ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Mkuu Balantanda hizi nyimbo mbili hauna au haujawahi kuzisikia? Nyimbo hizo ni

1. Mama Jeni ... Inaimbwa

Mama Jeni mke wangu kwaheri mamaa, Mungu akulaze mahali pema peponi

2. Nyote wake zangu

Nyote wake zangu mapenzi yangu kwenu ni sawa, mpendane ndio heshima ya ndoa eeh.

Tatizo bandi zilizoimba nyimbo hizi pamoja na waimbaji wake nimewasahau. Kitambo sana hiyo.
Nyote wake zangu waliimba vijana jazz band ,nakumbuka nilikuwa mdogo sana kwenye radio cassette ya spika mbili miaka kama 1993
 
kuna wimbo nautafuta sikumbuki kama waliimba vijana Jazz au bendi gani, kibwagizo chake kilikuwa hivi "enyi wote wake zangu mapenzi yangu kwenu ni sawa mpendane ndio heshima ya ndoa ee"
Vijana jazz
 
MImi naomba huu wimbo uliimbwa na binti mwenye sauti nzuri..." nimeshagunduaa... na yule jiraniii iii,na picha niligundua nilipokuwa nikifuua...
Bwana weee bwana weee.... niambieee ukweliiii...bwanaweee bwana we...nimechoka kudanganywaa
Kiitikio - wacha wacha wacha uongo wako bwana eeh!..
 
Nyote wake zangu waliimba vijana jazz band ,nakumbuka nilikuwa mdogo sana kwenye radio cassette ya spika mbili miaka kama 1993
Asante sana mkuu, ngoja nijaribu kuutafuta kupitia band ya vijana jazz labda nitaupata. Ila tatizo sijui kama hilo ndio jina sahihi la wimbo au walitumia jina lingine kuuita.
 
Diamond 💎 Sound _Etra Time Popori (Official Audio) Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=o2TmN2Ljsm0
Elistone, Jesus, LiverHassan, King Dodoo Le Bouche, Lomalisa, Jojo Jumanne, Joniko Flower, Liva Sultani, Magustino, El Sadat .....

Wana Kimalumalu Kibinda Nkoi, sponsor Muzee Rwegasira, Jack Pemba @ Silent Inn Dar es Salaam, Tanzania
 
Huu uzi ukiwa below 45 yrs hutaambulia kitu, ahsante Balantanda kweli wewe ni makumbusho japo nahisi ulikua mwanamziki ama mmiliki mmojawapo wa bendi enzi hizo
 
ZENA - by TK LUMPOPO in honour of Juma Ramadhan Magola Kilaza


View: https://m.youtube.com/watch?v=OnODG579vVY
TK Lumpopo band na mtindo wao maarufu wazee wanauita ''Subisubi"
Song Zena was first recorded almost fifty years ago (1971). It was recreated at KC Records with support from Maneno Kilaza, Saidi Makelele, Shaban Lendi, Fadhili Msofe, Baba Isaya and Jeydrama.

Source: KC MEDIA

Juma Ramadhan Magola Kilaza, anayefahamika kwa jina la Kilaza ni mmoja wa wanamuziki bora zaidi kuwahi kutokea nchini Tanzania. Kilaza alianza kazi yake ya muziki mapema miaka ya 1960. Enzi za uhai wake alitamba na kuziongoza bendi mbalimbali ambazo ni pamoja na bendi ya Morogoro Jazz, Cuban Marimba, TK Lumpopo, Magola International na Les Cuban zote za Morogoro mjini. Katika bendi hizi zote alizowahi kuzitumikia alicheza nafasi kubwa kama mtunzi na mpangaji wa muziki, hamu yake kuu ilibaki kuwa muziki wa rumba maarufu nchini kama muziki wa dansi. Kuna sababu ya kuzingatiwa hivyo, kwani muziki uliopigwa na takriban bendi nyingine zote za muziki nchini ulikuwa kwa kiasi kikubwa muziki wa rumba wenye asili ya Cuba. Kitabu hiki kinaelezea kazi ya muziki ya Kilaza, kutoka Morogoro jazz hadi Les Cuban. Inaeleza mchango wake katika kukuza lugha ya Kiswahili, kuelimisha, kuburudisha wapenzi wa muziki, na katika kuutangaza mji wa Morogoro alikozaliwa ambao aliupenda na kuupenda sana. Kitabu hiki pia kinaangazia baadhi ya changamoto alizowahi kukumbana nazo katika kazi yake ya muziki na mikwaruzano maarufu aliyowahi kuigiza kati yake na nyota mwingine wa muziki wakati huohuo maarufu mjini Mbaraka Mwinshehe Mwaruka. Source :

