ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao


Nginde
Dunia nzima
 
Namba moja
Namba moja

dah nilikuwa na miaka 9 wakati huo
 
kuna ubishi wa kumbukumbu...
je kwenye wimbo Asha Bora wa sikinde solo limepigwa na nani?
1) Kasim mponda delashamshi
2) Mkanyia
Sina uhakika sana..Ila bendi zetu hizi zilikuwa na wapiga solo wawili...First solo na second solo...

Ila mpini wenyewe wa solo aliukamata Kassim Mponda 'De la Chance' (sio Delashamshi)...

Na inawezekana second solo alipiga Henry Mkanyia...

All in all Kassim Mponda ni mmojawapo wa wapiga solo bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania...

Ukitaka uone ubora wake pia sikiliza wimbo wa 'Kiu ya Jibu' wa Nginde...
 
Reactions: bdo
Waungwana kuna mtu anaukumbuka wimbo uliopigwa na Six Manyara unaitwa Tabu, ambapo mmoja ya waimbaji wake
alikuwa Hassan Rehani Bichuka.
Wimbo uliimbwa na Juma Ubao akiwa na Six Manyara Band

Enjoy mkuu....

 

Mulenga numero uno
 
Tatizo wewe Gang una mahaba ya sikinde asilimia 100.

Nipe kisa cha Nico Zengekaya...


heh heh heh kuna swahiba wangu anadai kuwa hakuna wimbo wa nginde ulio bora zaidi ya Solemba ambao Zengekala kaunguruma saana humo.

dah aysee amenisikitisha na kunisononesha wallah
 
Salama wana JF, mwenye video za nyimbo ya albamu ya RABANA ya ottu jazz band naomba anisaidie, albamu ile si mchezo, waliimba malegendary tx moshi, gurumo,maina, bitchuka na othman momba
 
salama wana JF,Mwenye audio ya nyimbo ya sekuntoza kigudi chauma ya ottu jazz band anisaidie, naitafuta sana
 
Kuna Bendi ilikuwa inaitwa Diamond Sound mwaka 1997 ilitoa albam yenye wimbo "kibinda nkoi" Sina hakika kama nimepatia, naweza kupata audio yake?
 
wadau kama kuna mtu anaufaham huu wimbo au anao.
Nidhamu ya kazi ni msingi wa mafanikio bora kazini, viongozi na wafanyakazi lazima wote muwe na nidhamu, migogoro na migongano makazini ni ukosefu wa nidhamu
 
na pia kama kuna mtu anaufaham wimbo una maneno
cheka lakini kaburi lakungoja, unahusu ukimwi ni wa zamani......
 
wadau kama kuna mtu anaufaham huu wimbo au anao.
Nidhamu ya kazi ni msingi wa mafanikio bora kazini, viongozi na wafanyakazi lazima wote muwe na nidhamu, migogoro na migongano makazini ni ukosefu wa nidhamu
Dah! We jamaa umenikumbusha mbali sana.Nizamu ya kazi ni ushindi na mafanikio mema kazi,viongozi na wafanyakazi daima wote tuwe na nidhamu...migogoro na migongano ya kazini ni ukosefu wa nidhamu!! Aisee hapo ikiwa inapigwa hyo ngoma,mama anaunga kisamvu na ugari unanukia,hapo mshua amekalia kiti kama cha baba madenge anasoma gazeti la mzarendo...aisee mwenye nao atusaidie
 
Mamaaa eeeh eyaeeh Madona eenh!

Mamaaa eeeh eyaeeh Madona eenh!

Mtoto wa kwetu eenh Madona eenh!

Unipe habari eenh Madona eeenh!

Nipate kujua eenh Madona eenh!

Mwenyewe ulienda eenh Madona eenh!

Mtoto wa kwetu eenh Madona eenh!

Iyolelah Iyolelah Iyolelah.......!!!

Eeenh venye niliendaaaa!!

Oooh nakuya Na miyumbiiii..!!

Oooh miyumbi Ndio ya kwakoooo!!

Oooh ya babaee na Mamaa !!

Wanasema Mrudieeeh Mrudieeh..!!

WANASEMA Mrudie,

Mrudie Kasongo!

Wanasema Mrudie we baba!

Kwenye natoka kunawaka moto!

Kwenye natoka Kivumbi Na Jasho ooh!

Kweni kumujini ikaa eenh magangaa!

Oooooooh Kasongo! Hawa Jamaa walikua Na Mziki mzuri sana! Huwezi amini ukitazama hiyo video ya Kasongo! Wenyewe Wanasema ilikua Ni Miaka ya 1974/1975.. King Kikii Na wenzie wanafanya mambo! Hata Kiswahili walikua bado hawajakijua vizuri.
 
Reactions: bdo
Ha ha ha ha ha ha ha haaa! Kinaitwa kiti cha uvivu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…