Zimbabwe = Iraki

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,841
9,971
Nimesoma kuhusu habari za makampuni ya mafuta ya exxon mobili na bp, wanategemea kurudi iraki kuanzia tarehe 30/6 mwaka huu, na wanategemea kutiliana mkataba na serikali mpya ya iraki, ikumbukwe kwamba makampuni hayo yalifukuzwa na sadamu huseni miaka 35 iliyopita kutoka iraki, sasa hii kutokana na mimi ninavyoiona hii inaonyesha sababu hasa za vita.... kwani sadamu(simtetei) ndiye pekee aliyeweza kusimama na kuwafukuza hawa mashetani maharamia makuma waingereza wakongozwa na malaya wao mwizi mkubwa elizabeti, na wakaanza propaganda kumachafua sadamu kwa kumita dikteta na watu woote (isipokuwa wachache) wakaamini waliyoambiwa na vita ikaanza, sasa matokeo yake tunayaona......
Je kuna mtu anweza kuona uwiano kati ya sadamu na mugabe (simtetei pia)?
ja hamuaoni watu mnaomhukumu mugabe mmedanganywa na hawa mashetani waingereza? Je kama Mugabe asingetaifisha mashamba na kuwafuka wazungu na kuwambatia huyo malaya mkubwa duniani elizabeti angeifanyia zimbabwe anaivyoifanyia?
watu mnao mhukumu mugabe Je mmshawahi kujiuliza kama mnaongea au kutoa hukumu ya yale msioyelewa vizuri na mnashabikia tuu na kumeza kila kitu kama pipa la taka bila hata kutofautisha kati ya takataka na si taka.....
Je hamuamini kwamba siku hawa wezi waingereza wakimtoa mugabe ukweli utajidhihirisha kwa kuanzia kurudi kwa wazungu.....
ni hivi punde nimesoma kwamba serikali ya wezi waingereza imemuahidi changarai dola za kimarekani bilioni 1, kama akingii serikalini ili kurudisha uchumi lkni kwa mashari mengi sana ikiwamo kusimamisha biashara na makumpuni ya china, na kutaifisha rasilimali zote za zimbabwe kwa makampuni ya makachero waingereza....
NIMEANDIKA HII SI KWA WOOTE BALI KWA WACHACHE WENYE UWEZO WA KUFIKIRI KWA KINA KUHUSU HAYO NILIYOYASEMA (usijali matusi) NA KUTOA MCHANGO WAO KAMA WANAONA KUNA UWIANO KATI YA HIZO NCHI MBILI......
 
Hii haiondoi ukweli kwamba Mugabe ni shetani mkubwa kuliko shetani mwenyewe
Je unaufahamu ukweli wa zimbabwe na mugabe?
mugabe ni shetani mkubwa kuliko changarai? unajuaje hilo.....
Je hauoni labda wewe hauelewi kinachoendela huko zimbabwe na unajaribu kutoa hukumu bila kuwa na ukweli wote....
mugabe ni shetani kama unavyosema una uhakika gani... Je ni kwa ajili ya hali mbaya ya kiuchumi inayoendelea sasa hivi zimbabwe?
kama ni hvyo basi napenda kukuuliza Je umeshafika zimbabwe hivi karibuni?
kama hivyo sivyo, Je unafahamu kwamba ukilinganisha hali ya maisha ya mzimbabwe wa kawaida sasa hivi zimbabwe bado ni bora kuliko mtanzania wa kawaida pamoja na yoote unayoyasikia.....
Kama mugabe ni shetani mkubwa kama ulivyomuita na kama sababu ni kuporomoka kwa uchumi, Je nyerere nae ni shetani mkubwa? kwa maana wakati wa utawala wake uchumi wetu pia uliporomoka na mara mia hata ya zimbabwe na watu walikuwa na bado wankula mizizi tanzania je unalijua hilo?
Je unafahamu kuwa tanzani kuna watu wengi wanafanya kazi hasa walimu na polisi na hawajalipwa mishahara kwa zaidi miezi sita? na hilo halijaanzia jana bali liposiku zote sasa kama sababu za ushetani wa mugabe ni uchumi Je kwa nini haumwiti pia nyerere na wengineo mashetani?
kama yoote hayo niliyoyasema hapo juu sii sawa basi weka sababu zako za kumwita mugabe kuwa "shetani mkubwa kuliko wote" kuliko malkia elizabeti na wengineo wengi.....naomba uweke mambo unayoyaelewa nasio kufwata mkumbo kwani nina uhakika wewe una tofauti kubwa na pipa la taka kwani unaweza kupima na kuelewa mambo na sio kuchukua kila unachopewa....
 