THE MAESTRO JUMA KILAZA FROM MOROGORO TANZANIA The town famous in football and music: Dancing to Ambiyansey tunes from mji kasoro bahari​

Anthony Marwa Mwita

 
25 October 2024

MFAHAMU SOLOIST INTERNATIONALE MBARAKA NWINSHEHE WA BENDI YA ORCHESTRA SUPER VOLCANO


View: https://m.youtube.com/watch?v=fbJ2OlOadnY
Simulizi Nzuri Sana na MPYA KABISA ya Maisha ya LEGEND MBARAKA MWINSHEHE. 🔥🔥🔥HADITHI YA MAISHA YAKE YAMESIMULIWA NA MWANAMUZIKI NGULI SAID MAKELELE ALIYEKUWA MPIGA SAXOPHONE WA BENDI YA ORCHESTRA SUPER VOLCANO❗️💢ILIYOKUWA IKIMILIKIWA NA MBARAKA MWINSHEHE.
Source: KC MEDIA
 
Muziki wa dansi original wa Tanzania umerudishwa hewani

January 2025

Song Shida by Super Volcano ft. Muhtaji Mbaraka Mwinshehe Mwaruka


View: https://m.youtube.com/watch?v=Jb_GOxUG3UQ

KC MEDIA presents Muhtaj Mbaraka Mwinshehe who as usual is on the bass guitar and vocals.

The hit SHIDA was recorded at KC Records, enjoy the vibe. Muhtaji Mbaraka Mwinshehe is the daughter of the Tanzanian maestro Mbaraka Mwinshehe, she was only two years old when her father died. The two children Masiku and Muhtaji and their mother had just joined their father in Mombasa when the accident happened.

Muhtaj has also re produced other of his fathers records: Ester, Soniasa and Morogoro yapendeza which are already available on youtube.

All songs were recorded at KC Records by the great producer Jeydrama. It is worth to note that in all the recorded songs the trumpet was played by Saidi Makelele who appears in the video, Makelele was one of the Super Volcano musicians a Tanzanian band , who had featured with the Maestro and after Mbaraka's death joined Les Volcano, Jobiso, Les Wanyika and other bands
Source : Muhtaji Mbaraka Mwinshehe Mwaruka
 
Exclusive na mwanamuziki mkongwe Skassy Kasambula

View: https://m.youtube.com/watch?v=9O8yA0p2t70
1977 Katanga Zaire kwenda Kolwezi mpakani na Angola kuburudisha wanajeshi, 1980 Fan Fan Mosese Sengo na Remmy Ongala, Kasoloo Kyanga, King Kikii, Sambulumaa Band,


View: https://m.youtube.com/watch?v=6KOCYEH63Yo&t=3s
Wanasema eeh Kasongo wanasema urudie, ...Kwenye Unatoka Kuna Waka Moto, Kivumbi Na Jasho, Kwako Wanalia Sana , Mama Urudie Kasongo


View: https://m.youtube.com/watch?v=aygyLxJvT0c
Bolingo na Telephone ...
 
Kuna wimbo niliuona sana 2004-2006 sema nishausahau jina Kuna mdada kavaa kitamaduni kibwebwe anakata nyonga balaa, nishausahau szan kama ntakuja uona tena
 
Harare, Zimbabwe

Muziki wa rhumba dansi wa Tanzania live :

Sulu Chimbetu ft Artist Pitshou Lumiere of Diamond Musica Band singing the Late Hero Simon Chimbetu's song Africa Iyohihihi 2021

View: https://m.youtube.com/watch?v=320Q5xPr_jU
Concert📺 🥁🎸🎤🎼 on NashTV Zimbabwe 🇿🇼👌👆

Harare, Zimbabwe

WIMBO : AFRIKA HII INALIA
Wazazi wa mwanamuziki mkongwe wa Zimbabwe tajwa Simon Chimbetu ni wahamiaji wenyeji wa kutoka Tukuyu mji mdogo wa mkoa wa Mbeya nyanda ya juu kusini ya Tanzania na ndiyo akauimba wimbo huu ukawa maarufu sana nchini Zimbabwe :

Afrika Hii Inaliya

View: https://m.youtube.com/watch?v=sgv-JHxTyN8
 
Mie natafuta nyimbo za TOM MALANGA:
1.AMIGO
2.AFRO
3.BARUA.
Na pia natafuta nyimbo za yule mwanamziki mkongwe(marehemu kwa sasa)ni msambaa wa VUGA Lushoto na kwa jinsi nilivyokua nampenda mwaka 2010 nilisafiri mpaka kijijini kwao nikaliona kaburi lake.
wimbo wake ninao upenda zaidi unaitwa Mwisho wa mwezi.Hapa namuongerea EDDY SHEGGY.
mi pia nililiona lipo kata ya vuga kijiji cha baghai
 
Back
Top Bottom