ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

September 2025
Exclusive interview in English :


Moto Pamba ilivyombeba Awilo Longomba kutoka kuwa drummer hadi mwimbaji pia

View: https://m.youtube.com/watch?v=wcuWuDlKRCc

Nilikuwa nipo wazi napiga mitindo yote Rhumba, Zouk, Sokous, Soul Makossa, Ndombolo, Sebene n.k nimefanya kazi na wakali mbali mbali kama Oliver Ngoma, Papa Wemba n.k


TOKA MAKTABA :


View: https://m.youtube.com/watch?v=1utfA59aabE
Longomba baba yake ni Vicky Longomba mwanamuziki nguli wa TP OK Jazz ya Franco wa DR Congo anayeonekana ktk kazi nyingi za Franco ndani ya YouTube ....


View: https://m.youtube.com/watch?v=ctJvtfj-2Jg
 
"Wapendeza" - by Makonde Band



Source : Sammy Kasule

25 June 2025

LIVE : Wapendeza / Makonde Band at Hijazz Club Uppsala

View: https://m.youtube.com/watch?v=luDMizYbc_M

Makonde Band at Hijazz Club Uppsala Sweden Homage to Sammy Kasule and Gerald

  • Nnaddibanga.Bass/
  • vocal:Sammy Kasule
  • Vocal:Christina Frank
  • Vocal: Gerald Nnaddibanga
  • Guitar:Kahanga Dekula Vumbi
  • Keyboards: Arne Winald
  • Congas: Sebastian Prinz-Werner
  • Drums:Mike Trumpet:.....
Makonde Band Live concert at Hijazz Club in Uppsala Sweden 2009
Source : Dekula Band (official )
 
Orchestra Safari Sound - Isihaka

View: https://m.youtube.com/watch?v=Tl9JOS9QgLM
Mtindo wao wa muziki wa rumba wa Ndekule, huku line up ya kushiba ya wanamuziki
Muhidin Ngurumo, Skassy Kasambula, Bitchuka ... IOSS International Orchestra Safari Sound iliyomilikiwa na mwekezaji Hugo Kisima tajiri asiyetaka kushindwa walilifanya jiji la Dar es Salaam kuchemka kwa burudani ...
 
Slavery is Crime - Maestro Vumbi & Dekula band

View: https://m.youtube.com/watch?v=FCPWO0-nhrU
Mtindo wao wa dansi wa Sendema ya moto version 2.0

  • Main artist : Vumbi Dekula
  • Main artist : Dekula Band
  • Producer : Kahanga Vumbi Dekula
  • Composer: Kahanga Dekula
  • Vocal : Gaby Kababa Nkomba
  • Music Publisher : Manus
 
Nanreen......Eddy(mtoto wa Tambaza almaarufu kama msomi wa Tambaza huyu) kwa kweli alikuwa anavutia hasa,alikuwa ana sauti ya kipekee kabisa,sikiliza nyimbo alizoimba kama Wivu,Mwisho wa mwezi,Ngapulila(Vijana Jazz), Julie,Nelson Mandela,Yaliyopita si ndwele(Washirika Tanzania Stars), Shakaza(Bima Lee Orch), Milima ya kwetu(Super Rainbow), Ngondoigwe,Baba Jane(Bantu Group) utagundua ni kwa nini nasema Eddy Sheggy 'Mzee Shakaza'(R.I.P) alikuwa na sauti ya kipekee........Japo wadogo zake Francis na Christian Sheggy walijaribu kumuiga,hawakuweza.....Jamaa alikuwa sayari nyingine kabisa.......

Hebu angalia kitu hiki ulichokiomba ambacho Eddy alikitunga na kukiimba akiwa na Super Rainbow,aliimba kwa kushirikiana na Nanah Njige.....Kitu Milima ya kwetu...

Milima ya Kwetu

Nikitazama milima ya kwetu ee,
machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo,
tulitoka wawili ninarudi peke yangu,
baba na mama wataniuliza bibi yako yuko wapi ee,
Ndugu jamaa wataniuliza bibi yako yuko wapi eee,

japokuwa ninakaribia kufika nyumbani ee,
Ninatamani gari isifikie upeesi,
kwa ile aibu nitakayopata mbele ya wazazi ii,
kwa vile ni miezi michache imepita nilitoka na bibi yangu,

(Eddy)
Nitasema nini kwa baba mimi najuta aa,
kwa pesa zake nyiingi alizopotezaa,
harusi ilifanyika kwa gharama kubwa sana,
watu walikula na kunywa na kusaza mamaa,

Nikaenda kuishi na bibi yule mjini,
kazi yake ilikuwa ni vituko,
nikaenda kuishi na bibi yule mjini kazi yake ilikuwa ni vitiimbwi,

Alianza kuweka sukari kwenye mboga,
nikaonja haviliki tukalala na njaa,

kafuatia na kuweka chumvi kwenye chai,
nilikuwa na wageni wakatoka bila kuaga,

kafuatia kuchelewa akienda sokoni,
nikimuuliza anitukana hadharani aibu,

kuna gari imekuja hadi mlangoni,
kujitetea akasema mjomba wake kaja,

hivi juzi kavunja kioo cha dirisha,
apate kuchungulia wapitao njiani,

hatimaye kunibeza na kunidharau,
shikamoo ikaisha ikabaki
Vipi babu, mambo zakoo ee x2

Nilishindwa kumuuliza ee sikutaka kumuudhi,
sababu nilikuwa nampenda nampenda saana x 2

chorus:

walisemaa dalili ya mvua ni mawingu,
niliyempenda kanitoroka mama,

(Eddy Sheggy)
Nilinyang'anywa tonge mdomoni,
nilinyang'anywa tonge kinywani,
niliyempenda kanikimbia mama yoyo,
niliempenda kanikimbia masikini nifanye nini mama,

(chorus)

Vituko ee, vituko vya bibi huyoo,
sitaweza kusahau mimi oo mama ee,
sitaweza kusahau mimi oo sheggy ee,
alikuwa kama helikopta, ndege isiyochagua mahali pa kutua ee,
kila mtaa hapa mjini jamani tazameni oo,
ana bwana mmoja ama wawili mama mama oo,
nifanye nini mama oo,
Eddie Sheggy hakuwahi kuhamia Bantu Group hizo nyimbo ziliimbwa na Muumini Mwinyijuma, Ally Choki na Musemba wa Minyungu
 
Eddie Sheggy hakuwahi kuhamia Bantu Group hizo nyimbo ziliimbwa na Muumini Mwinyijuma, Ally Choki na Musemba wa Minyungu
Duh...We jamaa...Una umri gani wewe?...Nani kakudanganya?....Eddy alipotoka Washirika Tanzania Stars yeye na wadogo zake Christian na Francis waliungana na Komandoo Hamza Kalala kuanzisha Bantu Group...Hao akina Mwinjuma na Choki walikuwa waitikiaji (back vocals) tu...Sikiliza wimbo wa Ngondoigwa hapa chini ndio utajua kama Eddy Sheggy ameimba Bantu group ama la....Pia kasikilize Vicky, Mkanda wa Mapenzi na Yaliyopita si Ndwele....


View: https://youtu.be/MeB37s46pe0?si=_Udm_XlJ83a1vi10
 
Eddie Sheggy hakuwahi kuhamia Bantu Group hizo nyimbo ziliimbwa na Muumini Mwinyijuma, Ally Choki na Musemba wa Minyungu
IMG_3682.jpeg

Hawa ni Bantu Group Band wakiwa jukwaani....Huyo wa Tatu kutoka kushoto ni Eddy Sheggy (Mzee Shakaza) akiwa anashambulia Jukwaa na 'Wana Bantu Boma Tunakula Miziki'......
 
Tancut Almasi Orchestra na mtindo wao wa Mangala Dance. Makazi yao yalikuwa Iringa nchini Tanzania.

"Samahani ya Uongo" - Tancut Almasi


View: https://m.youtube.com/watch?v=amEvstUOrqY

Kawele Mutimuana - "Wanasema Uridie Kasongo" (Orch. Maquiz du Zaire song) Live in England


Source : kawele mutimuana
..............................................................................
Iringa, Tanzania

Tancut Almasi Band
Kawalee Mutimuana mpiga gitaa mahiri akiwa na Tancut Almasi Band ya mjini Iringa Tanzania bendi iliyokuwa imesheheni wanamuziki kamili kina Skassy Kasambula, John Kitime, Mapacha Kyanga Songa ..



Source : Sulutani Kasambula
 
Usitumie Pesa Kama Fimbo - DDC Mlimani Park


View: https://m.youtube.com/watch?v=Fs4uzWHVzKs
The band was the resident orchestra of the Tanzania Transport & Taxi Services (TTTS) owned Mlimani Park Bar in Dar es Salaam, Tanzania
Mlimani Park ilianzishwa mwaka 1978,ikiwa na wanamuziki kama Abel Balthazar (solo na second solo), Muhiddin Maalim Gurumo(muimbaji), Cosmas Thobias Chidumule (muimbaji), Joseph Mulenga(Bass), Abdallah Gama (rhythm), Michael Enoch (Saxophone), Hamisi Juma(mwimbaji), George Kessy(kinanda), Haruna Lwali(Tumba), ikiwa chini ya TTTS (Tanzania Transport and Taxi Services).

Mwaka 1983 shirika hilo lilipopiga mueleka kifedha kama mashirika mengi wakati huo bendi ikawekwa chini ya himaya ya Dar es Salaam Development Corporation (DDC).
Source : The band was the resident orchestra of the Tanzania Transport & Taxi Services (TTTS) owned Mlimani Park Bar in Dar es Salaam, Tanzania

Info credit to John Kitime
 
Back
Top Bottom