ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Hii nyimbo ni nzuri sana
IMG_5086.jpeg
 
VULI YENI PAYING TRIBUTE TO KIAMUNGANA MATETA VERCKYS. IN SONG BALUTI VERCKYS STANDS OUT AS ONE OF AFRICA'S GREATEST SAXOPHONE PLAYER Tribute to Kiamungana Mateta Verckys from Kinshasa Congo DR

Source : Vuli Yeni

Baluti - Orchèstre Vèvè

The man himself Kiamuangana Mateta Verckys


23 June 2026
Washington DC

MEKANISI MODERO AFARIKI DUNIA MAREKANI​


6a3a3187c93a10.84041962.png
Juni 23, 2026 - 10:07 AM
Mwanamuziki wa Kongo Mekanisi Modero amefariki dunia.

Kifo chake kilitangazwa na mwenzake wa zamani wa bendi katika Afrisa International, mpiga gitaa Dino Vangu, kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.

Ingawa hakufichua maelezo ya kifo hicho, Mekanisi Modero, mmoja wa wanachama waliohudumu kwa muda mrefu wa Afrisa International, alikuwa akiishi Marekani kwa miongo kadhaa, ambapo alifariki.

"Nimejifunza kutoka Marekani kuhusu kifo cha jana, tarehe 21 Juni 2026, kuhusu mwenzetu, rafiki, na kaka, msanii, mwanamuziki, mpiga saksafoni, na mtangazaji wa kipindi Mekanisi Zemba Gabwisa Modero. Roho yake ipumzike kwa amani."

Ujumbe wa Dino Vangu ulisomwa kwa sehemu.

Mekanisi Modero, aliyejiunga na Afrisa International ya Tabu Ley mwaka 1970, alizaliwa Mekanisi Zemba Bagwisa huko Kikwit, Bandundu, Januari 4, 1944.
Kuvutiwa kwake na Louis Armstrong kulimfanya ajifunze tarumbeta na saksafoni mapema maishani. Tabu Ley alichunguza kipaji chake baada ya habari za zawadi yake kuenea, na akaendelea kuwa mmoja wa wachezaji maarufu wa saksaksi nchini.

Pia aliongoza Afrisa chini ya Tabu Ley, alihudumu kama MC katika matamasha mengi ya bendi, na pia alikuwa mtunzi mzuri wa nyimbo. Saksafoni yake inaweza kusikika katika nyimbo nyingi za Afrisa.

Alikuwa akiishi Washington, DC, tangu 1984, aliposafiri huko na bendi hiyo, na alikuwa akitumbuiza na wanamuziki kadhaa, miongoni mwao Dodo Munoko na Huit Kilo, ambao pia walikuwa wanachama wa bendi hiyo. Muziki wa Kongo umepoteza moja ya nguzo zake kuu, wale waliochangia pakubwa ukuaji wa aina hiyo ya muziki.

View: https://m.youtube.com/watch?v=F817yT85KYc
 
SIMULIZI ZA KINA, MTINDO WA CAVACHA BEATS ULIVYOTUA MIAKA YA 70s NA KUTEKA MIOYO YA WANA AFRIKA MASHARIKI

View: https://m.youtube.com/watch?v=vR_1zskiQMk
Bana Ngenge, Orch. VEVE, BANA MOJA, NEGRO SUCCESS, HI FIVES BAND, ORCH KIAM , SUPER VOX. ORCH SUPER MAZEMBE, ...BABA ILUNGA WA ILUNGA BABA NATIONAL, ORCH LES MANGELEPA, ORCH BWAMBE BWAMBE, ORCH LEKI NOIRE SAM OMAR MAPANGALA, ORCH SAKA SAKA...
Source : Mfumu Kibangu
 
Mtindo wa Zembwela Sendema ya Moto ndani ya Sweden wimbo wa Orch. Marquis Orignal ya Tanzania, utunzi wa Tshimanga Asosa mtoto Kinondoni Dar es Salaam. Pia historia ya wanamuziki wakongwe Dekula na Gaby Kababa wakisimulia Orch. Marquis band ya Dar es Salaam kuanzia kumbi za jijini DSM za Chini ya Mwembe hadi Langata Kinondoni hadi kwa sasa walipo huko Ulaya ya Kaskazini

Stockholms, Sweden
USINICHEKE [Orch. Marquis-Wakati Nilikuwa Mdogo] - DEKULA BAND


View: https://m.youtube.com/watch?v=yJPyV4k2jj0
Dekula Band Soukous Music:Songs: Wakati Nilikuwa Mdogo& AIE Mwana( by Orch Maquis and Black Blood)(live) Parkteatern Husby torg Stockholm Sweden 28/06/2022
Musicians:Guitar/singer:
  • Kahanga Dekula (Vumbi)-Solo Guitar:
  • Göran Larsson -Bass:
  • Joseph Semafumu Drums:
  • Michigan Ngoy rhytmn
  • Sax: Henrik Westerberg
  • Singer: Gaby Kababa
NkombaCameraman: Arwa Mzee Kobe Brayo :Quality images courtesy of Arwa-iCTv

FEBRUARY 2026
Stockholm City
Valentine’s Day Special Concert – Live in Stockholm! ❤️

Go behind the scenes with Dekula Band in this exclusive interview from the 🎤In this exclusive sit-down, Dekula Band members Dekula Kahanga, Gaby Kababa.....

View: https://m.youtube.com/watch?v=ed3Mw36mZZ4
 

HISTORY of DEKULA KAHANGA 'VUMBI'​

1790262794717.png

DEKULA KAHANGA 'VUMBI' AKICHARAZA NYUZI ZA GITA LA SOLO HUKO SWEDEN.


1790262818349.png

DEKULA KAHANGA AKIPIGA GITA KATIKA UKUMBI WA WHITE HOUSE UBUNGO DAR ES SALAAM, TANZANIA.

1790262846331.png

DEKULA KAHANA AKIWA KATIKA PICHA YA 'POZI' NA GITA LAKE.

1790262873539.png

'MAMBO YA ULAYA' VUMBI AKIWA NA FARASI.

1790262908814.png


DEKULA KAHANGA ‘VUMBI’ ALIZIBA PENGO LA NGUZA

Kwa hisani kubwa ya Kiyungi Moshy


January 28, 2013
KATI YA WANAMUZIKI WAAFRIKA waliopata mafanikio makubwa kwa kuchacharika, jina la Dekula Kahanga haliwezi kukosa. Ni mwanamuziki wa dansi, aliyefanikiwa kuanzisha bendi yake katika jiji la Stockholm nchini Sweden baada ya ‘kuitosa’ Maquis Original.


Dekula ambaye ni maarufu kwa jina la ‘Vumbi’, anasisitiza kwamba mafanikio yoyote katika maisha ni lazima mtu kuwa na malengo, na dhamira ya dhati, hatimaye kufanya maamuzi magumu.


Kabla ya kwenda nchini Sweden, ‘Vumbi’ alikuwa mpigaji wa gita la solo katika bendi ya Maquis Original, iliyokuwa ikipiga muziki wake katika ukumbi wa Lang’ata Kindondoni jijini Dar es Salaam, miaka ya 1990.


Akiwa katika mapumziko mafupi nyumbani kwake Mikocheni kwa Warioba jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Dekula alitamka baadhi ya maamuzi magumu aliyoyafanya mojawapo ni lile la kondoka katika bendi hiyo ya Maquis Original, na kutokomea kwenda Sweden bila kujua atakuwa mgeni wa nani huko ughaibuni.


Vumbi anaeleza kwamba hivi sasa hajutii maamuzi yake kwakuwa amepata mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na kumiliki bendi yake iitwayo Dekula Band. Amesema bendi hiyo hupiga muziki kwa mkataba mara mbili kwa mwezi katika ukumbi wa Lala Vin, mjini Stockholm nchini Sweden.


Dekula Band ina wanamuziki mahiri toka nchi mbalimbali duniani, wakiwemo akina Luhembwe Mwanahita ‘Bobo Sukari’ ambaye ni mwimbaji na kucheza Show, Sammy Kasule, huyo ni injinia pia huimba, kupiga gita la besi, drums na kinanda. Wengine amewataja kuwa ni Joe Gerald Nnaddibanga, ambaye huimba, kupiga konga na kucheza show, Christina Frank, na Marceline Kouakoua.

Mwanamuziki Dekula Kahanga, hulicharaza gita la solo na rhythm pamoja na Arne Winald ambaye ni mbonyezaji wa kinanda. Safu hiyo kwa pamoja huufanya muziki wao kukubalika kimataifa hadi kupelekea kupata mialiko lukuki ndani na nje ya Sweden zikiwemo nchi za Ulaya, Asia, Marekani, Japan, Falme za kiarabu na Afrika.


“ Hakuna kitu muhimu kama kuwa na mahusiano mema na baadhi ya watu toka nchi mbalimbali ninazotembelea. Nimefikia kuweza kuongea kwa ufasaha lugha tano tofauti za Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Lingala na Kiswidish” Anajigamba Dekula ‘Vumbi’.
Historia ya Dekula Kahanga anailezea kwamba alizaliwa mwezi Aprili 02, 1962 katika kijiji cha Lumera, Wilaya ya Kivu Kusini huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ni baba wa familia akiwa na mke na watoto watatu. Dekula ni mtoto wa kwanza kati ya watoto kadhaa wa Mzee Aloyce Obeid Dekula, aliyekuwa mfanyakazi katika serikali ya Zaire iliyokuwa ikiongozwa na rais Mobutu SeseSeko.

Alipata elimu ya Sekondari katika shule mbili tofauti za Bukavu na Uvira huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alihitimu kidato cha nne mwaka 1979. Mwaka uliofuatia wa 1980, safari yake katika muziki ilianza kwa kujiunga na bendi za Bavy National, na Grand Mike jazz, ambako alikutana na wanamuziki akina Kyanga Songa na Issa Nundu.


Akiwa huko kwao wilaya ya Kivu, ‘Vumbi’ alikuwa msikilizaji mzuri wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo ilikuwa ikisikika wakati huo na alizitamani sana nyimbo zilizokuwa zikiporomoshwa na bendi za Morogoro Jazz, Jamhuri Jazz, Tabora Jazz, Nyamnyembe Jazz, NUTA Jazz, Mlimani Park, Maquis du Zaire na Orchestra Safari Sound.

Kamwe hatomsahau John Luanda katika historia ya maisha yake, kwa kuwa huyo ndiye aliyekuwa chanzo cha yeye kuingia hapa Tanzania. Luanda alikuwa akimiliki bendi ya Chamwino Jazz, aliwachukua toka Kongo akiwa na wenzake akina Bwami Fanfan, Sisco Lunanga na Baposta kwa madhumuni ya kujiunga katika bendi yake ya Chamwino. Bendi hiyo wakati huo ilikuwa ikipiga muziki maeneo ya Tandale huko Manzese, jijini Dar es Salaam.

“Mwenye bahati habahatishi” ndivyo anavyosema mkung’utaji mahiri wa gita la solo Dekula Kahanga ‘Vumbi’, kwamba mwaka 1980 alikutana na mwanamuziki Chimbwiza Nguza Mbangu ‘Viking’ katika ofisi za ubalozi wa Kongo hapa nchini.

Nguza wakati huo alikuwa mpiga gita la solo pia alikuwa ni mmoja kati ya wanahisa wa Orchestra Maquis Comapy (OMACO) na mmoja kati ya viongozi wa bendi ya Orchestra Maquis du Zaire. Katika maongezi yao, Chimbwiza Nguza alimpa mwaliko yeye na wenzake kwenda kuburudisha kwenye ukumbi wa White House, uliokuwa maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam.


Dekula alikubali mwaliko huo na Weekend moja walifika na kupewa nafasi ya kuburudisha kwa muda mfupi. Walipopanda jukwaani waliweza kuzikonga nyoyo za wapenzi wa muziki waliokuwa wamefurika ukumbini humo pamoja na wanamuziki wa bendi hiyo ya Maquis du Zaire.

Dekula Kahanga baadaye aliitwa na uongozi wa bendi ya Maquis du Zaire akina Chibangu Katai ‘Mzee Paul’, Mutombo Lufungula ‘Audax’ na Mbuya Makonga ‘Adios’ wakimtaka aandike barua ya kuomba kujiunga na bendi yao kwa mkataba usio na mshahara. Alitakiwa na bendi hiyo ili kuziba nafasi ya Nguza ambaye alikuwa tayari ameanza mgomo baridi. Vumbi alikubali na akajiunga na Maquis du Zaire.

Vumbi anaikumbuka siku mmoja wakipiga muziki katika ukumbi wa Temeke Stereo, alimuona Nguza akiwa amejibanza pembeni mwa ukuta ukumbini humo huku akisikiliza midundo inavyounguruma..


“Nilipomuona, nikaingiwa na hofu kubwa nikijihisi kama ninamvunjia heshima Nguza. Nikaomba nimpishe ili ashike nafasi yake” Anasema kwa kujiamini Dekula Kahanga.


Lakini viongozi wake akiwemo Chibangu Katai ‘Mzee Paul’ na Ilunga Lubaba, walimwamuru aendelee kushika ‘mpini’.
Kwa amri hiyo, ilikuwa kama Fisi aliyeachiwa Bucha kuilinda.

Aliweza kuzicharaza kwa umahiri mkubwa nyimbo zote alizokuwa zikipigwa Field Marshal Nguza zikiwemo za Makumbele, Ngalula Seya Malokelee, Karubandika, Mage, Dora mtoto wa Dodoma, Clara, Mwana yoka ya Babote, Nimepigwa ngwala na nyingine nyingi pasipo kutofautisha kati yake na Nguza.

BANZA MCHAFU & VUMBI MAGITAA YAO KTK WIMBO HATARI - NGALULA [CHACHANDA]

View: https://m.youtube.com/watch?v=riNzCtuCfOQ

Aliachiwa kulivurumisha gita hadi mwisho wa onyesho hata mpiga solo Ilunga Lubaba hakutaka kuligusa siku hiyo. Baada ya hapo kwa adabu zote alikwenda kumsalimia na Nguza pale alipo naye hakusita kumpa hogera kwa kazi nzuri.


“Mungu mkubwa, siku hiyo Nyota yangu iling’ara kiasi kwamba hata mimi mwenyewe sikuweza kuamini nilichokuwa nikikifanya jukwaani hapo” Anasema Dekula Kahanga ‘Vumbi’ huku akitabasamu.


Taharuki kati ya uongozi wa Maquis du Zaire na Nguza ‘Vicking’ ziliendelea hatimaye aliondoka rasmi bendi hiyo, hadi kwenda kuanzisha bendi yake ya Orchestra Sambulumaa akiwa na mwanamuziki wengine akiwemo mwanaye Papii Kocha. Bendi hiyo ilikufa baada ya Nguza na mwanaye huyo kuhukumiwa kutumikia kifungo cha maisha gerezani.

Miaka ya 1989 na 1990 Dekula alikuwa kivutio kikubwa kwa wapenzi wa Maquis Original, jina lililozaliwa toka Maquis du Zaire baada ya kuhamia katika ukumbi Lang’ata Kinondoni. Mtunzi na mwimbaji Maquis Original Tshimanga Kalala Assosa, alikuwa akipaza sauti ya kumpandisha mori kwa kumuita mara kwa mara Vumbiii,Vumbiii,Vumbiii kama kibwagizo wakati wa chorus kwenye wimbo wa Ngalula.

Vumbi wakati huo alikuwa na umri ambao unamruhusu kuhangaika kutafuta maisha yenye maslahi mazuri. Hivyo maamuzi magumu yakaanzia hapo Lang’ata baada ya kuamua kuicha bendi ya Maquis Original, iliyompa jina na kuchepukia katika jiji la Stockholm nchini Sweden.

Akiwa Stockholm, Vumbi alianza kuchacharika mitaani akitafuta bendi ya kupiga, hatimaye akakutana na mwanamuzi toka Uganda, aitwaye Sammy Kasule. Mwaka 1993 wakaamua kuanzisha bendi yao ikiitwa Makonde Group.


Mwaka 1999, Dekula Kahanga alifyatua Album iitwayo Bolingo Ekesemi iliyosheheni nyimbo za ‘Dunia kuna mambo’ na ‘mpenzi Asha’
Dekula Kahanga anajivunia kwamba yeye ni mwanamuziki wa kwanza toka Afrika huko Sweden, kufyatua album. Alitoa album iitwayo ‘DEKULA Sultan Qaboos’ yenye nyimbo za Sultan Qaboos, Mon Amour, Babylon, Mayanga, Rozina, Mambo leo na Nostalgie nyimbo hizo anasema zinazopigwa mno katika vituo vingi vya redio Duniani.


Ili kupata unafuu wa maisha nchini Sweden, Dekula alilazimika kuomba uraia wa nchi hiyo hivyo ilifuata taratibu zote. Alichukua maamuzi magumu mengine ya kuukana uraia wa nchi yake ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ili kupata uraia wa nchi hiyo.

Hivi sasa yeye na wanamuziki wenzake wa bendi hiyo ni raia halali wa nchi ya Sweden na wanaweza kusafiri kwenda nchi za Marekani Ulaya Asia na kwingineko pasipo kuomba VISA.


Dekula ametoa mwito kwa wanamuziki chipukizi kujifunza kupiga ala za muziki ili wafikie viwango vya kuwa wanamuziki. Pia amewaasa kuacha kulewa sifa ndondogo pia kuepuka anasa zisizo na tija.


“Nawapenda sana Watanzania, walinipokea, wakanilea, wakanithamini na wakanipenda. Ninatarajia kutoa zawadi endelevu kwa Watanzania siku za usoni kuanzisha bendi ya vijana, itakayokuwa ikitumia ala za muziki wa kisasa” anamaliza Dekula Kahanga Vumbi
Source : kwa hisani kubwa ya blogger HISTORY of DEKULA KAHANGA 'VUMBI'
 
Dekula Band - Zinduna


View: https://m.youtube.com/watch?v=786G8ScYWAQ
  • Gaby Kababa Nkomba,
  • Kahanga Dekula Vumbi,
  • Henry Matano,
  • Michigan Ngoy,
  • Henrik Westerberg, Eddy,
  • Jonas Fogelström
Mtindo wa Muziki wa dansi wa Tanzania bila jasho ukipamba moto nchi za Scandinavia


05 October 2026
Stockhölm, Sweden

Habari za kusikitisha, mzee wetu Gaby Kababa Nkomba ameaga dunia nchini Sweden ambapo amekuwa akiishi kwa zaidi ya miaka 40.

1791374446113.png

Gaby Nkomba Kababa, a former member of Orchestre Safari Sounds dunia msongamano, has passed away

The veteran musician, Kababa Nkomba Gabby, has passed away in Stockholm City where he has been living for the last 40 years

Until his death, the highly gifted, Kababa Nkomba was playing with Dekula Band

Our thoughts and prayers are with the family mzee Gaby Nkomba Kababa , the Dekula band members, friends and fans of muziki wa dansi around the world.
 
Back
Top Bottom