Habari za mchana wa leo wanajamvi.....
Katika utamaduni wetu Watanzania tumezoea kupeleka zawadi mbalimbali kwa maharusi, zawadi hizo zinaweza kuwa ni pesa au vitu vya thamani. Ila kuna uvumi umeenea kuwa kuna watu ambao huwa wana nia mbaya na maharusi na kuishia kuweka vitu vya ajabu katika mabox mazuri kisha kuyafunga na gift papers safi na kuwapatia maharusi.
Mara baada ya maharusi hao kufungua zawadi na kukuta vitu vya ajabu wamekuwa wakidhurika na vitu hivyo, nafikiri wengi wetu tumewahi kushuhudia ama kusikia jambo hili. Na hii imesababisha maharusi wengine kutaka zawadi zote zifunguliwe toka katika gift papers na ZIWEKWE WAZI ili kuepuka madhila haya!
Nimewahi kushuhudia wanandoa flani wakifungua zawadi katika bahasha, cha ajabu waliambulia Sh. 20. Ile ya rangi ya Silver, sijui kama bado zipo au lah. Walijiuliza sana kuwa mtoa zawadi hiyo alikuwa na lengo gani???? Ila Mungu ni mwema hawakudhurika iwapo mtoaji alikuwa na lengo baya.
Kwa imani zetu tofatui tofauti hebu tujadili ni jinsi gani ya kuepuka mambo kama haya yasitokee katika jamii zetu, Inaweza kuwa ni wewe, ndugu yako ama rafiki yako anaweza kukutana na hii changamoto una ushauri gani kwake........ KWa wale waliokumbana na haya madhila walichukua hatua gani??? Tupe Uzoefu wako..........
KARIBUNI KWA MJADALA