Ziara ya Rais Masisi: Wakubaliana na Rais Samia kuendeleza Sekta ya Madini na kufufua Tume ya Pamoja ya Ushirikiano

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
330
1,000

Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mokgweetsi Masisi amewasili kwa na ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania, kuanzia leo Juni 10, 2021 kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Viongozi hao wawili wanatarajia kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya nchi mbili, uhusiano wa kidiplomasia, matumizi ya lugha ya Kiswahili nchini Botswana, bishara na uchumi pamoja na namna ya kuimarisha zaidi Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)

Updates:

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN:

UHUSIANO WA BOTSWANA NA TANZANIA NI TANGU ENZI ZA UKOMBOZI
“Karibu sana Rais Masisi, ziara yako nchini inatoa fursa ya kukuza uhusiano na urafiki wa kihistoria kati ya Botswana na Tanzania, uhusiano wetu ulianza tangu enzi za harakati za ukombozi, Tanzania, Botswana na Zambia zilikuwa mstari wa mbele kwenye kupigania Uhuru”

BIASHARA KATI YA NCHI MBILI IMEONGEZEKA
“Biashara kati ya Tanzania na Botswana imeongezeka kutoka Tsh. Milioni 731 mwaka 2005 hadi Tsh. Bilioni 3.5 mwaka huu, Botswana imewekeza nchini miradi yenye thamani ya USD Milioni 231 ambayo imetoa ajira 2128 kwa Watanzania”

MLIMANI CITY NI UWEKEZAJI WA WABOTSWANA
“Miongoni mwa miradi mikubwa ambayo Botswana wamewekeza Tanzania ni mradi wa Mlimani City, wengi tunakwenda pale kununua tunakwenda na Watoto wanacheza na nini lakini ni Uwekezaji wa Wabotswana walioingia mkataba pamoja na Chuo Kikuu cha DSM”

“Nimuhakikishie Rais Masisi kwamba tutalinda mradi wa Mlimani City (ambao Mwekezaji ni Botswana pamoja na UDSM) ili mradi ule uendelee kwa muda mrefu kwasababu mbali na biashara mradi ule umekuwa kivutio kwa Watanzania wengi”

WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA BOTSWANA
“Tumekubaliana kuwahamasisha Wafanyabiashara wa Nchi zetu kuchangamkia fursa zilizopo, Botswana inasifika kwa kupiga hatua kubwa kiuchumi Afrika ambapo inaongoza kwa kuuza Madini ya Almasi Duniani ila haiongozi kwa bahati mbaya ilijipanga nasi tumejifunza mengi kwao”

KUFUFUA TUME YA PAMOJA YA USHIRIKIANO
“Tumekubaliana kufufua Tume ya pamoja ya ushirikiano ambayo ilianzishwa mwaka 2002 na kufanya mkutano wake wa mwisho mwaka 2009 tumewataka Mawaziri wetu wa Mambo ya Nje kuitisha mara moja ili kuangalia maeneo ya ushirikiano ya kiuchumi na kijamii kwa undani zaidi”

NITATEMBELEA BOTSWANA
“Kutembelea kwa Rais Masisi Tanzania na tuliyompangia kufanya, kumempa hamu na yeye anialike Mimi kwenda kwake (Botswana) na nimepokea mwaliko huo na nimemuahidi nitatembelea Botswana wakati utakaporuhusu”

SuluhuMasisi.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Botswana, Dkt. Mokgweetsi Masisi, Dar es Salaam

RAIS WA BOTSWANA, DKT. MOKGWEETSI ERIC KEABETSWE MASISI:

KUFUFUA TUME YA USHIRIKIANO, MAWAZIRI WAANZE KUKUTANZA NDANI YA MIEZI 3
“Tumewaelekeza mawaziri wetu wa mambo nje kuweza kufufua ile tume ya ushirikiano na waanze kukutana ndani miezi mitatu, lazima wayabainishe maeneo ya ushirikiano ambayo mimi na wewe tumeyajadili ambayo ni utalii, mifugo, ulinzi na usalama pamoja na Corona,”

NIMEKUALIKA BOTSWANA KAMA RAFIKI NA KAMA DADA YANGU
“Nataka nikwambie mheshimiwa rais, kama kuna mtu alidhani unajialika mwenyewe Botswana nataka nitamke kwamba ni mimi ninayekualika. Ninakualika kama rafiki unawakilisha Watanzania lakini pia kama dada yangu,”

Njoo ili tuweze kushirikishana uzoefu wetu kwenye sekta ya madini namna ambavyo tunachimba na namna ambavyo tunanufaika na madini,”

“Utakuja kujionea mwenyewe namna ambavyo mahusiano yetu ya kidemokrasia yametusaidia kupata maji kutoka Angola na namna ambavyo tunatumia maji hayo,”

“Botswana ipo karibu sana, unaweza kupata kifungua kinywa Dar au Dodoma na ukapata chakula cha mchana Botswana,”
 
Midevu

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
237
500
Tunajipambanua kama wapigania Kiswahili lakini elimu yetu bado ipo kwa lugha ya mkoloni. Hayo yote licha ya tafiti juu ya tafiti kuonesha kwamba Kiswahili kina ufanisi zaidi kufundishia katika mazingira yetu na sera yetu ya elimu inataka hivyo.
 
Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,794
2,000
Rais Samia amesema wamekubaliana na Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi kushirikiana ambapo wataalamu wa Tanzania wataenda kujifunza kuhusu kuendeleza madini nchini Botswana.

Amesema wamefikia makubaliano hayo kwa kuwa Tanzania ina madini mengi lakini kibiashara Botswana inafanya vizuri kuliko Tanzania.

TANZANIA NA BOTSWANA KUFUFUA TUME YA USHIRIKIANO

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania na Botswana zimekubaliana kufufua Tume ya Pamoja ya Ushirikiano iliyoanzishwa 2002 na kufanya mkutano wake wa mwisho 2009

Amesema, "Tumewataka Mawaziri wetu wa Mambo ya Nje kuitisha mara moja mkutano huu. Kwasababu kuna Magonjwa yanatuzuia kukutana pamoja, tutaangalia njia rahisi"

BOTSWANA IMEWEKEZA MLIMANI CITY

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Biashara kati ya Tanzania na Botswana imeongezeka kutoka Tsh. Milioni 731 (2015) hadi kufikia Tsh. Bilioni 3.5. Imeelezwa, Taifa hilo limewekeza miradi yenye thamani ya Dola Milioni 231 iliyotoa Ajira takriban 2,128

Ameeleza, "Miongoni mwa Miradi mikubwa waliyowekeza ni Mlimani City. Wengi tunaenda kununua na watoto wanacheza lakini ni Uwekezaji wa Botswana walioingia Mkataba pamoja na Chuo Kikuu cha Dar (UDSM)"

E3hQkLbXMAcRlAV.jpg

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,353
2,000
Tatizo la Tanzania na madini yake sio elimu, madini tayari tunayo na yanajulikana duniani kote na bei zake, tatizo letu ni ulafi wa viongozi wa CCM na serikali yake wanaosaini mikataba mibovu wanachukua 10% kwa manufaa yao binafsi na kuwaacha wananchi na umasikini wa kutupa.
 
Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,787
2,000
Ni vizuri ila wasije na mapendekezo ya kinyonyaji kama kipindi cha nyuma.

Tuendelee kuwabana hao wawekezaji kama sheria invyotaka, tumeshabadilisha sheria mpaka tukaanzisha kampuni ya Twiga, amabyo ina hisa kwenye madini.

Tusipokuwa makini hao hao wataalum wetu wataturudisha kulekule
 
kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
4,329
2,000
Nadhani Tanzania 🇹🇿 ina mchango wake Botswana 🇧🇼 iweje leo tena twende kujifunza
Nimekumbuka mawese ya Kigoma kwenda malaysia 🇲🇾 then tunaenda Malaysia kujifunza kuhusu mawese🥶
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,956
2,000
Mnataka kufuja mali za umma kulipana posho bure na wakati miaka yote wanaenda hatuoni mabadiliko
Mstari mmoja unaosema yote ndani ya kurasa mia moja!

Hivi kuna mwaka ambapo tutampata kiongozi ambaye atasimama na kusema "SASA INATOSHA", na kuanza kusimamia hawa watu wote tulionao hapa wafanye kazi na kuleta matokeo yanayoonekana?

Nchi hii haina upungufu wa wataalam katika eneo lolote tunalohitaji litusaidie kuleta maendeleo; bali tuna upungufu mkubwa sana wa kuwasimamia na kuhakikisha wataalam hawa wanatimiza wajibu wao kwelikweli.

Nadhani tunamhitaji kiongozi anayeweza kutumia MABAVU katika eneo hili, kama yale ya Magufuli, bila ya yale mabovu yake mengine.
Mimi nipo tayari kumuunga mkono kiongozi wa namna hiyo wakati huu.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,062

Tatizo ni sera zetu mbovu, wataalam hawalipwi vizuri lakini wabunge wagonga meza wanalipwa vizuri sn
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,956
2,000
Nadhani Tanzania 🇹🇿 ina mchango wake Botswana 🇧🇼 iweje leo tena twende kujifunza
Nimekumbuka mawese ya Kigoma kwenda malaysia 🇲🇾 then tunaenda Malaysia kujifunza kuhusu mawese🥶
Na KOROSHO ya Vietnam je!

Mbona yapo mengi sana ya aina hii, ambayo kama tungekuwa makini nayo nchi hii ingekuwa na hali tofauti sana na iliyopo sasa!

Na bado, hata kushtuka tu bado; tunaendelea tuuu vilevile kama hatuoni kitu!
 
Mikono yenye Sugu

Senior Member
Jul 1, 2020
133
250
Tunajipambanua kama wapigania Kiswahili lakini elimu yetu bado ipo kwa lugha ya mkoloni. Hayo yote licha ya tafiti juu ya tafiti kuonesha kwamba Kiswahili kina ufanisi zaidi kufundishia katika mazingira yetu na sera yetu ya elimu inataka hivyo.
Najiona mwenye hatia nisipopongeza maoni yako! Asante! Ni Kiswahili kitakachowakomboa Watanzania na sio lugha ya kigeni. Tunaweza kujifunza lugha hizo lakini Kiswahili kikawa lugha kuu ya kufundishia kama tunavyokitumia kwenye mawasiliano.
 
kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
4,329
2,000
Na KOROSHO ya Vietnam je!

Mbona yapo mengi sana ya aina hii, ambayo kama tungekuwa makini nayo nchi hii ingekuwa na hali tofauti sana na iliyopo sasa!

Na bado, hata kushtuka tu bado; tunaendelea tuuu vilevile kama hatuoni kitu!
Duuuh
Kumbe hadi korosho 🤔🤔
 
Midevu

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
237
500
Najiona mwenye hatia nisipopongeza maoni yako! Asante! Ni Kiswahili kitakachowakomboa Watanzania na sio lugha ya kigeni. Tunaweza kujifunza lugha hizo lakini Kiswahili kikawa lugha kuu ya kufundishia kama tunavyokitumia kwenye mawasiliano.
Kabisa. Tuendelee kupaza sauti. Hili jambo tayari lipo kwenye sera ya elimu, kimebaki utekelezaji.
Tunahitaji kuwapa push viongozi walifanyie kazi.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,956
2,000
Najiona mwenye hatia nisipopongeza maoni yako! Asante! Ni Kiswahili kitakachowakomboa Watanzania na sio lugha ya kigeni. Tunaweza kujifunza lugha hizo lakini Kiswahili kikawa lugha kuu ya kufundishia kama tunavyokitumia kwenye mawasiliano.
Hili wengi hatulisemei mara nyingi kwa umuhimu wake; katika taasisi zilizofanikiwa sana katika taifa hili ni hili Baraza la Kiswahili Tanzania.

Hawa ndio wanaostahili kupewa tuzo, toka mwanzo walipopewa jukumu la kusimamia kazi ya kuiendeleza lugha hiyo. Matokeo yake yanaonekana wazi na kila mtu.

Napendekeza, kwa wenye historia kamili na watendaji wa taasisi hiyo tokea ianzishwe ipandishwe hapa JF watu waweze kujua juhudi zao walizofanya hadi kukifikisha kiswahili hapa kilipofikia.

Mkuu 'Mikono yenye Sugu', unaoufahamu mzuri wa historia ya taasisi hiyo ili utujuze hapa?

Ni jambo jema sana kupongeza mahali panapostahiri pongezi. Kwa hakika hawa wanastahili pongezi.

Na kama kuna taasisi au shirika jingine lolote tunaloweza kuwapongeza kwa juhudi zao zenye matokeo yanayoonekana, na wao pia itafaa tuwe na taratibu za kuwapongeza.
Tusiwe watu wa kushutumu tu na kulaumu kila mara.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom