Zanzibar 2020 ZEC yawaengua wagombea wengi wa ACT-Wazalendo. Je ACT-Wazalendo itashiriki Uchaguzi?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Naam kumekucha tume ya zanzibar ya uchaguzi imetangaza haya yafuatayo:-

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imewaengua wagombea kumi na watano (15) kati ya hao kumi na mmoja (11) ni wa Chama Cha ACT-Wazalendo, CCM mmoja (1), CUF mmoja (1), UPDP mmoja (1) na Demokrasia Makini mmoja (1), waliokuwa wakigombea nafasi za Uwakilishi Zanzibar.

Sababu za kuondolewa ni kushindwa kufuata kanuni za uchaguzi katika kujaza fomu za uteuzi.

ACT-Wazalendo ni:-
1. Haji Ali Haji (Tumbatu).
2. Hassan Jani Masoud (Nungwi).
3. Haji Mwadini Makame (Kijini).
4. Juma Duni Haji (Mtoni).
5. Hasne Abdallah Abeid (Bububu).
6. Hamad Masoud Hamad (Ole).
7. Omar Ali Shehe (Chake Chake).
8. Khamis Rashid Khamis (Chonga).
9. Issa Said Juma (Micheweni/Konde).
10. Mmanga Mohammed Hemed (Konde/Tumbe).
11. Is-haka Ismail Shariff (Wete).
CUF ni:-
1. Juma Ali Juma (Ole).
Demokrasia Makini ni:-
1. Abbas Omar Abbas (Ole).
UPDP ni:-
1. Yussuf Said Hamad (Chake Chake).
CCM ni :-
1. Othman Ali Khamis (Mtambwe).
chanzo ni mwndishi Ally Mohammed kutoka zanzibar
 
Huyo 1 ni kafara. Tena kwenye majimbo yale ambayo huwa wanashindwa. Yale ya Pemba.

Wapinzani wakianzishe. Liwalo na liwe... After all, baada ya 28 Okt 2020, NEC na ZEC zitawatangaza CCM washindi, washinde, wasishinde!
Mkuu Mnapokuwa nyuma ya keyboard akili zenu huwa mnamkabidhi nani?

Unaposema wakianzishe ni kwa faida ya nani? Je unakuwa umewaza juu ya watoto wetu,akina mama na wazee wasiokuwa na pakukimbilia?

Ogopa sana kugombea mabaya.kuwa makini,hubiri amani na upendo
 
Kwa hiyo unataka wakifanyiwa ubaya waseme tu "hewala mzee", mpaka mwisho wa dunia. Kama wewe utaishi milele, kaa pembeni kimya. Watu makini wanahubiri haki.
Mkuu Mnapokuwa nyuma ya keyboard akili zenu huwa mnamkabidhi nani?

Unaposema wakianzishe ni kwa faida ya nani? Je unakuwa umewaza juu ya watoto wetu,akina mama na wazee wasiokuwa na pakukimbilia?

Ogopa sana kugombea mabaya.kuwa makini,hubiri amani na upendo
 
Mkuu Mnapokuwa nyuma ya keyboard akili zenu huwa mnamkabidhi nani?

Unaposema wakianzishe ni kwa faida ya nani? Je unakuwa umewaza juu ya watoto wetu,akina mama na wazee wasiokuwa na pakukimbilia?

Ogopa sana kugombea mabaya.kuwa makini,hubiri amani na upendo
Wewe umewaza juu ya watoto wao walioenguliwa.
 
Mkuu Mnapokuwa nyuma ya keyboard akili zenu huwa mnamkabidhi nani?

Unaposema wakianzishe ni kwa faida ya nani? Je unakuwa umewaza juu ya watoto wetu,akina mama na wazee wasiokuwa na pakukimbilia?

Ogopa sana kugombea mabaya.kuwa makini,hubiri amani na upendo
We ni mpuuzi pasipo na haki we unategemea nini, watakoleta vurugu ni hao waubirio amani bila haki.
 
Yaani Kama hivyo wabaki wenyewe , ona madudu mengine ya ZEC haya hapa
IMG_20200918_024635.jpg
 
Back
Top Bottom