zanzibar.....

Nilicheka siku mmoja kusikia Mzungu akisema "I am building hotel resort in MNEMBE..."
 
Ule Mfenesi wenye mazizi makubwa haupo umekatwa...saivi pamepandwa mwengine palepale ulipokuwa ule wa awali na unastawi vizuri tu...umenikumbusha enzi zangu pale madrasa za Maalim Imam RIP na Maalim Bi.Afua zote zikipakana na Msikiti wa Simba mpaka leo zipo ila msikiti ulibomolewa na kujengwa upya...kuna Mzee(khamis kibatari,RIP) aliyekuwa mwazini mwenye sauti kali akiadhini bila ya bomba sauti yake unaisikia mpaka Mwembeladu na Mbuyutaifa...hata waadhini wa misikiti ya Salum Makka na Kwabiziredi wakimsubiri Kibatari amalize ndo waanze wao...saivi wapi?
vijana wapo na bongo flava upuuuzi mtupu...mjini.


junius umenikumbusha watu ambao walikwisha nitoka akili maalim Imam wakati mmoja tupo wadogo alikuwa akifundisha netiboli ,Maalim bi afuwa atakuwa mtu mzima sana kama bado sasa yupo hai lakini juu ya yote hayo umemsahau Maalim wetu Bi Mariam bin Hussen mwalimu wa wengi aliyetusomesha Gulioni na mitaa ya karibu wanafunzi wake wengi wao leo ni watu muhimu katika ulimwengu wa kwanza , kwani kulikuwa na vyuo viwili vikubwa cha Bi Mariam na Bi Zena na kufatiwa maalim imam na wengineo leo wapi siku zile kila mzee ni mzee wako udugu mshikamano imani zetu zilikuwa moja leo wapi?karaha tupu( ARDHI HAINYONYI MAZIMA )hubakia juu na kuwa mithili ya Gome.
 
Back
Top Bottom