BinMgen
JF-Expert Member
- Jun 18, 2008
- 1,854
- 262
Bila kuwasahau Bima Lee Orchestra....Bendi hii ilikuwa ikimilikiwa na Shirika la Bima la Taifa.....Iliimarika zaidi mwaka 1984 baada ya kuwapata wanamuziki kutoka bendi tofauti tofauti walipoletwa kwenye bendi hii kwa lengo la kuiimarisha....Wanamuziki hao ni Shaban Dede,Jerry Nashon 'Dudumizi',Joseph Mulenga,Abdalaah Gama na Athuman Momba....Bendi hii ilikuwa ikitumia mtindo wa Magnet 84 na baadae uliboreshwa ukawa Magnet ndele Tingisha.....
Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Neema,Shangwe ya harusi,Makulata,Linalonisibu,Milionea wa mapenzi,Linalonisibu,Siri yako,Visa vya mesenja,Uzuri ni tabia,Dunia ni upepo,Busu pande tatu,Ndoa fungo la hiyari,Penzi dawa ya chuki,Samaki baharini,Baba Shani,Shakaza na nyingine nyingi....
Bendi hii iliundwa na wanamuziki kama Shaban Dede,Athuman Momba,Joseph Mulenga,Abel Barthazar,Abdallah Gama,Belesa Kakere,Maxmilillian Bushoke,Jerry Nashon,Coumson Mkomwa,Eddy Sheggy,Fresh Jumbe na wengine wengine
Hapa mkuu umenikumbusha mbali hii bendi niliipenda sana,na nimejaribu kutafuta nyimbo zake bila mafanikio. Kama kuna link naweza pata nyimbo zake plz iweke hapa.
shangwe ya harusii imekuwa kitendawili kilichokosa mfumbuuzi jamaaniee,
furaha yoyooo imegeuka maachozi niiliyemtegemea kanisalitii! kaniumbuaae.
www.Muziki.net hapa zipo nyingi lakini za bima lee sijaziona