Ukiangalia kwa undani ziara ya Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton nchini Malawi na maneno 'Mwanza' na 'Tanzania' kwenye nguo ya Rais wa Malawi Bi. Joyce Banda vinaweza kuwa na ujumbe mzito kwetu hasa katika kipindi hiki ambacho tuko kwenye mgogoro wa mipaka kati ya nchi yetu ya Tanzania na nchi ya jirani ya Malawi, ni ngumu kutabiri ni kitu gani au ujumbe gani uliojificha nyuma ya pazia lakini kwa wachunguzi wa mambo ya kisiasa, kivita na kiuchumi na hasa kwa upande wetu wa Tanzania ni nafasi ya kuweza kutafakari kwa kina na kufahamu yaliyojificha nyuma ya pazia na ni zipi hatua za kuchukua kwa sababu zinazoweza kupatikana, inaonekana Malawi hawakukurupuka na wanafahamu ni kitu gani wanakifanya, inawezekana pia wanafahamu uwezo wetu kwa sasa na namna ya kuukabili, inawezekana pia sisi kwa miaka mingi hatukumdhania Malawi au nchi yoyote ya kusini mwa Afrika kama 'potential' adui wakati wao siku zote tangu kuisha kwa mgogoro wa kwanza wamekuwa wakituchunguza na kujipanga, kama Intelijensia yetu ilikuwa makini miaka yote hiyo basi ni jambo la kushukuru (ingawa kwa namna moja au nyingine nina shaka nayo kwani ilihamia kuwa Intelijensia ya CCM katika kupambana na vyama vya upinzani badala ya kusimamia kwa dhati na kwa kweli kabisa Usalama wa Taifa letu) na walitakiwa walione suala hili miaka mingi iliyopita kuwa linakuja, tukae chini tuumize kichwa tufahamu ni ujumbe gani tumetumiwa na Bi. Hillary Clinton na Bi. Joyce Banda (pamoja na mlinzi wake mwenye-combat), NACHELEA KUFIKIRIA KWAMBA SIO UJUMBE MZURI.