Zawadi kwa maharusi

hizi zawadi hizi
kuna mdada alipewa zawadi ikiwa imefungwa kwenye box zuri kabisa
alivoenda kufungua akakuta pedi zilizotumika..na yai
Mwili unanisisimka hapa
 
Kwenye graduu ya form 4 miaka hiyo kuna dada alipewa zawadi ikiwa kwenye gift paper basi kaenda nayo home, kufungua akakuta mawe yamejaa. Alafu akawa anawajua waliotoa zawadi hiyo sema ni watu ambao ni makuzi sana shuleni
 
zawadi za harusi zina mambo sana kikubwa ni kuhakikisha unaziombea kabla ya kufunguliwa na usipende sana kuzitumia ikiwezekana na wewe gawa
 
Kweli mkuu... Kuna sendoff moja ilifanyika majuzi basi wakawaambia wageni waalikwa kuwa zawadi ni pesa tu. ....

Wanawake ndo wanayo hayo mambo sana...kuna harusi dada mmoja alikuta amefungiwa kinyesi kwenye box...uzuri mkanda wa video uliwaumbua maana walionekana wanamkabidhi shostiwao hilo box kwa mbwembwe zote.
 
Actually mimi naona ni vizuri wanafungua zawadi papo hapo…desturi za watu wa magharibi,wanafungua zawadi papo hapo unapompatia,mbele yako na hii inasaidia kwa mtoa zawadi kuona reaction ya hao waliopewa kama wataipenda au lah na pia kama ni kitu cha kumdhuru atajua pia papo hapo kama wewe unahusika….
 
Kweli mkuu... Kuna sendoff moja ilifanyika majuzi basi wakawaambia wageni waalikwa kuwa zawadi ni pesa tu. ....

Wengi wanafanya hivyo hasa Kama maharusi hawaishi hapa nchini and it makes sense!! Mzima lakini wewe mwanangu??
 
Bora sisi Wachagga zawadi zetu unapewa full mjengo na mzazi/wazazi...siku ya harusi unakabidhiwa hati ya nyumba kwa mbwembwe nyingi...

Ninyi mnaosubiria zile za kwenye maboksi subirini kutiliwa unga wa kimeta huko...

Umeshasema wazazi. Vp kuhusu marafiki,wafanyakazi wenzio na wale wa upande wa mume? Au wote watakuwa wachaga so watakukabidhi funguo za magari na nyumba?
 
mimi nilishuhudia harusi ya ndugu yangu alipewa zawadi ya chupa ya chai lakini ndani ya chupa ya chai kulikuwa na hirizi kubwa sana hata haijulikani iliwekwaje na kuitoa ile hirizi tulivunja ile chupa ndio tukaitoa na kuichoma moto ktk jina la YESU
 
Duuh.. swala la zawadi ni kumuomba Mungu saaanaa. .. kuna dada alinishuhudia alipewa box zuri lililofungwa kwa gift paper siku analifungua anakuta panya aliyekufa baada ya hapo kila akibeba mimba mtoto hufia tumboni..

kila mtu na imani yake ila kwa waaminio KUZIPONYA na KUZITAKASA kabla ya kuzitumia wafanye hivyo,
 

Dah... So sad aisee... Ni Mungu tu ndiye aweza kutukinga na haya madhila!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…