ZEC: Makosa kwenye Daftari la wapiga kura yamechangiwa na wapiga kura wenyewe

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imesema kukosewa kwa majina, picha au jinsia kwa baadhi ya wapigakura kwenye daftari la wapigakura kumechangiwa na wapigakura wenyewe kushindwa kufanya uhakiki wa taarifa zao wakati kazi hiyo ilipofanyika.

Mkurugenzi Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), Thabit Idarous Faina amesema hayo leo Oktoba 22, wakati akitoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari ofisini kwake Maisara mjini Unguja.

Amesema kabla ya Zec kuweka wazi daftari hilo ilifanya uhakiki wa wapigakura na wengine kusajiliwa upya, ila kuna baadhi ya wananchi walishindwa kujitokeza kufanyiwa uhakiki huo.

Amesema licha ya kosa hilo kuwa la kibinadamu lakini pia limechangiwa na wapigakura wenyewe ambao baadhi yao walifanyiwa uhakiki na kuwekwa sawa majina yao.

Amesema kutokana na hali hiyo Tume itatoa msimamo wa hatua za msingi juu ya watu hao waliokosewa majina yao, jinsia au wengine kubadilishwa kwa picha za wanaume kuwekwa taarifa za mwanamke au kinyume ya hapo baadaye baada ya kikao cha uongozi.
 
Hilo suala ni kwel ndio maaana kunakuaga na uhakiki.sisi tuliofanya data entry kipind kile cha kusajil line unakuta jina linakosewa
Typing error
 
Back
Top Bottom