Zijue Faida 4 za Ndoa

Zijue Faida 4 za Ndoa

Wateule

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2010
Posts
390
Reaction score
368
WANAWAKE wengi ambao hawajaolewa (Singles) wanaweza wakaangalia baadhi ya ndoa za marafiki zao na kuona mahusiano mabovu na wanandoa ambao hawana raha, lakini sio tu kwasababu eti baadhi ya wapenzi siku hizi hawaipi ndoa kipaumbele, haimaanishi kwamba ni bora zaidi kuishi kivyakovyako maisha (Stay single for life), anasema Rabbi Shmuley, anapozungumzia faida za ndoa.
Rabbi Smuley, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kijamii, kwa mfano; ndoa, mahusiano, malezi ya watoto, na pia muandishi wa vitabu 18 vyenye mauzo ya juu (Best-Selling author); anatupa faida 4 za kuwa ndani ya ndoa:
1. Utulivu na mshikamano wa watoto. Rabbi Shmuley anasema kwamba watoto wananufaika sana wanapolelewa katika nyumba ya wazazi wawili, yaani baba na mama.
2. Una mtu wa kushirikiana nae kimaisha. Kutoka kujenga familia mpaka kushirikiana majukumu na masuala yanayohusiana na majukumu hayo. Rabbi Shmuley anasema ndoa inatoa faida nyingi za muda mrefu katika masuala haya.
3. Maisha marefu. Rabbi Shmuley anasema baadhi ya tafiti zimeonysha kwamba wanandoa wanaishi maisha marefu na wana raha kuliko wale wasio kwenye ndoa.
4. Suala la kujamiina. Wanandoa wana mshirika wa uhakika linapokuja suala la kujamiina, na Rabbi Shmuley anasema hili lina faida kwa mwili na akili (mind and Body) vitu ambavyo ni muhimu kwa maisha ya mwanaadamu.
Chanzo: Oprah.com
Tafsiri: Blog ya habari Tanzania | Online Newspaper | Thehabari.com
 
Source ni oprah....anawezaje kutushauri hivo wakati

yeye mwenyeke kasema hatokaa haolewi.au hajaona hizo faida
 
Khaaa...yaani taabu zote zile za kutafuta mwenzi wa kuoa, taabu zoote za kuandaa harusi, na vimbwanga vyoote hivyo vya kuwa kwenye ndoa..yaani NDOA ina 'tufaida tunne tuu'!?
 
hana mpango ye hajazaliwa watu tumeshajua nini umuhimu wa ndoa.Nalog off
 
Khaaa...yaani taabu zote zile za kutafuta mwenzi wa kuoa, taabu zoote za kuandaa harusi, na vimbwanga vyoote hivyo vya kuwa kwenye ndoa..yaani NDOA ina 'tufaida tunne tuu'!?
Riwa tufaida tunne tunaweza kuwa na umuhimu kuliko uhai wako. Any way hicho ni chache hakuexhaust zote.
 
Ongezea ongezea nyama kwe huu uzi unawaza kuwa na impact nzuri
 
Source ni oprah....anawezaje kutushauri hivo wakati

yeye mwenyeke kasema hatokaa haolewi.au hajaona hizo faida

Lazima utofautishe Kati ya Oprah mtu na Oprah taasisi, ndio maana source imeandikwa ni oprah.com (mtandao au taasisi). Hivyo basi, kukunasua kwenye mtego wa kuchanganya mambo, hapo "source" ni Rabbi Shmuley (ndani ya website ya Oprah), ambaye ndio muandishi halisi wa faida hizo nne za ndoa, na thehabari.com imetafsiri tu kwa lugha yetu ya Kiswahili.

Natumai nimekusaidia kidogo kuelewa tofauti ya vitu hivyo viwili.

asante.
 
Khaaa...yaani taabu zote zile za kutafuta mwenzi wa kuoa, taabu zoote za kuandaa harusi, na vimbwanga vyoote hivyo vya kuwa kwenye ndoa..yaani NDOA ina 'tufaida tunne tuu'!?


Mkuu nadhani zipo nyingi ila zilizo kuu ndo hizo hapo
 
Khaaa...yaani taabu zote zile za kutafuta mwenzi wa kuoa, taabu zoote za kuandaa harusi, na vimbwanga vyoote hivyo vya kuwa kwenye ndoa..yaani NDOA ina 'tufaida tunne tuu'!?

Ni tunne tuu ILA VYA MUHIMU kulik0 unavy0dhania...
 
Back
Top Bottom