Zijue dalili za kuvamiwa na mapepo

Zijue dalili za kuvamiwa na mapepo

Urusi, China, Korea Kaskazini, idadi kubwa ya watu huko hawaamini kwamba kuna mapepo. Na wakiona sisi tunataja mapepo wanasema tuna tatizo la afya ya akili!!

Lakini angalia shetani alivyoteka fikra zao bila wao kujua. Kanisani hawaendi lakini wanatumia muda mwingi na pesa nyingi kutengeneza silaha za kuangamiza binadamu wenzao. Hayo kama sio mapepo ni nini. Yamewavamia ila wao hawajui. Kuua binadamu wenzao ndiyo furaha yao.

Kazi mojawapo ya shetani na mapepo ni kuchinja na kuua.

Yohana 10:10:
Mwivi[shetani] haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mim[Yesu]i nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Hapo Yesu anaonyesha tofauti kati yake na Shetani, kwamba Shetani (anayefananishwa na mwizi) huja ili kuharibu, lakini Yesu alikuja kuleta uzima wa milele kwa wanadamu.

SIri hii ndio shetani hataki watu waijue. Watu wakisema wana mapepo, shetani anageuza anasema ni tatizo la afya ya akili ili waendelee kuteseka maana anajua mapepo hayawezi kuondoka kwa dawa za kawaida.
Na wana ongoza kwa kuangamiza watu duniani ni watu wanao amini Mungu
USA(In God We Trust) ndio taifa linaongoza kutengeneza sila za maangamizi na ndio taifa linaongoza kuangamiza watu na kuset agenda ya ushoga duniani
Israel(Taifa teule la Mungu) lina wamwagia wapalestina mvua za mabomu utadhani sio binadamu
Iran(In Allah we trust) hawa wanaongoza kwa kufadhili vikundi vya kigaidi vinavyo leta dhama kubwa duniani kwa watu kuchinjwa kama kuku

Ukiondoa Mrusi ambaye kimsingi kwa sehemu kubwa wanaamini katika Mungu nitajie ubaya wa maangamizi mwenye mapepo wengine kama Korea na China?
Wachina na wakorea wako busy kuishi maisha HALISI na sio maisha ya KUFIKIRIKA ya kutafuta favor kwa Mungu asiyekuwepo

Stop quoting Bible verses on me kwasababu hizo ni hadithi kama hadithi zingine za sungura na fisi
 
Tayari washaitwa mapepo hata kama asili yao ni Malaika, ila walishamuasi Mungu. Ila bado kuna imani inawatambua na kuwa ngangania kuwa ni wema.
Wewe unachanganya tu mambo, hiyo imani nyengine haizungumzii kabisa malaika waliyogeuka mapepo kwa kifupi haizungumzii kabisa kuhusu mapepo. Unaweza kuonyesha ushahidi wa hiyo imani nyengine ikifundisha kuwa malaika walimuasi Mungu na kwamba bado ni wema? Hiyo imani nyengine imewazungumzia malaika mwanzo mwisho hakuna iliposema malaika waliwahi kumuasi Mungu.
 
Mapepo ni malaika walioasi mbinguni, wakafukuzwa pamoja na shetani, wakatupwa duniani.

Ufunuo 12:7-9:
Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake. Lakini hawakushinda, wala mahali pao hapakuwapo tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule joka mkubwa wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake[mapepo] wakatupwa pamoja naye.

Andiko hili linaonyesha kwamba Shetani (anayeitwa joka) aliasi mbinguni na akaangushwa pamoja na malaika walioshirikiana naye kufanya uasi, ambao sasa ndio wanajulikana kama mapepo.
Sasa mbona huwa mnachanganya hao mapepo(malaika) na majini?
 
