mtoto wa mchungaji
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 279
- 480
Nashindwa kujizuia hili jamaa kuliita Dume na Mwamba wa Afrika
Tuliambiwa kuwa Idi Amini alikuwa dicteta wa hatari, anakula watu, anakula damu za watu na mambo mengi yanayofanana na hayo lakini siku zinavyozidi kwenda inakuwa tofauti sana. Baba zetu na mama zetu walimuimba sana mashuleni zikiwemo nyimbo za kuudhi kutusi na kashfa za namna kwa Idi Amini Dadaa, Mbio za mchaka mchaka zilikuwa zake pekee wakati ule.
Je, hili dume kweli lilikuwa linakula watu, linakula damu za watu na dicteta?
Baadhi ya mambo niliyoyaona yanashangaza na hayafananini na tuliyo ambiwa. Kwamfano katika kipindi chake cha uongozi Idi Amini Dadaa kuanzia 1971 mpaka 1978 aliupandisha uchumi wa nchi yake kuwa juu ya nchi zote za Afrika mashariki na hata fedha ya Uganda ilikuwa juu ya Tanzania na Kenya kithamani ikichuana na ile dola ya Zimbabwe ya wakati ule.
Alibadilisha jina la Kwini Elizabeti Neshino paki kuwa Ruwenzori neshino paki. Alibadilisha Muschoson Fall kuwa maporomoko ya Kabalega
Alibadilisha jina la Ziwa Albart kuwa ziwa Idi Amini
Alibadilisha jina la barabara ya Kwini Eliza kuwa barabara ya Lumumba
Alibadilisha jina barabara ya Salisbury kuwa barabara ya kwame Nkuruma
Mlima Elgon kuwa Masaba
Aliwalazimisha waganda kuongea kiswahili nchi nzima huku yeye akiongea kiswahili kila mahali.
Alikuwa kiongozi wa kwanza wa kiafirka kusema hadharani kuwa uhuru wa bendera hauna maana yoyote kwa muyuganda, bari uhuru wa kiuchumi ndiyo uhuru kamili kwa mutu ya Uganda kwani wakati anaingia madarakani uchumi wote ulikuwa umeshikwa na waingereza, wahindi na waislael.
Aliwai sema kuwa Uganda ni ya waganda na Israel ni ya waisrael na kama Yesu atakataa amuhukumu sasa hivi.
Aliwafukuza wazungu, wahindi na wana wa Israel nchini Uganda kwa kuwapa masaa 24 na nchi ilimilikiwa na waganda wenyewe kwa miaka 9 na uchumi ulikua kwa kasi ya ajabu.
Mi nahisi Afrika kuna tatizo. Na hili nene dikteta tufundishwa maana yake upya linazidi kutupoteza.