Zijue Nchi zinazochangia fedha EU!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Hela ambayo nchi inachangia EU inaendana na ukubwa wa Uchumi wa nchi husika, hivyo nchi zenye Uchumi mkubwa zinachangia fedha nyingi zaidi!
Nchi ambazo hazimo kwenye hiyo orodha ni nchi ambazo hupokea fedha ktk EU, yaani husaidiwa kwa kuwa zina Uchumi dhaifu!


10. Finland, analipa Euro milioni 809 kwenye kapu la EU!
6-format2114.jpg


9.Denmark, analipa Euro milioni 836 kwenye kapu la EU!
4-format2114.jpg


8.Austria, analipa Euro bilioni 1.2!
4-format2114.jpg



7. Ubelgiji, analipa Euro bilioni 1.48!
4-format2114.jpg


6.Uswidi, analipa 2.31 Bilioni (Euro)!
3-format2114.jpg


5.Italia, analipa Euro Bilioni 4.47 !
4-format2114.jpg


4.Uholanzi, analipa Euro bilioni 4.71
3-format2114.jpg


3.Uingereza, analipa Euro Bilioni 5.6!
3-format2114.jpg


2.Ufaransa! Analipa kama Euro Bilioni 7 kwenye kapu la EU!
3-format2114.jpg


1.Ujerumani! Ujerumani inalipa Euro Bilioni 16 kwenye kapu la EU ambayo ndiyo mchangiaji mkubwa kwa mbali kuliko wote, anachangia mara mbili zaidi ya Ufaransa!
4-format2114.jpg
 
German ndio Super Power wa EU na ndio amekuwa threat kwa US.

Naona vita vya middle east vimefikia Malengo yake.
 
Duh kumbe kujitoa kwa UK kunaathiri sana kapu la EU, madhara yake hadi TZ miradi ya EU itadoda nahisi
 
Watu wakisema UK ni wabaguzi wengine wanakataa,sasa kati ya germany na UK nani alipaswa kupiga kelele?
 
Duh kumbe kujitoa kwa UK kunaathiri sana kapu la EU, madhara yake hadi TZ miradi ya EU itadoda nahisi
nchi nyingi za afrika zitaguswa na hili maana watahitaji kustablize kwanza hapo ndipo tutaisoma namba 2o_Oo_O
 
Watu wakisema UK ni wabaguzi wengine wanakataa,sasa kati ya germany na UK nani alipaswa kupiga kelele?

Tatizo Germany na Ufaransa wameifanya E.U kama ndio Shirika lao binafsi,mambo mengi wanakaa na kuamua wao wawili.
 
nchi nyingi za afrika zitaguswa na hili maana watahitaji kustablize kwanza hapo ndipo tutaisoma namba 2o_Oo_O

Lakini mchakato wa U.K kujitoa E.U na kwa Mwanachama yeyote yule kwa mujibu wa Katiba ya E.U kikao kilichofanyika Lisbon Ureno 2009 sio chini ya miaka miwili,maana kutakuwa na vikao vingi sana.
 
nilichokuwa najaribu kuangalia EU baada ya UK kujitoa GERMANY atakubali kuchukua mzigo wa UK au watafanya nn?ndio hapo tunaotegemea misaada tutakesha kwenye maombi
 
Ivi nchi ikijiunga na EU inapata faida gani hadi ichangie pesa nyingi kiasi hicho.
 
Ivi nchi ikijiunga na EU inapata faida gani hadi ichangie pesa nyingi kiasi hicho.


Kwani ulifikiri hiyo EU inaendeshwa na sasa na fedha gani? Unafikri Jumuiya yetu ya AM sisi hatuchagii fedha?
 
Ww unafikiri huko kungekuwa kuna faida uk wangejitoa?


Haya mambo ni mapana sana kuliko unavyoweza kudhania na ndiyo maana hata hiyo kura ya maoni tofauti ni ndogo, kuna mambo mengi sana kwa taarifa yako tu Uingereza wamejitoa kwenye Umoja wa Ulaya lkn bado ni sehemu ya Ulaya, hilo la kujitoa liko kisiasa zaidi, EU ina mambo mengi sana kwa mfano kuna nchi kama Uswisi, Norway hizo siyo Wanachama wa EU lkn sehemu ya Umoja huyo kwenye mambo ya kiuchumi, na mengineyo kama Ulinzi n.k kwa mfano Raia wa Uswisi au Norway ingawaje nchi siyo EU lkn wanaweza kuishi na kufanya kazi EU bila kibali na wa EU vivyo hivyo, hivyo Uingereza wamejitoa kama Mwanachama tu lkn kuna mambo mengi sana ambayo EU inafanya ambayo Uingereza hawezi kujitenga nayo kwa maana ni muhimu kwa maisha yao kiuchumi na kisiasa pia!
 
Na Tanzania inalipa bei gani kwa wazee.

swissme
Uliza inapokea bei gani, sisi wazee wakukinga mikono tu. Halafu tuna jeuri kama vile tunazo. Utasikia hatuhitaji msaada wa mtu yeyote kuiendeleza nchi yetu. Siku msaada ukija meno yote nje na kusema asante kwa msaada huu maana ulikuwa ukihitajika sana.
 
Tatizo Germany na Ufaransa wameifanya E.U kama ndio Shirika lao binafsi,mambo mengi wanakaa na kuamua wao wawili.
Hiyo kawaida kabisa mkuu, hata kwenye kampuni shareholder mkubwa ndo anasikilizagwa zaidi, aliyesema money talks hakukosea
 
Back
Top Bottom