Zawadi nono kwa atakae fumbua tatizo hili

SOKO LA MAGARI

Senior Member
Oct 26, 2014
115
66
ZAWADI NONO KWA ATAKAE FUMBUA TATIZO HILI.

MADEREVA TAPELI(baadhi) VS WAMILIKI MAGARI UBER

Wakuu wanasheria naomba msaada wa ufumbuzi wa hii changamoto hasa biashara ya UBER.(magari zaidi ya 15)

Nikiwa kama mmiliki naingia mkataba wa maandishi na dereva, awe na (i)wadhamini wawili,(ii) barua serikali za mtaa, (iii)copy leseni, vyeti, picha n.k

Unakabidhi gari kazi inaanza, labda mwezi hivi unagundua yafuatayo:

1) Akipigwa traffic notification ya kosa lake hatoi taarifa na HALIPI ukimuuliza ana aahidi kulipa.

2) Malipo ya gari yana sua sua kwa visingizio vingi, kuuguliwa, kazi sio n.k analimbikiga madeni.

3) Uki kagua matunzo ya gari mabovu sn km anazotembea nyingi sana kuliko kawaida.

Muda sio mrefu aidha anasingizia ugonjwa au kufiwa humuoni tena, au ukigutuka anatoa ahadi humuoni tena.

Unapoanza follow up kwa wadhamini wake unagundua nao ni madereva wenzio matapeli ni mchezo wao wote kudhaminiana na kuendelea kutapeli watu.

Unaweza kuta anakuachia deni la notification hadi 500,000= na wewe unamdai 1.5 mln total 2mln.

Ukimwambia aandike kukiri anadaiwa wengi wanakubari na kuandika na kutoa ahadi za uongo.

Ukienda Traffic wakusaidie angalau alipe notification wanadai mwajiri anapawa ku control driver wake, na hiyo ni civil case hawawezi mkamata kwa hilo tu watakamata gari lako.

Haya process za civil case ya Tsh 2 mln nadhani ntakuwa mnaijua gharama plus muda disturbance n.k

Naomba kuwasilisha NAAHIDI ZAWADI NONO KWA ATAKAYE PATA UFUMBUZI

Aidha ni mawazo yang tu, Hawa wadaiwa kwa kupia sharia tunaweza watangaza kwenye vyombo vya habari ? mitandao ya kijamii ? n.k pengine wanaweza lipa
 
Pole mkuu, ndio vijana na watanzania hao ukiwakuta vijiweni wapo kulaumu tu ukiwapa ajira ndio hivyo
 
Back
Top Bottom