Kuna kipindi Mabibo hostel iliongoza kwa tuhuma za vitendo vya ngono baina ya wanachuo kwa wanachuo na wanachuo na watu wa nje. Baada ya kuishi Mabibo Hostel kwa miaka miine mfululizo, nikagundua tuhuma hizo sio za kweli, ila Mabibo ilionekana sana kwa sababu ya geti moja tuu la kuingilia na halls zote ziko mahali pamoja hivyo kupelekea kuonekana sana kwa pilika za malove dove wakati Main Campus ndio imekua ikiongoza ila kwa vile halls ziko mbalimbali na mageti kibao, pilika hizi hazikuonekana kwa karibu.