Zanzibar yarejea kwa Bamkwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar yarejea kwa Bamkwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by salmar, Oct 31, 2012.

 1. s

  salmar JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 782
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  By Salma Said,

  Kovu za majeraha yaliyowapata na adhari za bakora zilizoachwa katika miili ya Wazanzibari bado zipo bada ya miaka arobaini na nane ya mapinduzi. Kovu za majaraha hayo yaliyoachwa na Field Marshal Okello na kundi lake kwa upande mmoja na athari za bakora za akina Rashid Abdulla Mamba kwa upande mwengine bado zinatukumbusha wapi tumetoka. Ilikuwa ni zama za ujahilia nguvu na amri zilitawala na sharia pamoja na utawala wake vikapewa kisogo.

  Kipindi hiki ni kipindi kilichoacha kiza katika historia ya Zanzibar. Kuna wale ambao wamepotea ndani ya mikono ya serikali na mpaka leo hii serikali imeshindwa kutoa kauli kuhusu wapi wapo watu hao, akina Abdu Nadhif, Abdulla Kassim Hanga, Othman Shariff, Jaha Ubwa na wengineo wengi.

  Wazanzibari hawa hawakuwahi kuhukumiwa kifo na Mahkama wala hata hawakuwahi kufikishwa Mahkamani na kuambiwa kosa ambalo washitakiwa nalo. Kimya hiki cha kutojua khatima ya watu hawa na wengi wengine kina ashiria kwamba watu hawa wameuwawa nje ya mahkama (Extra judicial killings), kwani kama watu hawa wako hai basi miaka arobaini na nane sasa hawajaletwa mbele ya Mahkama kufunguliwa kesi au angalau kujulikana wapi wapo na kama wapo basi waarifiwe watu wao kuwa wako hai.

  Watu wanasema tusikumbushe kilio matangani, lakini kama hujakumbusha kilio matangani utakikumbushia wapi?. Sio kila anaelia matangani anamlilia marehemu au maiti anaesubiri kuzikwa au aliezikwa basi wapo wengi wanaokumbuka ndugu na jamaa zao ambao walishatangulia na msiba huo au tanga hilo huwa linawakumbusha msiba wao pia.

  Jengine waswahili tuna msemo wetu wa Kiswahili kama ilivyo katika lugha zote , tunasema “ilopita si ndwele tugange ijayoâ€, ndio hili tunataka kulizungumza. Matokeo ya utekaji nyara watu na kufichwa kwa kutuhumiwa kuwa wamekiuka sharia. Mambo haya ya utekwaji nyara watu na watu wa usalama yalikithiri na kushamiri katika Awamu ya Kwanza ya Rais Karume na kuendelea hata katika Awamu ya Pili ya rais Aboud Jumbe, ambapo Jumbe aliweza kidogo kidogo kukomesha hilo.

  Tunakumbuka vyema utekaji nyara uliokuwa ukifanywa na usalama na kuwafanya Wazanzibari kutokuwa na raha wala buraha na kuwatia khofu watu katika majumba yao hata kufikia hadi kusema chumvi imeadimika unaogopa kusema kwa kuhofia na wewe kutiwa ndani, Kwani wapo waliotiwa ndani kwa kusema bidhaa fulani imeadimika.

  Hiyo nyara inayotekwa mtu haiishi kituo cha polisi bali moja kwa moja “kwa Bamkwe†na huku ndio utakiona kilichomtoa kanga manyoya. Mateso ya kwa Bamkwe hayasimuliki kwani baada ya mateso huwa kuna kiapo kwa kutakiwa kuwa hayo mambo na mateso ya kwa Bamkwe usiyasimulie uyawache hapo hapo. Lakini binaadamu hawezi kujizuiya na hasira na kila akijitizama bakora za Bamkwe zilizoota mgongoni kama alama za punda milia anakumbuka mateso ya Bamkwe. Mwisho humtoka yale ya kule kwa Bamkwe.

  Naam ilifika hata watu kususia gari ya Taxi ya mmoja kati ya hao walokuwa wakitesa wtu. Wapo wengi hao Bamkwe wengine wamefikia kuwa na nafasi kubwa serikalini na wanajulikana.

  Leo hii tunazungumzia kutekwa nyara kwa Sheikh Farid Hadi Ahmed. Kesho atatekwa mtu mwengine au kiongozi mwengine, hili si la kulinyamazia. Dola inayofuata utawala wa Sheria na kuzingatia huru binafsi na haki za kibinaadamu haiwezi kukaa kinya na kuacha hali hii ikaendelea. Leo Sheikh Farid kesho mwengine, hawa wanaoteka nyara watazoea ni lazima wawajibishwe kama kweli tunataka kweli kusimamisha Utawala wa Sheria na kulinda Haki za Binaadamu. La vyenginevyo tutakuwa tukiimba wimbo wa Komandoo Salmin Bin Amour , SHERIA, SHERIA , SHERIA. Vyenginevye itakuwa ni jina tu la mzee sharia uzia.

  Komandoo, Salmin alijilabu sana na wimbo wake wa SHERIA ,SHERIA, SHERIA, lakini kwa kweli ni katika kipindi chake utawala wa sharia na kulindwa haki za binadamu havikuwepo.

  Tutamkumbuka Salmini na maskani zake ambazo alikuwa akizifadhili. Huku zikitukana na kuvunjia heshima watu pamoja na kujingiza katika vitendo vya uvunjivu wa haki za binaadamu, si hao tu bali hata wale vijana wa “JANJAWID†ambao walikuwa wanatumiliwa kuingia majumbani na wengine kupelekwa Pemba kuwaadhibu watu na kuwaibia. Tutamkumbuka pia Komando kwa kupandikiza mbegu ya fitna na chuki ya Upemba na Uunguja na mengi mengineyo.

  Wazanzibari tusikubali kurejeshwa tena nyuma kule kwa “BAMKWE’ na kina FUMU pamoja na JANJAWID, tusiruhusu uhalifu huu unaotaka kurudi tena. Tudumishe ustaarabu wetu pamoja na ustaarabu wa kuimarisha UTAWALA WA SHERIA na Kusimamia HAKI za Binaadamu.

  Utaratibu wa kufunguliwa kesi upo sasa ya nini haya ya kutekwa nyara. Kama mtu anashukiwa kuvunja sharia za nchi basi utaratibu wa sharia utumike katika kumshughulikia na sio kufanya vitendo vya uharamia vya utekaji nyara watu. Hili lisipite ,lilaaniwe kwa nguvu zote na serikali lazima lifanye uchunguzi.

  Baraza la Wawakilishi lazima liitake serikali kufanya uchuguzi. Tusikubali kurejeshwa tena kwa BAMKWE. Utekaji nyara umefanyika Mrima haukuchunguzwa hiyo umepita bila kulaaniwa sasa umevuka bahari nakuja tena visiwani, Wazanzibari tulikuwa tumeshasahau watu kusombwa usiku na kutiwa ndani ya vigari vya usalama kwa kupelekwa kwa BAMKWE sasa haya yanarudi tena.

  Tukiyanyamazia na kusema aah ni huyo Sheikh Farid wa Uamsho basi tutakuwa tumekosea kwani huu ni mwanzo leo Farid kesho mwengine Vuai Ali Vuai wa CCM au Ismail Jussa Ladhu wa CUF. Vitendo viovu haifai kupewa fursa kukujichomoza na kumea katika jamii hasa vile tunaamini na kukubali Utawala Bora pamoja na kulinda Haki za Binaadamu. Maandiko ya Kusimamia Utawala Bora na Hifadhi ya Haki za Binaadamu Katika Katiba yatakuwa hayana maana ikiwa yatabaki katika kurasa za Katiba bila ya kusimamiwa na kutekelezwa.
   