My take...Iraqi kuna vita...Zimbabwe bado....Tanzania je?
Ofcourse tunayajali maslahi ya wazimbabwe.
nia hayo tu.
Asante
 
pole sana!! siitaji kufikiri kama unavyofikiri wewe, umekwenda mbali mno ambako utaumiza kichwa chako! WaTanzania au WaZimbabwe priority yao ni chakula na usalama wao kwanza, all what you said are secondary!
sasa kama ni hivyo wewe binafsi unafikiri kufikiri hivyo ni sawa?
Je kama nimekuelewa vizuri unamaanisha kwamba wazungu wakirudi na changarai raisi wakapata chakula na usalama na hali ikarudi kama ilivyokuwa hapo mwanzo kwamba wao wazim ni wafanyakazi tuu wa mashambani na wazungu ndio mabosi maadamu wanapata chakula hilo ni sawa?
sasa kama ni hivyo mugabe hana siku nyingi na mwishowe changarai ataingia alafu tutaona kama maisha ya mzim wa kawaida yatakuwa bora......
 
pole sana!! siitaji kufikiri kama unavyofikiri wewe, umekwenda mbali mno ambako utaumiza kichwa chako! WaTanzania au WaZimbabwe priority yao ni chakula na usalama wao kwanza, all what you said are secondary!

KIJAkazi hadi leo hii Africa nzima wazungu ni ma-boss, tatizo lako lisiwe kuwa ni kuogopa wazungu wawe mabosi. Tunacholilia Zimbabwe siyo Tsvangirai awe Raisi no, ni kuwa Mugabe lazima akubali mabadiliko ya nchi, lazima akubali mtawala mwingine anaweza kuwa rais. Hebu twambie hivi wewe unafikiri ni Tsvangirai tu anayemchallenge Mugabe? Wapo wengi. Simba Makoni, baada ya kusimama kutaka urais through Zanu PF alifukuzwa chama akawa independent. Yale ya Moyo unayakumbuka? Halafu yule mzee anapoambiwa apumzike anatoa matusi ambayo mzee mwenye umri wa miaka 84 kama yeye angekuwa na busara.

What makes you buy that Tsvangirai will bring back whites? What makes you think any president other than Mugabe will not tackle Zimbabwe economic problems? Mugabe is terorising his own people Nyerere never did that! When the signs came he just stepped down; but this tyrany at the age of 84 wants everybody loose. He will loose the country and before loosing it he wants it to be ruined first!
 
Kijakazi: inahitaji roho ya bata kutetea yale anayoyafanya Mugabe kwa watu wa Zimbabwe. Hata hivyo huhitaji kuishi Zimbabwe kutambua kwamba Mugabe is the worst dictator that Africa has ever had. Mtu anayeua watu unataka afanye mabaya kiasi gani ndiyo uone kwamba ni hatari na hafai?
 
Mzee Unaona Mwisho Hacha Hawa Vibaraka Waendelee Kujujikomba Kwa Waheshimiwa Weupe Ili Wapate Kibaba Mawazo Yao Yapo Tumboni Vichwa Vimelala
 
.
Mkumbo Wewe Unajua Remote Iko Wapi Usihofu Scholarship Yako Iko Palepale Sema Ukweli UWE HURU
Prof Dr Ing Tumaini Geofey Temu

i regret if a professor like you thinks abnormal; the worst is even; you are infecting poison to our offsprings; Note; professors are big thinkers!!
 
Kijakazi: inahitaji roho ya bata kutetea yale anayoyafanya Mugabe kwa watu wa Zimbabwe. Hata hivyo huhitaji kuishi Zimbabwe kutambua kwamba Mugabe is the worst dictator that Africa has ever had. Mtu anayeua watu unataka afanye mabaya kiasi gani ndiyo uone kwamba ni hatari na hafai?

wewe kitila mfwata mkumbo una matatizo, ni wapi nilipoandika kuwa namtetea Mugabe? hivi umesema posti yangu vizuri na kuielewa kabla ya kujibu? kumbuka sijakulazimisha ujibu hoja kama hauielewi... kwa maana unaanza kupindisha maneno...mimi nimejaribu kutoa usambamba wa yale yanayotokea zimbabwe na iraki na nilitegemea wewe ujibu kufwatana na hivyo....
unasema mugabe ni dikteta mkubwa hajawahi tokea afrika, Je una uhakika na unayosema sema?
Je unajua kagame kaua wangapi rwanda na kongo... unajua museveni kaua na anua wangapi mpaka leo mbona hakusikii kuhusu hawa....
unajua nchi inaitwa equatorial guinea... unajua kinachoendela huko?
je unajua kwamba zimabwe karibu asilimia 50 ya wabunge ni wapinzani? sasa walichaguliwa vipi kama mugabe ni dikteta hivyo....
hivi unaelewa maana ya hilo neno au unaongea tuu...ktk nchi gani ya kidekta ambapo ucahguzi unarudiwa kwa sababu hakuna mtu aliyepata zaidi asilimia 50..., mugabe angekuwa ni katili kama unavyomfikiria cahngarai asingeishi zimbabwe, nchi zote zenye madikteta wapinzabi wanaongeleaga nje ya nchi lkni changarai yupo zimbabwe na anafanya kampeni......
kwa kifupi nilichotaka kusema ni kwamba siku zote jaribu kwanza kuelewa mambo kabla hujaanza kutoa hukumu jiulize maswali kwanza... kama ni umaskini kama nilivyosema watanzania leo hii bado maskini zaidi ya wazimbabwe kwanza ukilinganisha wazimbabwe ktk afrika bado wana ahueni ya maisha kuliko nchi nyingi sana za kiafrika kupita tz, kenya,ug, na nyuma tuu ya botswana,sa namibia basi....

mimi nafikiri wewe ni wale watu ambao mnafwata mkumbo kama jina lako linavyosema na kama kweli ungekuwa na uwezo hata kidogo wa kufikiri ungeweza kujiuliza ni vipi vyombo vyote vya magahribi vinaongelea zimbabwe na sio kongo, uganda, e. guinea, nigeria n.k
 
Acheni kuumiza vichwa

Matokeo ya uchaguzi ni kwamaba Mugabe atashinda kwa kishindo cha Tsunami.

Dogo wa Upinzani kesha banwa,hawezi hata kupumua hawezi.
 
Kijakazi,
Asante sana kwa hii analysis yako.Mimi huwa kila mara nawaambia watu kuwa ukiwaona waingingereza na wamerekani wameshupalia jambo kuwa ni human rights abuse au violence against humanity na kwamba wao ndiyo wanapush au wanataka kuleta amani think twice kabla ya kuweka kuconclunsion!!!! Mara nyingi huwa ni kutetea interests zao na sio vinginevyo!!

Mtetea haki haangalii au hachagui pa kutetea haki.Mtetea haki atasema na kusimamia haki popote pale duniani bila ya kuangalia nchi ,utawala,kiongozi,imani,dhehebu,rangi au lugha! Mtetea haki asingejiuliza mara mbili au kukaa kimya kuhusu yanaotokea Democratic Republic of Congo,Mtetea haki asingekaa kimya kuhusu yale yanayotokea Equatorial Guinea,Mtetea haki asingekaa kimya kwa yale yaliyotokea kwenye uchaguzi pale Uganda!( pale hata economic sanctions hatukuziona!!),Kenya ndiyo ilikuwa aibu kabisa kwa kuwa Marekani ilijump mara moja na kumtambua Kibaki kuwa ndiyo mshindi ila baadaye wakabadili msimamo wao!..na list hii haina mwisho...inaendelea hata Rwanda kwa Kagame! hii wenzangu ilipasa kutufundisha kuwa ukiwa rafiki wa marekani au uingereza kamwe hutawekewa vikwazo vya kiuchumi au kushutumiwa kwa lolote lile hata kama utakiuka haki za binadamu.Na baya zaidi ukiwa adui au kutokukubaliana na matakwa yao mara moja utakuwa kwenye kila news headline kuwa wewe ni mtu au kiongozi mbaya ambaye hajapata kutokea katika dunia hii au kizazi hiki....

Mimi ningependa kuwajulisha wenzangu hapa kuwa ukishakuwa rafiki wa Uingereza na Marekani kamwe hutaweza kusimamia haki ya raia wako! wao wanakwenda na sera moja kuu nayo ni interests zao kwanza then za wengine ndiyo hufuata hata kama wengine wanauwawa kinyama au kudhulumiwa ardhi au kunyimwa haki zao za msingi! hili nafikiri halina mjadala tumeshaliona mahala pengi tu ulimwenguni.

Ni kweli kuwa Mugabe amekaa madarakani kwa muda mrefu sasa,ni kweli kuwa naye anayo matatizo yake kama viongozi wengi wa afrika ila nilazima tuliangalie kwa mapana zaidi hii issue ya Zimbabwe na siyo kutumbukia kwenye huu mchezo wa Uingereza na Marekani kuwa kiongozi asipokubaliana nao eti basi ni adui wa kila mtu na awekewe vikwazo vya kiuchumi!!

Pili kitendo cha Marekani na Uingereza kuwapatia mamilioni ya fedha wapinzani ili kukaidi sheria za nchi au kuiangusha serikali ya Mugabe hakikuwa sawa na vinapingana na democrasia ya kweli,ilipaswa wao kuwa mstari wa mbele katika kutetea democrasia ya kweli kwa kutoa haki sawa kwa kila upande na siyo kuwarubuni wananchi wale ambao wanateseka kwa vikwazo vya uchumi vilivyowekwa na Uingereza na Marekani.Pia Uingereza na Marekani walipaswa kutimiza ahadi yao ya kulipa fedha ambazo waliahidi kwenye ule mkataba wa ugawanywaji ardhi wa mwaka 1998.

-Wembe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom