Ziara za kushutikiza za Magufuli ziliishia wapi?

Ziara za kushutikiza za Magufuli ziliishia wapi?

Tukubaliane tu kuwa kuna wanafiki wengi. Wanaoponda utawala wa Jk ndio hahao waliokuwa wakimsifia. Sasa wamahamia kwa Jpm na baadae watamponda pia ili mradi wanapalilia kitumbua chao. Naomba JPM awaangalie hawa wanafiki kwa jicho kali
 
Wewe mpk sikujua kama wewe ni kimeo. Yani unataka rais afanye jambo hilo hilo mwaka mzima? Hujui kuwa kuonyesha mfano ni tija ili wengine waendeleze? Usiku mwema ngoja nikiamka kesho nitakupasha vizuri zaidi
 
Akina nani sasa wanaendeleza? Nadhani ungenijibu ziara zimeishia wapi na nani alimpokea kazi hiyo
 
Siamini kama kuna watu wameajiriwa kutoona ukweli bali wanaojipendekeza kutoona ukweli na ambao nadhani ndiyo hawana kazi

Na namba utaisoma

Uhuru hiyo inakuja fagio umeshalitayarisha...usafi mbele kwa mbele

#hapakazitu
 
we mtoa uzi unaishi wapi? ziara mbili tu za kushtukiza za jpm zimeleta amshaamsha kila mahali. wasimamizi wanaboresha utendaji uendane na kasi ya magufuli wa hapa kazi tu. we kalagabaho.
 
Umeuliza alafu ukajijibu na kupoteza maana ya swali lako

Ungekuwa unetulia na kufikiria vizur kwanini kauliza na kujijibu basi usingemjibu hivyo, bahat mbaya hujui hata maana ya rhetorical question
 
Kilaza ni yule anayesifia kila kitu bila kuhoji. Ni sawa na wale waliosifia ziara za Mkwere lakini leo wanamsifia JPM kuzifuta

Magufuli hajafuta ziara za rais wewe raia na hajafuta kabisa ziara zozote.
 
Wewe mpk huyu ni mkuu wa nchi kuna mengi ya kufanya zaidi ya ziara, kwa upeo wako pamoja na kwamba hajafanya ziara nyingine huoni mengine aliyoyafanya yenye umuhimu kuliko ziara? So far wakati anakwenda muhimbili hakukupa taarifa basi subiri hata kwingine hatakupa taarifa
 
Nilijua tu kwamba ulikuwa moto wa mabua na nguvu za soda. Jiulize alipoenda Muhimbili mambo gani yalikuwa yanaendelea bandarini? Kama angeenda bandalini mambo gani yangekuwa yanaendelea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere?

Kama angekuwa uwanja wa ndege nini kingeendelea TRA? Kama angekuwa TRA nini kingeendelea Makao makuu ya Jeshi la polisi? nk nk nk. Hatutaki siasa nyepesi, tufuate sheria na tufanye kazi.
Ewe nyumbu, tumia kichwa kufikiri. Hapa kazi tu
 
sasa ukimkejeli rais na yeye ni rais wako inakusaidia nini? zaid ya kujipa presha?

lowassa bana
 
we mtoa uzi unaishi wapi? ziara mbili tu za kushtukiza za jpm zimeleta amshaamsha kila mahali. wasimamizi wanaboresha utendaji uendane na kasi ya magufuli wa hapa kazi tu. we kalagabaho.

Sijiauliza zimeleta nini bali zimeishia wapi
 
Kuna njia kibao anazotumia kufika sema ukiwa chizi huwezi kuziona, na katika mambo ya kushtukiza rais wetu ni master.
 
Back
Top Bottom