Unaweza kuangalia tatizo hili kupitia kwenye mfumo wa uundwaji wa Halmashauri zetu na uwajibikaji wake....so kazi ya mbunge/diwani ni kuwabana,na kama amefanya hivyo na bado hamna kilichofanyika nani alaumiwe ? Hapo ndo tunapishana mtazamo na zembwela yeye anatupa lawama kwa mbunge/diwani wakati si kazi yake. Tukienda mbali zaidi hiki ndo chanzo cha rushwa,mfuko wa jimbo na serikali kutojali kauli za wabunge maana inajua haitawajibishwa kwa makosa yake bali mbunge ndo atawajibishwa kwa kosa ambalo kimsingi ni la serikali...
Nimefuatilia kwa muda mtazamo wa huyu mwanahabari zembwela na nimegundua kunamambo hafikirii sawa. Kwa mtazamo wake ni kwamba mbunge na diwani ndo mwenye dhamana ya maendeleo ya jimbo. Sitaki kuhoji kiwango chake cha elimu,lakini kwa mtu mwenye ufahamu unajua nani anawajibika kuleta maendeleo na nani anapaswa kupeleka vipaumbele vya wananchi husika. Bwana mdogo zembwela nadhani unapaswa kuwaunganisha vijana kuishinikiza serikali kutimiza yale mliyowatuma wabunge wenu wakayapeleke serikalini kwa kutengewa bajeti na utekelezaji. Lakini ukiendelea kuwaaminisha watu uzembe wa serikali ni wa mbunge unakosea. Sote tunawajua wabunge wawajibikaji na wazembe na lazima tuwawajibishe,lakini hujuma za serikali kwa baadhi ya wabunge kuwafanya hawawajibiki ndo kumezaa mfuko wa jimbo. Sasa wabunge wakiwa watendaji nani ataisimamia serikali ? Mwisho nilistuka na kuogopa zembwela alipowahamasisha wananchi kumng'oa diwani bila uchaguzi eti hawawezi kusubiri uchaguzi wakati anachelewesha maendeleo. Nahisi sheria ya uchaguzi haijui. Amekomaa na azimio la arusha bila kujua kuna azimio la zanzibar wameleta ccm.
Unaweza kuangalia tatizo hili kupitia kwenye mfumo wa uundwaji wa Halmashauri zetu na uwajibikaji wake.
Shughuli za Halmashauri zinafanywa kupitia vikao vyake. Kwa mfano mkutano mkuu wa Halmashauri, katibu wake huwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri. Vikao vya kawaida vya Halmashauri hizo katibu wake huwa ni Mkuu wa Idara. Mkurugenzi wa Halmashauri ni cheo cha kuteuliwa na Rais... Aidha kwa wakuu wa idara nao wanateuliwa toka serikalini. Hapa ndio walakin unapoanzia.
Hivyo basi labda tuanzie hapa na kuona je kuna wakurugenzi wenye kudharau maelekezo ya madiwani wao kwa sababu tu ni wateuliwa wa Rais, na kwa namna moja ama nyingine hawawajibiki moja kwa moja kwa Madiwani?
Je kimefanyika nini ili kuona kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri anachaguliwa na Madiwani, ili aweze kuwajibika moja kwa moja kwa Madiwani hao na sio venginevyo?
Mkuu umewapa somo zuri! Zembwela is right!
Zembwera jembe huwezi mlinganisha na wale wa Clausi fm
...maazimio yote ni kwaajili ya tanzania,majina yalikuja kwa kuzingatia mkutano wa hilo azimio ulifanyika wapi....
Acha kupanic huo Mfano nimeutoa kuoonesha kuwa Zembwela yuko sawa na Kazi ya mbunge ni kuhishinikiza serikali kuahakikisha maendeleo yana patikana na hakishindwa yeye ndiye wa kwanza kupewa lawama!
Mnyika Swala la maji limemshinda na bahati mbaya hawezi kurudi bungeni Tena!
Tatizo Bawacha mnachojua ni matusi tuu! Jimbo linapokosa maendeleo wa kwanza kuulizwa ni Mbunge!
...so kwa mtazamo wako mnyika ndo anapaswa kujenga miundombinu ya maji toka ruvu mpaka ubungo,em tusaidie kuondoa uvivu...
Jukumu la Mnyika ni kuimiza serikali kuwaletea wana ubungo maji na alikubali kubeba jukumu hilo na kama hawezi sisi tutampa mtu mwingine 2015 .
...kiongozi na kama amehimiza na akathibitisha kufanya hilo,lakini serikali haijaleta hapo inakuwaje,atabeba msalaba kwa niaba ya serikali au inabidi waziri awajibike....?
Wewe ni wakuonea huruma yani mtu kasema ukweli mnatokwa na povu!
kumuita zembwela mwanahabari ni kushushia hadhi tasnia ya habari.
lakini unajua ya kwamba tokea mwanzo zanzibar ilikuwa bado nichi ndani ya nchi? Tokea zanzibar walipofanya mapinduzi walianza kuwa na rais wao na jeshi,bunge n.k
embu nitabanaishe kidogo, azimio la arusha lilifanya kitu gani zanzibar au azimio la zanzibar lilifanya jambo gani huku tanganyika
samahani hivi mwandishi wa habari ni nani? Je wajua kuwa mwanavichekezo anaweza kutumia taaluma yake ya vichekesho kuelimisha jamii na kukosoa serikali?