Zijue tabia sugu za wanachuo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zijue tabia sugu za wanachuo

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Toboamambo, Jan 12, 2009.

 1. T

  Toboamambo Member

  #1
  Jan 12, 2009
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Hupenda kwenda baa na kumbi za starehe kuliko Lecture na Semina.
  2. Hushinda room kuliko Library.
  3. Hufahamu mitindi ya mavazi kuliko Module.
  4. Huogopa CARRY,SUP na DISCO kuliko dhambi.
  5. Hufahamu waziri wa mikopo kuliko wahadhiri.
  6. Huudhulia birthdays,harusi na starehe weekend kuliko Ibada.
  7. Hutoa zawadi kubwa kwa boyfriend au girlfriend kuliko kwa yatima na wajane.
  8. Hulinda ATM Cards na PENZI kuliko DESA na VITABU.
  9. Wapo makini na ratiba ya BOOM kuliko UE.
  10. Wanapenda haki ila wengi ni waoga wa kuzidai.
   
 2. m

  millanzigabriel New Member

  #2
  Jan 12, 2009
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli ila ungekuwa na njia ya ku2saidia ingekuwa bomba ena mkazuzu,ila poa saaana kwa ku2amsha,usikonde we are 2gether
  erhard
   
 3. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,032
  Likes Received: 564
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli uliopitiliza( it is more than the truth itself). Na ndio viongozi wetu wa kesho
   
 4. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #4
  Jan 13, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sijui kama alimaanisha TABIA ZA WANAFUNZI WA SASA? au kwakuwa ametaja waziri wa mikopo, otherwise you are in, unless hukuwahi kuwa mwanachuo.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,616
  Trophy Points: 280
  Huo ni ukweli mtupu ambao umesababishwa na mazingira ya utoaji elimu ya chuo kikuu inayoendana na mikopo. Na katika kuogopa supp na disco, baadhi ya wanafunzi wa kike ambao ni dhaifu katika kudesa, huwa wanakuwa tayari kufanya lolote ili kuepuka supp, hiyo inapelekea kujitoa kutumika hata miili yao.

  Kuna kipindi Mabibo hostel iliongoza kwa tuhuma za vitendo vya ngono baina ya wanachuo kwa wanachuo na wanachuo na watu wa nje. Baada ya kuishi Mabibo Hostel kwa miaka miine mfululizo, nikagundua tuhuma hizo sio za kweli, ila Mabibo ilionekana sana kwa sababu ya geti moja tuu la kuingilia na halls zote ziko mahali pamoja hivyo kupelekea kuonekana sana kwa pilika za malove dove wakati Main Campus ndio imekua ikiongoza ila kwa vile halls ziko mbalimbali na mageti kibao, pilika hizi hazikuonekana kwa karibu.
   
 6. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Pasco
  Uko sawa ila usiwanyonge sana wakuu wa Mlimani, hizi ni tabia za wanachuo kwa ujumla wao, nadhani baadhi yake ni za kiulimwengu hasa mtu akiitwa mwanafunzi. Utata unakuja zaidi katika mhimili mkuu wa uchumi na uwezo binafsi na wa nchi kwa ujumla...ila uanafunzi raha jamani
   
Loading...