Na wana ongoza kwa kuangamiza watu duniani ni watu wanao amini Mungu
USA(In God We Trust) ndio taifa linaongoza kutengeneza sila za maangamizi na ndio taifa linaongoza kuangamiza watu na kuset agenda ya ushoga duniani
USA sio holy nation bwana. Kuna Wakristo wa kweli kabisa, lakini wenye mashetani hawakosekani. Hao ndio wanaotetea ushoga. Na hao ukiwaambia wana mapepo watakuambia hivyohivyo una tatizo la afya ya akili. Kwahiyo point yangu ile ni kwamba hata walioendelea kiuchumi bado mapepo yanawaingia kwa njia ambazo wao hawaoni kuwa ni mapepo.
Israel(Taifa teule la Mungu) lina wamwagia wapalestina mvua za mabomu utadhani sio binadamu
Iran(In Allah we trust) hawa wanaongoza kwa kufadhili vikundi vya kigaidi vinavyo leta dhama kubwa duniani kwa watu kuchinjwa kama kuku
Israeli bado wanaongozwa na Torati - Jino kwa jino. Ndio sababu wakipigwa na wao wanashusha kipigo. Wakristo hatuongozwi na sheria hiyo. Kwetu sisi mtu "akupigaye shavu la kushoto, unamgeuzia na la kulia."
Wachina na wakorea wako busy kuishi maisha HALISI na sio maisha ya KUFIKIRIKA ya kutafuta favor kwa Mungu asiyekuwepo
Maisha ya kufikirika? Historia inaonyesha wazi kuwa imani katika Mungu imewasaidia mamilioni ya watu kuwa na matumaini, maadili mema, na mwelekeo mzuri wa maisha.
Stop quoting Bible verses on me kwasababu hizo ni hadithi kama hadithi zingine za sungura na fisi
I acknowledge your prerogative to maintain skepticism, yet to juxtapose the Bible with puerile allegories of anthropomorphic creatures is to engage in a grossly reductive and intellectually disingenuous dismissal of one of history’s most profoundly consequential texts. Unlike jejune fables concocted for mere amusement, the Bible is an unparalleled compendium of theological profundity, moral jurisprudence, and historical gravitas. Its didactic precepts have undergirded entire civilizations, engendered epochal philosophical discourses, and served as the lodestar for ethical paradigms spanning millennia. To cavalierly relegate it to the realm of mythos without meticulous exegetical scrutiny betrays not only a lack of scholarly inquisitiveness but also an unexamined predisposition toward secular dogmatism.
 
USA sio holy nation bwana. Kuna Wakristo wa kweli kabisa, lakini wenye mashetani hawakosekani. Hao ndio wanaotetea ushoga. Na hao ukiwaambia wana mapepo watakuambia hivyohivyo una tatizo la afya ya akili. Kwahiyo point yangu ile ni kwamba hata walioendelea kiuchumi bado mapepo yanawaingia kwa njia ambazo wao hawaoni kuwa ni mapepo.

Israeli bado wanaongozwa na Torati - Jino kwa jino. Ndio sababu wakipigwa na wao wanashusha kipigo. Wakristo hatuongozwi na sheria hiyo. Kwetu sisi mtu "akupigaye shavu la kushoto, unamgeuzia na la kulia."

Maisha ya kufikirika? Historia inaonyesha wazi kuwa imani katika Mungu imewasaidia mamilioni ya watu kuwa na matumaini, maadili mema, na mwelekeo mzuri wa maisha.

I acknowledge your prerogative to maintain skepticism, yet to juxtapose the Bible with puerile allegories of anthropomorphic creatures is to engage in a grossly reductive and intellectually disingenuous dismissal of one of history’s most profoundly consequential texts. Unlike jejune fables concocted for mere amusement, the Bible is an unparalleled compendium of theological profundity, moral jurisprudence, and historical gravitas. Its didactic precepts have undergirded entire civilizations, engendered epochal philosophical discourses, and served as the lodestar for ethical paradigms spanning millennia. To cavalierly relegate it to the realm of mythos without meticulous exegetical scrutiny betrays not only a lack of scholarly inquisitiveness but also an unexamined predisposition toward secular dogmatism.
Hicho kimombo ulichotema umenitoa kapa kabisa😂😂
 
Hicho kimombo ulichotema umenitoa kapa kabisa😂😂
Ah, my apologies if my linguistic embellishments left you in a state of bewilderment! Perhaps I should recalibrate my diction to a more palatable level. But in essence, my point remains—dismissing the Bible as mere fable is an oversimplification that disregards its historical and philosophical gravitas.
 
Kuna siku nilikuwa nimelala usiku, ghafla nikahisi kitu kizito sana kinanikandamiza kifuani. Nilijua haraka sana ni pepo, nikakemea kwa Jina la Yesu. Mgandamizo ukatoweka, nikalala shwari.
Hali iliyokutokea inaelezeka kisayansi, Google Sleep Paralysis
 
Kwanini wanaoanguka mapepo kwa 99% ni wanawake?

Au ndio tuseme shetani na jinsia ya kike ni mabest tangu bustani ya Eden?
Wanawake kuanguka wakati wa maombezi sio ishara kwamba mapepo yanashambulia zaidi wanawake. Kwanza, wanawake mara nyingi ndio wengi zaidi katika mikutano ya injili, hivyo ni rahisi kuwaona wakihusika zaidi. Pili, wanawake kwa asili huwa na hisia za wazi zaidi kuliko wanaume, hivyo mwitikio wao wa kiroho unaweza kudhihirika kwa njia kama hiyo. Biblia inaonyesha kuwa mapepo hayabagua jinsia—Yesu alitoa pepo wachafu kwa wanaume na wanawake (Marko 5:2-13, Luka 8:2).
 
