Zijue dalili za kuvamiwa na mapepo

Zijue dalili za kuvamiwa na mapepo

Kwanini wanaoanguka mapepo kwa 99% ni wanawake?

Au ndio tuseme shetani na jinsia ya kike ni mabest tangu bustani ya Eden?
 
Kwenye Nchi za wale watu wenye ngozi nyeupe hawatambui uliyotaja kama mapepo bali Mental Disorders

Ukiona unapitia hali zilizotajwa hapo juu kabla ya kuzunguka kwenye Makanisa ya Mwamposa pita pale idara ya magonjwa ya akili Muhimbili; utaambiwa una schizophrenia, msongo wa mawazo na diet yako mbovu ya kushindia maharage na mihogo (umaskini) imezalisha gesi tumboni ambayo inakufanya ujisikie unawehuka
 
Dalili za kuvamiwa na mapepo zinaweza kutofautiana kulingana na aina ya mapepo na kiwango cha uvamizi.

Kulingana na Biblia na mafundisho ya Kikristo, dalili zinaweza kuwa za kimwili, kiakili, kihisia, na kiroho. Nakutajia hapa baadhi ya dalili kuu:

1. Dalili za Kiroho:
Chuki au upinzani mkali dhidi ya maombi, Biblia, na mambo ya kiroho.

Kushindwa kuomba au kusoma Biblia, hata kama unataka kufanya hivyo.

Kusikia sauti au maono ya kipepo yanayokuongoza mbali na Mungu.

Kufanya au kuvutwa na matendo ya uchawi, mizimu, na nguvu za giza.

Kupenda kushiriki katika ibada za kishetani au matambiko yanayohusiana na mapepo.

2. Dalili za Kihisia na Kiakili:
Kuhisi unafanya tendo la ndoa(usiku) na mme au mke asiye wako, na unajisikia furaha zaidi kuliko inavyokuwa kwa mke au mme wako halisi. Mke au mme wako unahisi kumchukia tu bila sababu yoyote.

Hofu isiyo ya kawaida, huzuni, au msongo wa mawazo bila sababu za msingi.

Kutamani kupata pesa na utajiri kwa njia za giza au maovu.

Kuota ndoto mbaya mara kwa mara, zinazokutisha na kukukosesha amani.

Kupata msukumo wa kujiua au kuua wengine.

3. Dalili za Kimwili:
Kupatwa na magonjwa yasiyoeleweka na madaktari, hasa ikiwa yanahusiana na maumivu ya ghafla, kuhisi moto mwilini au kuona moshi wakati watu walio karibu na wewe hawaoni

Hujaokoka lakini unasema kwa lugha usiyoijua, hasa wakati wa maombi ya kukemea pepo kanisani au katika mkutano wa Injili. [Mtu aliyeokoka akinena kwa lugha asiyoijua hiyo ni dalili ya kujazwa Roho Mtakatifu].

Kuhisi maumivu au shinikizo mwilini unapokaribia mahali patakatifu, kama kanisani au unapowakaribia watumishi wa kweli wa Mungu.

4. Dalili za Kimaisha:
Kupata mikosi ya mara kwa mara, hasa katika maeneo mbalimbali ya maisha bila sababu inayoeleweka.

Kushindwa kubadilika au kuacha maisha ya dhambi hata baada ya kujaribu mara nyingi.

Kuwa na roho ya uasi, kiburi cha kupindukia, au chuki isiyoelezeka dhidi ya watu wa Mungu.

Kupata mvuto wa ajabu kwenye mambo ya giza, mizimu, au hadithi za kishetani.

Ukiona dalili hizo kwako au kwa mtu mwingine ujue hizo ni dalili za kuvamiwa na mapepo. Nini cha Kufanya?

Tafuta msaada wa kiroho.

Omba maombi/sala ya toba. Mruhusu Yesu Kristo awe Mwokozi na Mlinzi wa maisha yako.

Funga na kuomba kwa dhati ili kuvunja nguvu za giza.

Kubali Watumishi wa kweli wa Mungu wakufanyie maombi ya kukufungua kutoka katika nguvu za giza.

Acha matendo yote yanayotoa nafasi kwa mapepo, kama uchawi, ushirikina, uzinzi na dhambi za makusudi.

Mungu akubariki. Mungu akulinde na kukuweka huru mbali na uvamizi wa mapepo, katika Jina la Yesu Kristo. Amen
Hebu Noel ewe she una maana gani kusema “kusikia sauti au maono ya kipepo yanayokuongoza mbali na Mungu.”
 
Kwa kweli Kuna saa, ukisoma maandiko ya watu kama atheist wanaopinga uwepo wa Mungu Kuna saa wanajenga hoja hadi unaanza kuamini hizo hoja vipi kuhusu hilo? Nalo ni mawinds
Pia hili linahusu mm, Nikitaka ku do na mwanamke napokaa na biblia chumbani nimewekaa juu ya vitabu Ila nikifikia ku do sx ni lazma niitoe pale ile biblia niifiche hata chini ya ufungu au kokote pale
Hiyo ni dalalli ghani.
*******
 
Umeandika kwa utuo dalili za kupatwa na mapepo
Nikakwambia kwanini tusio amini katika Imani hatupatwi na mapepo?
Umekimbilia kunukuu barua ya Paulo aliyo waandikia Wakorintho...... inahusiana nini na dalili ulizo zitaja hapo awali?

Hapa issue sio kuamini au kutokuamini
Issue ni kwanini hayo mapepo hayatupati tusio amini yana wapata mnao amini?
Soma vizuri uzi. Nimekutajia baadhi tu ya dalili...

Paulo ni Mtumishi wa Mungu. Matendo aliyokuwa akifanya kabla hajaokoka yalikuwa ya kipepo kabisa. Akili zake zilikuwa zimepofushwa.

Shetani ni mjanja. Ana mbinu nyingi za kuwateka, kuwaonea na kuwatawala watu - silently or overtly. Of course mapepo yakiishapofusha akili zako yanaweza yasihangaike na wewe kwa sababu tayari yanajua wewe ni mtu wao. Utajiona uko vizuri tu lakini umeishapofushwa. Kutoamini ni kupofushwa kifikra.
 
Hehee, umenichekesha 🙂
Katika dalili hizo, niambie umeona dalili gani kwangu.

Mimi mapepo hayaniwezi. Yanakuja mara nyingi kutaka kunidhuru lakini kwa Jina la Yesu nayasambaratisha.
Samahani, hivi ni jina la Yesu au majina ya Yesu? Maana naona kama Yesu ana majina mengi.
 
Umeandika ukweli ila utapigwa na wanao amini katika Imani zao kuwa mapepo ni viumbe wazuri hadi wanasali nao katika majumba yao ya ibada.
 
Matajiri hatuoni mambo yao mengi sana hata yale ambayo tunajua wanayo kama binaadamu.
Kwahiyo mimi nisiye amini Mungu nina mapepo? 😂😂😂

Hizi imani tulizo letewa na majahazi zime haribu kabisa akili zetu aiseee
 
Hivi hayo mapepo kwanini yana wasumbuaga sana watu mnao Amini Mungu na Imani za ajabu ajabu tu?

Mbona sisi tusio amini kwenye hayo mambo ya imani hatuguswi na hayo matakataka
Unakusudia nyie kwa hapa afrika?
 
Umeandika ukweli ila utapigwa na wanao amini katika Imani zao kuwa mapepo ni viumbe wazuri hadi wanasali nao katika majumba yao ya ibada.
Kwani malaika ni viumbe wabaya kusali nao? Hao mapepo si inasemwa kuwa ni malaika kiasili?
 
Kwahiyo mimi nisiye amini Mungu nina mapepo? 😂😂😂

Hizi imani tulizo letewa na majahazi zime haribu kabisa akili zetu aiseee
Wapi nimesema wewe usiyeamini Mungu una mapepo?

Halafu hata wewe hiyo misimamo uliyo nayo ni ya kuletewa.
 
Hizi imani tulizo letewa na majahazi zime haribu kabisa akili zetu aiseee
Urusi, China, Korea Kaskazini, idadi kubwa ya watu huko hawaamini kwamba kuna mapepo. Na wakiona sisi tunataja mapepo wanasema tuna tatizo la afya ya akili!!

Lakini angalia shetani alivyoteka fikra zao bila wao kujua. Kanisani hawaendi lakini wanatumia muda mwingi na pesa nyingi kutengeneza silaha za kuangamiza binadamu wenzao. Hayo kama sio mapepo ni nini. Yamewavamia ila wao hawajui. Kuua binadamu wenzao ndiyo furaha yao.

Kazi mojawapo ya shetani na mapepo ni kuchinja na kuua.

Yohana 10:10:
Mwivi[shetani] haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mim[Yesu]i nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Hapo Yesu anaonyesha tofauti kati yake na Shetani, kwamba Shetani (anayefananishwa na mwizi) huja ili kuharibu, lakini Yesu alikuja kuleta uzima wa milele kwa wanadamu.

SIri hii ndio shetani hataki watu waijue. Watu wakisema wana mapepo, shetani anageuza anasema ni tatizo la afya ya akili ili waendelee kuteseka maana anajua mapepo hayawezi kuondoka kwa dawa za kawaida.
 
Kwani malaika ni viumbe wabaya kusali nao? Hao mapepo si inasemwa kuwa ni malaika kiasili?
Tayari washaitwa mapepo hata kama asili yao ni Malaika, ila walishamuasi Mungu. Ila bado kuna imani inawatambua na kuwa ngangania kuwa ni wema.
 
Kwani malaika ni viumbe wabaya kusali nao? Hao mapepo si inasemwa kuwa ni malaika kiasili?
Mapepo ni malaika walioasi mbinguni, wakafukuzwa pamoja na shetani, wakatupwa duniani.

Ufunuo 12:7-9:
Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake. Lakini hawakushinda, wala mahali pao hapakuwapo tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule joka mkubwa wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake[mapepo] wakatupwa pamoja naye.

Andiko hili linaonyesha kwamba Shetani (anayeitwa joka) aliasi mbinguni na akaangushwa pamoja na malaika walioshirikiana naye kufanya uasi, ambao sasa ndio wanajulikana kama mapepo.
 
Back
Top Bottom