Marekani yaombwa kuiondolea Zimbabwe vikwazo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Alhamisi ameiomba Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Zimbabwe akisema kwamba vimeongeza janga la kibinadamu pamoja na kudorora kwa uchumi, wakati akipendekeza kuwepo kwa mashauriano ili kumaliza uhasama uliopo.

Alena Douhan ambaye ni mjumbe maalum wa UN wa masuala yanayohusiana na vikwazo na amekuwepo nchini Zimbabwe kwa karibu wiki mbili sasa wakati akitathmini athari zitokanazo na vikwazo vya Marekani kwenye taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Marekani iliweka vikwazo vya kifedha na vya kusafiri kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa na kijeshi pamoja na wafanyabiashara yakiwemo makampuni yanayohusishwa na serikali, takriban miongo miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AP hatua hiyo ilichukuliwa baada ya wakulima wa kizungu kupokonywa mashamba yao pamoja na wizi wa kura na ukiukaji wa haki za binadamu kutoka kwa kiongozi wa muda mrefu marehemu Robert Mugabe.

Ubalozi wa Marekani mapema wiki hii umesema kwamba unaweza kuondoa vikwazo hivyo baada ya kuthibitisha kwamba watu waliowekewa wameacha kuhujumu demokrasia, kushiriki ufisadi pamoja kukiuka haki za kibinadamu.
 
Sasa kuwekea nchi vikwazo sababu ya viongozi wenye uwezo wa kuishi watakavyo huku wananchi ndio wakiwa wahanga nayo sio kukiuka haki za binadamu?

Kosa la viongozi adhabu ya wananchi halafu unasema unatetea haki za binadamu kweli?
Marekani na washkaji zake wauaji wakubwa.
 
Mjitegemeee,
Ukianza harakati za kujitegemea unaanza kupata upinzani kutoka ndani ya nchi yako na wananchi wenzio ndio watakaotumika kukuua ili maisha ya wabinafsi yaendelee.

Africa tunahitaji ukombozi wa fikra na utaifa kiasi kikubwa mnoooo.

Tizama Libya walisema adui Yao Ghadafi, wamemuua lakini nchi haina progress Tena.
Sudan adui Yao Al Bashir leo hayupo lakini mapinduzi na vurugu zimeshamiri
Zimbabwe tatizo walisema ni Mugabe, miaka mingapi tangu afe lakini vikwazo bado vipo
Sudan kusini walitaka Uhuru, wako huru Nini kinaendelea
Chad, Africa ya Kati, nk

Afrika hatuhitaji kuvushwa stage na demokrasia ya Marekani, tuna changamoto za kifamilia za njaa zaidi kuliko uhitaji wa madaraka ya wachache...
 
Kuna baadh ya waafrica hushangilia vikwazo
 
Sasa kuwekea nchi vikwazo sababu ya viongozi wenye uwezo wa kuishi watakavyo huku wananchi ndio wakiwa wahanga nayo sio kukiuka haki za binadamu?
Kosa la viongozi adhabu ya wananchi halafu unasema unatetea haki za binadamu kweli?
Marekani na washkaji zake wauaji wakubwa.
aise!! Ila nisikushangae Hama hapo lumumba
 
Ukianza harakati za kujitegemea unaanza kupata upinzani kutoka ndani ya nchi yako na wananchi wenzio ndio watakaotumika kukuua ili maisha ya wabinafsi yaendelee.

Africa tunahitaji ukombozi wa fikra na utaifa kiasi kikubwa mnoooo.

Tizama Libya walisema adui Yao Ghadafi, wamemuua lakini nchi haina progress Tena.
Sudan adui Yao Al Bashir leo hayupo lakini mapinduzi na vurugu zimeshamiri
Zimbabwe tatizo walisema ni Mugabe, miaka mingapi tangu afe lakini vikwazo bado vipo
Sudan kusini walitaka Uhuru, wako huru Nini kinaendelea
Chad, Africa ya Kati, nk

Afrika hatuhitaji kuvushwa stage na demokrasia ya Marekani, tuna changamoto za kifamilia za njaa zaidi kuliko uhitaji wa madaraka ya wachache...
Unawalaumu wazungu wakati viongozi wetu ndio chanzo cha haya yote yanayotokea.

Mugabe aliwatimua wazungu akatuaminisha waafrika kuwa mashamba watapewa wananchi wakaida, kinyume na matarajio yale mashamba waliyopokonywa wazungu walipeana viongozi wa serikali na chama(Zanu pf) tu na kama hiyo haitoshi Grace Mugabe amehusika kwenye uporaji wa ardhi za wananchi zilizokuwa zinatumika kwenye kilimo. Mashamba yote waliyopeana hakuna alieyaendeleza ijapokuwa vifaa walikuwa navyo ila maarifa na utayari haukuwepo. Mugabe huyohuyo baada ya kufanya yote hayo bado akataka kumuachia nchi mke wake hadi jeshi lilipoingilia kati na kutolewa madarakani.

Al Bashir alikuwa dikteta aliewageuza aliewageuza wananchi wake kuwa wafungwa wa nje. Kaongoza muda mrefu nchi ikiwa na vikwazo na ilikuwa wazi asingweza kuiletea mabadiliko yoyote chanya, busara ilikuwa kuondoka lakini akawa muuaji wa wanaomkosoa.

Gadaffi alikuwa dikteta aliewasupport madikteta wenzake kama Iddi Amini, mminyaji wa haki na demokrasia nchini kwake(alikuwa anawaua wapinzani wake kwa kuwanyonga mbele ya halaiki bila kwenda mahakamani na wengine walipotea tu)lakini kuna mabadiliko kadhaa aliyaleta pia.

Hao wote walitolewa na wazungu kwa kwenda kinyume nao lakini pia wananchi wa hizo nchi waliwachoka pia sababu ya ubinafsi na roho mbaya zao.

Na Unaposema Afrika hatuhitaji kuvushwa stage na demokrasia ya Marekani unamaanisha nini hasa? changamoto ulizotaja hapo zinaweza kutatuliwa kwa njia gani?
 
Sasa kuwekea nchi vikwazo sababu ya viongozi wenye uwezo wa kuishi watakavyo huku wananchi ndio wakiwa wahanga nayo sio kukiuka haki za binadamu?

Kosa la viongozi adhabu ya wananchi halafu unasema unatetea haki za binadamu kweli?
Marekani na washkaji zake wauaji wakubwa.
Wakati wa Apartheid, OAU, UN pamoja na mataifa mengi tu duniani na hata wananchi wenyewe wa Afrika Kusini, hasa waafrika weusi waliunga mkono serikali ya makaburu wawekewe vikwazo vikali vya kiuchumi pamoja na kwamba waathirika wakuu hawakuwa makaburu bali wananchi wenyewe wa Afrika Kusini.

Sijui kama unalielewa hilo au hakukuwepo dunia hii wakati huo. Vikwazo vinapoiathiri nchi hata watawala hua hawapati usingizi na ndio maana wenyewe ndio wanakuwa mstari wa mbele kudai viondolewe.
 
Ukianza harakati za kujitegemea unaanza kupata upinzani kutoka ndani ya nchi yako na wananchi wenzio ndio watakaotumika kukuua ili maisha ya wabinafsi yaendelee.

Africa tunahitaji ukombozi wa fikra na utaifa kiasi kikubwa mnoooo.

Tizama Libya walisema adui Yao Ghadafi, wamemuua lakini nchi haina progress Tena.
Sudan adui Yao Al Bashir leo hayupo lakini mapinduzi na vurugu zimeshamiri
Zimbabwe tatizo walisema ni Mugabe, miaka mingapi tangu afe lakini vikwazo bado vipo
Sudan kusini walitaka Uhuru, wako huru Nini kinaendelea
Chad, Africa ya Kati, nk

Afrika hatuhitaji kuvushwa stage na demokrasia ya Marekani, tuna changamoto za kifamilia za njaa zaidi kuliko uhitaji wa madaraka ya wachache...
Libya kuna nini hata uitolee mfano?.
kuhusu Zimbabwe:, vikwazo viliwekwa kwa ajiri ya Zimbabwe na sio Mugabe.
Mugabe hakuwa Zimbabwe ndiyo maana amekufa(hayupo) ila Zimbabwe bado ipo na itaendelea kuwepo.
Zimbabwe ilipaswa imkate Mugabe mapema baada ya kuona ana haribu nchi kwa kutaka sifa za kipumbavu lakini wakaa kimya. na kwa kuwa Mugabe alikuwa ni chongo kwenye nchi ya vipofu akaajiri watu kalba ya akina jingalao hao kazi yao ni kutetea kila uovu wa Mugabe.
Nb:
ikiwa watu wa kalba ya akina Mugabe, Magufuli Gaddafi ndiyo Mashujaa wenu mjue ndiyo kwanza mmeanza safari km tilion 1 kwa kutumia usafiri wa tera la punda.
 
Back
Top Bottom