ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Mimi bana sikinde tuuu, jamani sikinde watani wangu msondo mtaniwia radhi. Dah kuna vibao nikivisikia mpaka natokwa na jasho kuna kitu km Duniani Kuna mambo, wikiendi nalala kwa taabu, kwa ujumla sikinde you rock my heart!! ningekuwa na pesa ninge invest trillions pale basi tu sina kitu. haya kuna hawa marques du zaire enzi za kamanyola bila jasho kuna kibao kama dola mtoto wa Dodoma( yakaa yaka eeehn mwana mama ndimandimaeee mwana mama ...... mtoto wa dodoma) kuna kinanda flani kinapigwa mle na gitaa yaani ni raha tupu!! inanikumbusha sana dada yangu marehemu Mage jamani wakati niko Sumbawanga alikuja toka Dar basi anaziimba hizi nyimbo za makwizzz aaah jamani KAMANYOLA BILA JASHO! ikaja telemuka telemuka chekechaaaaaa

Nginde
Dunia nzima
 
Namba moja
Namba moja
Kwa waliokuwepo Mwanza 1969 tukumbuke Orchestra Super Vea. Hapo alikuwepo pia mpiga rhythm mahiri Zahir Ally (Baba yake Banana) wakati huo tunamwita Zahoro "Zorro" na alikuwa kijana mtanashati sana. Tulikuwa tukipita Social Hall, karibu na Nyakabungo njiani kuelekea Isamilo toka Chopra Sec ilikuwa ni lazima tutulie kidogo pale na kuwasikiliza Super Vea mazoezini, walitamba sana na kibao chao cha Apollo kumi na moja. Vijana waliotamba enzi hizo Mwanza walikuwemo pia Martin (mchezaji wa Pamba Sports na mfanyabiashara wa madini). Zahoro alikuwa na uwezo wa kupiga gitaa wakati amelibeba nyuma ya kichwa, staili maarufu sana wakati huo. Baadaye nilikuja kukutana na Zahoro 1974 Dar es Salaam akiwa anafanyiwa audition na Bima Lee (bendi ya Bima wakati huo) kwenye jengo jipya la Kitega Uchumi pale chini (underground floor) kulikuwa na sehemu ya mazoezi kabla haijageuzwa kuwa Chinese Restaurant. Zahir hakufanikiwa kujiunga na Bima Lee lakini baadaye aliibukia JKT Kimbunga.

dah nilikuwa na miaka 9 wakati huo
 
kuna ubishi wa kumbukumbu...
je kwenye wimbo Asha Bora wa sikinde solo limepigwa na nani?
1) Kasim mponda delashamshi
2) Mkanyia

Sina uhakika sana..Ila bendi zetu hizi zilikuwa na wapiga solo wawili...First solo na second solo...

Ila mpini wenyewe wa solo aliukamata Kassim Mponda 'De la Chance' (sio Delashamshi)...

Na inawezekana second solo alipiga Henry Mkanyia...

All in all Kassim Mponda ni mmojawapo wa wapiga solo bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania...

Ukitaka uone ubora wake pia sikiliza wimbo wa 'Kiu ya Jibu' wa Nginde...
 
  • Thanks
Reactions: bdo

Mulenga numero uno
 
Tatizo wewe Gang una mahaba ya sikinde asilimia 100.

Nipe kisa cha Nico Zengekaya...

heh heh heh kuna swahiba wangu anadai kuwa hakuna wimbo wa nginde ulio bora zaidi ya Solemba ambao Zengekala kaunguruma saana humo.

dah aysee amenisikitisha na kunisononesha wallah
 
Salama wana JF, mwenye video za nyimbo ya albamu ya RABANA ya ottu jazz band naomba anisaidie, albamu ile si mchezo, waliimba malegendary tx moshi, gurumo,maina, bitchuka na othman momba
 
salama wana JF,Mwenye audio ya nyimbo ya sekuntoza kigudi chauma ya ottu jazz band anisaidie, naitafuta sana
 
Kuna Bendi ilikuwa inaitwa Diamond Sound mwaka 1997 ilitoa albam yenye wimbo "kibinda nkoi" Sina hakika kama nimepatia, naweza kupata audio yake?
 
wadau kama kuna mtu anaufaham huu wimbo au anao.
Nidhamu ya kazi ni msingi wa mafanikio bora kazini, viongozi na wafanyakazi lazima wote muwe na nidhamu, migogoro na migongano makazini ni ukosefu wa nidhamu
 
Dah! We jamaa umenikumbusha mbali sana.Nizamu ya kazi ni ushindi na mafanikio mema kazi,viongozi na wafanyakazi daima wote tuwe na nidhamu...migogoro na migongano ya kazini ni ukosefu wa nidhamu!! Aisee hapo ikiwa inapigwa hyo ngoma,mama anaunga kisamvu na ugari unanukia,hapo mshua amekalia kiti kama cha baba madenge anasoma gazeti la mzarendo...aisee mwenye nao atusaidie
 
Mamaaa eeeh eyaeeh Madona eenh!

Mamaaa eeeh eyaeeh Madona eenh!

Mtoto wa kwetu eenh Madona eenh!

Unipe habari eenh Madona eeenh!

Nipate kujua eenh Madona eenh!

Mwenyewe ulienda eenh Madona eenh!

Mtoto wa kwetu eenh Madona eenh!

Iyolelah Iyolelah Iyolelah.......!!!

Eeenh venye niliendaaaa!!

Oooh nakuya Na miyumbiiii..!!

Oooh miyumbi Ndio ya kwakoooo!!

Oooh ya babaee na Mamaa !!

Wanasema Mrudieeeh Mrudieeh..!!

WANASEMA Mrudie,

Mrudie Kasongo!

Wanasema Mrudie we baba!

Kwenye natoka kunawaka moto!

Kwenye natoka Kivumbi Na Jasho ooh!

Kweni kumujini ikaa eenh magangaa!

Oooooooh Kasongo! Hawa Jamaa walikua Na Mziki mzuri sana! Huwezi amini ukitazama hiyo video ya Kasongo! Wenyewe Wanasema ilikua Ni Miaka ya 1974/1975.. King Kikii Na wenzie wanafanya mambo! Hata Kiswahili walikua bado hawajakijua vizuri.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Dah! We jamaa umenikumbusha mbali sana.Nizamu ya kazi ni ushindi na mafanikio mema kazi,viongozi na wafanyakazi daima wote tuwe na nidhamu...migogoro na migongano ya kazini ni ukosefu wa nidhamu!! Aisee hapo ikiwa inapigwa hyo ngoma,mama anaunga kisamvu na ugari unanukia,hapo mshua amekalia kiti kama cha baba madenge anasoma gazeti la mzarendo...aisee mwenye nao atusaidie
Ha ha ha ha ha ha ha haaa! Kinaitwa kiti cha uvivu!
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom