Zijue sababu za wapinga mahari na watetea mahari

Zijue sababu za wapinga mahari na watetea mahari

evonik

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Posts
3,996
Reaction score
5,194
Heshima kwenu wakuu, natumai mko powa, Leo hii tatizo kubwa na sugu la vijana linalowakwamisha kupata wake au chumba nyingi kuharibika ni tatizo la mahari kwa baadhi ya makabila hapa Tanzania. Katika utamaduni wa kiafrika hasa Afrka ya mashariki , mwanaume ndiye hutoa mahari, na mahari hii hupewa wazazi wa binti.


Nitoe mfano kwa Kabila la wasukuma sehemu ya mkoa wa Shinyanga, katika jamii ya wafugaji kijana anapotaka kuoa huko, analazimika kulipa ng'ombe wengi kama mahari, na si rahis kijana kulipa na hii inepelekea vijana wengi kuwatorosha mabinti .
Huo ni mmoja tu wa mfano lkn makabila mengi hutoza mahari kubwa sana.

Wapinga mahari ni watu wenye msimamo sana dhidi ya mahari, hawataki mahari zitolewe kwa vijana wanaotaka kuoa, zifuatazo ni sababu zilizotolewa na wapinga mahari.

1) Wanasema Mahari zimewafanya wanawake wahesabiwe kama bidhaa katika jamii hiyo, kwa hiyo hadhi yao ya ubinadam imeshuka kwa sabubu huonekana kama Mali.

2) Mahari imekuwa kitega uchumi kwa wazazi na hivyo kushawishi vijana kutumia njia mbadala kuipata na hata wakati mwingine kulazimika kuingia katika madeni yasiyo ya hiari ili tu wapate mahari


3) Mahari pia imechangia wasichana kuolewa na watu wasiowapenda kisa tu wazazi wana taka mahari kutoka kwa mwanaume ambaye anatoa mahari nyingi ikiwepo Mali.


4) Mahari imesababisha kujenga hofu kwa wazazi wa binti kwa kurudisha mahari endapo binti yao atapewa talaka, kwa hali hiyo hawawez kumshauri binti kupinga kunyanyaswa badala yake humlazimisha avumilie manyanyaso kutoka kwa mumewe,

5) Wanaendlea kusema mahari imesababisha vijana kuzalisha wanawake na kuwaacha kisa tu wamekosa mahari ya kulipa na kuishi nao pamoja kama make namme.

6) Mahari inaua upendo wa dhati kwani mwanaume huona mwanamke kama kitu alichokinunua hivyo ni Mali yake na ana uwezo wa kutumia atakavyo.

Pia upande wa watetezi wa mahari ambao wanaona ni lazima kijana atoe mahari, nao walikuja kwa kutetea jadi ya kiafrika isivurugwe na ustaarabu wa kimagharibi na hoja zao za kutetea utoaji wa mahari ni kama zifuatazo;

1) Mahari humpima kijana wa kiume kwamba amekomaa vya kutosha kuchukua jukumu la ukuu wa familia.kwa maana atategemewa na mkewe pamoja na watoto wake kwa mahitaji mbalimbali kama vile chakula, malazi na mavazi

2) Mahari humfanya mwanamke ajione wa thamani na kwamba mume wake ana mthamini si wa bure bure. Hivyo hujenga mawazo kwa mwanamke kuwa anaheshimika.

3) Wanaendelea kesema Kulipa mahari njia ya kurudisha angalau gharama waliyotumia wazazi wa binti kumlea, kumtunza na hata kumuelimisha (ingawaje mahari hailipi gharama yote lakini inapunguz)

4) Mahari ni njia ya kuhalalisha ndoa katika mazingira ya kiafrika, kuonekana na jamii kuwa umenuia kuoa kweli, wakati mwingine hakuna harusi(sherehe) lakini kitendo cha utoaji wa mahari panakuwepo mashahidi/ washenga ambao hushuhudia utoaji wa mahari.

5) Mahari huimarisha uhusiano baina ya pande mbili za mwanaume na mwanamke kuliko angemchukua bila kutoa mahari kwa sababu kwenye mahari ndio huenda kutoa vitu kama kanga ya bibi, shuka lababu, Jembe la mjomba n.k hivyo kuendeleza mahusiano.

6) Mahari ni utamduni wetu wa kiafrika, hivyo katika utoaji wa mahari tunaenzi utamaduni wetu ukiokuwepo tangu na tangu hata kabla ya kuja kwa mkoloni.

TATHIMI YA MAHARI

Katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 16 cha Sheria ya ndoa kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 katika "Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kufunga Ndoa" hakioneshi kipengele cha utoaji wa mahari kwa mwanaume.

KWA WAKRISTO. Mahari ilichukuliwa kama adhabu kwenye agano la kale,
"Mtu akimshawishi mwanamwali aliyeposwa na mume, na kulala nae, Lazima atatoa mahari kwa ajili yake ili awe mkewe" (Kut 22:16) kwa hiyo mwanamke anaweza kuposwa pasipo kulipiwa mahari, na (Mat 1:18)
...Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu kabla hawajakaribiana ..."

KWA WAISLAM. Mahari inatakiwa apewe binti moja kwa moja na sio kwa wazazi kama ilivyo kwa tamaduni zingine,
Qur’ani inasema kwa ufasaha:
ﻭَﺁﺗُﻮﺍ ﺍﻟﻨِّﺴَﺎﺀَ ﺻَﺪُﻗَﺎﺗِﻬِﻦَّ ﻧِﺤْﻠَﺔً ۚ
“Wapeni wanawake mahari yao, hali yakuwa ni hadiya (zawadi)…” (Suratul Nisa 4:4) .
 
Kwani mimi sikusomeshwa au kutunzwa na wazazi wangu? hizo gharama vipi? Sema mahari imekuwa biashara tu.
 
Kutokana na kutokudumu kwa ndoa nyingi siku hizi haina haja ya kutoa mahari labda mpaka ndoa ifikishe miaka hamsini itapendeza zaidi
 
Back
Top Bottom