Zile kelele za Rais Magufuli aongezewe muda mbona hazipingwi kwa Rais Samia?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Baada ya uchaguzi mkuu ambao ni moja ya chaguzi mbaya kupata kutokea Tanzania, bunge la Tanzania kupitia wabunge wake wa chama kimoja waliopatikana baada ya uchaguzi kuchafuliwa na tume ya uchaguzi kulizuka mjadala bungeni wa kuwa rais Magufuli aongezewe muhula wa uongozi.

Mbunge wa Makambako bw. Deo sanga alilishikia bango suala hili na spika kumpa muda mwingi wa kulizungumzia. Mwaka 2020 wakati bunge linamaliza muda wake mbunge wa nkasi bw ally kessy alitaka rais magufuli aongezewe muhula wa uongozi na spika ndugai kwa kiburi alitalia kuwa hoja hiyo ailete bunge lijalo na kudai kuwa tena tutakuwa wenyewe(CCM) bila upinzani kwa maana walikuwa wamepanga namna uchaguzi mkuu utakavyokuwa kuwakata wapinzani. Spika Ndugai alisema Magufuli atake au asitake lazima aongezewe muda.

Mpango wao umefeli Magufuli kafariki najiuliza mbona zile kelele hazipigwi kwa Rais Samia kuwa aongezewe muda?

Mbona Deo Sanga kapoa?

Mbona spika nae kawa baridi?
 
Huyu kwenye lile genge atakuwa alikuwa outsider.

Ukizingatia engine yote kishaisasambua sambu wengine wako mahali salama, wengine wanapumulia mashine na wengine wanakaribia Njombe!
 
Baada ya uchaguzi mkuu ambao ni moja ya chaguzi mbaya kupata kutokea Tanzania, bunge la Tanzania kupitia wabunge wake wa chama kimoja waliopatikana baada ya uchaguzi kuchafuliwa na tume ya uchaguzi kulizuka mjadala bungeni wa kuwa rais magufuli aongezewe muhula wa uongozi...
Mkuu lile ni kusanyiko la Wapumbavu ndio walikua na ile hoja.

Bado wana matarajio Meko aatarudi waanze upya.
 
Baada ya uchaguzi mkuu ambao ni moja ya chaguzi mbaya kupata kutokea Tanzania, bunge la Tanzania kupitia wabunge wake wa chama kimoja waliopatikana baada ya uchaguzi kuchafuliwa na tume ya uchaguzi kulizuka mjadala bungeni wa kuwa rais magufuli aongezewe muhula wa uongozi...
Ile ilikuwa project maalum yav kayafa na ndio alikua mfadhili mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom