Zijue Athari Za Kula Chipsi, Moja Kati Ya Chakula Pendwa Zaidi Duniani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
Chipsi ni moja kati ya chakula kinanchopendwa zaidi duniani.jpg



Chipsi ni moja kati ya chakula kinanchopendwa zaidi duniani

KIUKWELI katika vyakula vitamu duniani na vinavyopendwa haswaa na watu duniani usiposema chipsi utakuwa mtu waajabu sana. Chipsi haziliki bongo tu ata ughaibuni chips zinalika sana na zinapendwa haswaa, chipsi zinaenda na vitu vingi kama chipsi yai, chipsi kuku na kadharika.

Hizi ndio athari za ulaji wa chipsi.

  • Husababisha magonjwa ya moyo
Kwa kuzingatia ukweli kwamba zimekaangwa sana katika mafuta ya hidrojeni, chipsi huja na kiasi kikubwa cha mafuta, ambayo huongeza cholesterol yako mbaya na kupunguza cholesterol yako nzuri. Athari kubwa ya hii ni kwamba utaongeza hatari ya ugonjwa wa moyo.

Ulaji wa chipsi husababisha magonjwa ya moyo.jpg

Ulaji wa chipsi husababisha magonjwa ya moyo
  • Hupunguza kinga ya mwili
Kulingana na utafiti uliochapishwa katika jarida la Current Opinion in Clinical Nutrition & Metabolic Care, kula chakula chenye mafuta mengi na vyakula vyakukaanga vingi unaweza kuwa unaharibu utumbo wako kwa kuongeza bakteria wasio na afya na kupunguza bakteria wa afya ya mwili wako. Kwa kuzingatia jukumu la utumbo katika kusaidia kufahamisha mfumo wa kinga ya mwili wako, unaweza kuwa unaweka mwili wako hatarini kupata magonjwa.

  • Huongeza uzito wa mwili
Vyakula vya kukaangwa katika mafuta, huwa mabomu ya kalori, na kusababisha kupata uzito. Utafiti uliochapishwa katika jarida la The American Journal of Clinical Nutrition uligundua kuwa kula vyakula vya kukaanga kunahusishwa moja kwa moja na unene kupita kiasi.
Chipsi huongeza uzito wa mwili.jpg

Chipsi huongeza uzito wa mwili. chanzo GBP
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom