Zijue namba za magari ya Tanzania! Pamoja na namba maalum za magari ya viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa ujumla

Siyo kila gari lazima namba yake ya usajili iandikwe kwenye kioo/vioo (huko kuandika namba kwenye vioo si utaratibu wa kisheria). Hiyo ya kuandika kwenye vioo ni watu wanaamua tu kwa kulinda vioo vyao visiibiwe. Labda kama ulikua na maana kwenye kioo kwa maana ya windshield, aangalie sticker ya Insurance. Hiyo sticker kwa gari ya serikali hutaiona kwa sababu magari ya serikali hayalipiwi insurance.
umeelewa sana point yangu ila unataka kuleta ubishi tu
 
Siyo kila gari lazima namba yake ya usajili iandikwe kwenye kioo/vioo (huko kuandika namba kwenye vioo si utaratibu wa kisheria). Hiyo ya kuandika kwenye vioo ni watu wanaamua tu kwa kulinda vioo vyao visiibiwe. Labda kama ulikua na maana kwenye kioo kwa maana ya windshield, aangalie sticker ya Insurance. Hiyo sticker kwa gari ya serikali hutaiona kwa sababu magari ya serikali hayalipiwi insurance.

Kunamoja nimeiona week mbili zilizopita MMM
Hii nayo ni nani
 
ST # A ni magari ya Ikulu
PT ni Police Tanzania na si TP kama ulivyoainisha
DFP ni Donor Funded Project hii ni badala ya TX
SU
ni Shirika la Umma
STA,...STG,STH,STK, STJ,...,STZ ni magari ya Idara nyingine za serikali pamoja na wizara
WN (abc) ni waziri wa nchi
W (abc) ni waziri
S ni Spika
NS ni Naibu Spika
JM ni Jaji mkuu
CAG ni Chief Auditor General
Uzi mzuri sana ndiyo uzuri wa JF
 
Kuna magari nimeona yana mlingoti wa bendera lakini namba zake ni SU, haya yanatumiwa na viongozi gani?
 
Hizo ST ni namba zinazowakilisha Serikali Tanzania kwa hiyo J K, just ni series, zilianza na ST, zikaja STA, STB....,STH ilvyoisha ilipaswa kuja STI lakini mara nyingi I na O huwa Zinarukwa kwa sababu ya kufanana na moja na sufuri, kama huo utaratibu hautabadilika basi hizo namba zitaenda mpaka STZ

TP Ni Tanzania Police
TP umeshaiona wp??
 
PT Police of Tanzania
 
Nauliza mwisho. Kwa nini kusiwe na consistence kwenye lugha? Kwa mfano: CS- Chief Secretary vs JM- Jaji Mkuu, n.k.
 
Hilo nalo neno. Baadhi ya taasisi zina namba plate za Kiswahili na nyingine za Kiingereza, kama CS, CAG nk.
 
Back
Top Bottom