Hali iliyokutokea inaelezeka kisayansi, Google Sleep Paralysis
Sleep paralysis, as explained scientifically, usually fades on its own after a short while. However, in my case, the oppression disappeared instantly when I rebuked it in the name of Jesus. If it were just a natural condition, why did it stop immediately at the mention of His name? This aligns more with a spiritual attack than a mere sleep disorder. Many people have encountered similar attacks and found deliverance through the name of Jesus. Science may explain the mechanics, but it does not negate the power of Jesus over spiritual forces. Not everything can be fully explained by science alone—spiritual realities do not necessarily contradict scientific explanations, but neither can they be reduced to them alone.
 
Hizi ni stori za ki-stone tu.
Aah, kwanini nikuletee stori za ki-stone, kwani hapa JF ni stonini? Acha kumfurahisha shetani na mapepo yake. Hao ma-demons wameishahukumiwa kwenda motoni. Wanaijua vizuri raha ya mbinguni. Hawataki wewe uingie mbinguni; wanataka wewe uende nao motoni, ndio sababu usiku na mchana wanafanya kazi ya kuwadanganya watu wasiamini mambo ya kiroho.
 
Dalili za kuvamiwa na mapepo zinaweza kutofautiana kulingana na aina ya mapepo na kiwango cha uvamizi.

Kulingana na Biblia na mafundisho ya Kikristo, dalili zinaweza kuwa za kimwili, kiakili, kihisia, na kiroho. Nakutajia hapa baadhi ya dalili kuu:

1. Dalili za Kiroho:
Chuki au upinzani mkali dhidi ya maombi, Biblia, na mambo ya kiroho.

Kushindwa kuomba au kusoma Biblia, hata kama unataka kufanya hivyo.

Kusikia sauti au maono ya kipepo yanayokuongoza mbali na Mungu.

Kufanya au kuvutwa na matendo ya uchawi, mizimu, na nguvu za giza.

Kupenda kushiriki katika ibada za kishetani au matambiko yanayohusiana na mapepo.

2. Dalili za Kihisia na Kiakili:
Kuhisi unafanya tendo la ndoa(usiku) na mme au mke asiye wako, na unajisikia furaha zaidi kuliko inavyokuwa kwa mke au mme wako halisi. Mke au mme wako unahisi kumchukia tu bila sababu yoyote.

Hofu isiyo ya kawaida, huzuni, au msongo wa mawazo bila sababu za msingi.

Kutamani kupata pesa na utajiri kwa njia za giza au maovu.

Kuota ndoto mbaya mara kwa mara, zinazokutisha na kukukosesha amani.

Kupata msukumo wa kujiua au kuua wengine.

3. Dalili za Kimwili:
Kupatwa na magonjwa yasiyoeleweka na madaktari, hasa ikiwa yanahusiana na maumivu ya ghafla, kuhisi moto mwilini au kuona moshi wakati watu walio karibu na wewe hawaoni

Hujaokoka lakini unasema kwa lugha usiyoijua, hasa wakati wa maombi ya kukemea pepo kanisani au katika mkutano wa Injili. [Mtu aliyeokoka akinena kwa lugha asiyoijua hiyo ni dalili ya kujazwa Roho Mtakatifu].

Kuhisi maumivu au shinikizo mwilini unapokaribia mahali patakatifu, kama kanisani au unapowakaribia watumishi wa kweli wa Mungu.

4. Dalili za Kimaisha:
Kupata mikosi ya mara kwa mara, hasa katika maeneo mbalimbali ya maisha bila sababu inayoeleweka.

Kushindwa kubadilika au kuacha maisha ya dhambi hata baada ya kujaribu mara nyingi.

Kuwa na roho ya uasi, kiburi cha kupindukia, au chuki isiyoelezeka dhidi ya watu wa Mungu.

Kupata mvuto wa ajabu kwenye mambo ya giza, mizimu, au hadithi za kishetani.

Ukiona dalili hizo kwako au kwa mtu mwingine ujue hizo ni dalili za kuvamiwa na mapepo. Nini cha Kufanya?

Tafuta msaada wa kiroho.

Omba maombi/sala ya toba. Mruhusu Yesu Kristo awe Mwokozi na Mlinzi wa maisha yako.

Funga na kuomba kwa dhati ili kuvunja nguvu za giza.

Kubali Watumishi wa kweli wa Mungu wakufanyie maombi ya kukufungua kutoka katika nguvu za giza.

Acha matendo yote yanayotoa nafasi kwa mapepo, kama uchawi, ushirikina, uzinzi na dhambi za makusudi.

Mungu akubariki. Mungu akulinde na kukuweka huru mbali na uvamizi wa mapepo, katika Jina la Yesu Kristo. Amen
Na anaepinga hiyo post ana mapepo maana anampinga mtumishi wa Mungu
 
Kuna tajiri mmoja alivamiwa na mapepo. Nyumbani kwake friji ilikuwa inaruka ruka juu. Baada ya pepo kukemewa na Mtumishi wa Mungu, hali hiyo ikaisha.
"Friji ilikuwa inaruka ruka juu" sijaelewa hapo msaada tafadhari
 
Back
Top Bottom