kuishi Zimbabwe kutambua kwamba Mugabe is the worst dictator that Africa has ever had. Mtu anayeua watu unataka afanye mabaya kiasi gani ndiyo uone kwamba ni hatari na hafai?
wewe kitila mfwata mkumbo una matatizo, ni wapi nilipoandika kuwa namtetea Mugabe? hivi umesema posti yangu vizuri na kuielewa kabla ya kujibu? kumbuka sijakulazimisha ujibu hoja kama hauielewi... kwa maana unaanza kupindisha maneno...mimi nimejaribu kutoa usambamba wa yale yanayotokea zimbabwe na iraki na nilitegemea wewe ujibu kufwatana na hivyo....
unasema mugabe ni dikteta mkubwa hajawahi tokea afrika, Je una uhakika na unayosema sema?
Je unajua kagame kaua wangapi rwanda na kongo... unajua museveni kaua na anua wangapi mpaka leo mbona hakusikii kuhusu hawa....
unajua nchi inaitwa equatorial guinea... unajua kinachoendela huko?
je unajua kwamba zimabwe karibu asilimia 50 ya wabunge ni wapinzani? sasa walichaguliwa vipi kama mugabe ni dikteta hivyo....
hivi unaelewa maana ya hilo neno au unaongea tuu...ktk nchi gani ya kidekta ambapo ucahguzi unarudiwa kwa sababu hakuna mtu aliyepata zaidi asilimia 50..., mugabe angekuwa ni katili kama unavyomfikiria cahngarai asingeishi zimbabwe, nchi zote zenye madikteta wapinzabi wanaongeleaga nje ya nchi lkni changarai yupo zimbabwe na anafanya kampeni......
kwa kifupi nilichotaka kusema ni kwamba siku zote jaribu kwanza kuelewa mambo kabla hujaanza kutoa hukumu jiulize maswali kwanza... kama ni umaskini kama nilivyosema watanzania leo hii bado maskini zaidi ya wazimbabwe kwanza ukilinganisha wazimbabwe ktk afrika bado wana ahueni ya maisha kuliko nchi nyingi sana za kiafrika kupita tz, kenya,ug, na nyuma tuu ya botswana,sa namibia basi....
mimi nafikiri wewe ni wale watu ambao mnafwata mkumbo kama jina lako linavyosema na kama kweli ungekuwa na uwezo hata kidogo wa kufikiri ungeweza kujiuliza ni vipi vyombo vyote vya magahribi vinaongelea zimbabwe na sio kongo, uganda, e. guinea, nigeria n.k