 2. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Zanzibar colony land of Tanganyika!!!Killings of zanzibaris will go on till uamsho and others watakapo salimu amri!Zanzibar ni wahalifu kama wahalifu wengine na hii inaatokana na dini yao bandia ya kiislamu...So msitegemee mafanikio,amani maendeleo wala utulivu kupitia uislamu maana haijawahi kutokea hapa duniani binadamu akapata amani kupitia uislamu ila ataambulia maumivu,kudhalilika,kuteketea na mwisho kupumzika jehanam kwa A.l.l.a.h kazi kwenu kina yakheeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji kashaandika sana hapa JF. Tatizo la Wazanzibar ni Wazanzibar wenyewe.

  Wakitaka kuvunja Muungano, basi wataweza kwa muda mfupi sana.

  Ila hata huyo mwenye domo la maneno machafu AKA Jussa, ni NATO kupindukia (No Action Talking Only).

  Huyu na matusi yake, Bunge likianza anakimbilia DODOMA kuchukua Posho. Si agome basi tumuone?

  Baniani mbaya ila kiatu chake kizuri. Tumewachoka bana.

  Nendeni salama. Waondooeni viongozi wenu wote Bungeni na Serikalini, mchezo umekwisha.

  Wanaume wa Makamo kufanya mambo kama Kibinti kigori, si vizuri sana na mnawaaibisha hata Wanenu.

  Chukueni uamuzi DUME na Susieni Bunge na Serikali ya Muungano na Taasisi zake zote - MTAKUWA HURU.
   
 4. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Uislam kama ulivo ni IMANI ya AMANI tatizo baadhi ya viongozi wao wanaitumia IMANI hiyo kwa MASLAHI yao tu ya hapa DUNIANI (TUMBONI).
   
 5. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakuelewa ndg mkuu Jacobus lakini mimi sijawahi matendo ya Amani hasa uislamu huo unapokua na waumini wengi ndivyo fujo za wao kwa wao huzuka na mauaji dhidi ya Imani nyingine huanza so nimeshindwa kudhibitisha hili kwamba eti hawa jamaa ni wa Amani...Huwa nasikia maneno watu wakisema lakini kwangu mimi waislamu nawaona ni Socialy Unfits groups
   
 6. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  laana ya upanga itawatafuna milele!
   
 7. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Gwakisa, kitabu chao kitakatifu cha Kuruani kinaelekeza Binaadam aishi kwa AMANI hapa duniani, tatizo ni VIONGOZI wao tu wakorofi kwa KUKOPI tofauti ya Upalestina na Uyahudi na KUPASTI kwa wafuasi wao ambao wengi hawana ILIMU ya Uislam. Wachache wenye ILIMU ya Uislam wanaelewa hili.
   
 8. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  kila kukicha zanzibar zanzibar zanzibar kitu gani? si mkoa tu? na ikiwa taifa ndio samaki zitongezeka bahrini? au zitashuka bei? tatizo mnapenda sana kupakatwa na kulishwa UROJO na waarabu....! hata hamstuki wenyewe nao hali ngumu fujo kila kukicha..ndo mnadhani wataendelea kuwaletea tende.......someni alama za nyakati.....
   
 9. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Zanzibar!... I'm sick and tired of it, let them go...
   
 10. J

  John W. Mlacha Verified User

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  wazanzibar kila kitu kipo mikononi mwenu..watanganyika wala hawahusiki...
  vurugu za visiwani ni muslims againts muslims...but najua makanisa mnayachoma huku wenyewe hamjui kwa nini mnayachoma
   
 11. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu. Wanahubiri kuwa dini ya Kiislamu ni ya Amani lakini mimi sijawahi kuona amani yoyote. Kila kukicha ni vurugu tupu. Mimi nadhani hiyo ni dini ya fujo na mauaji.
   
 12. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu ni kweli hujakosea. utulivu upo kwenye ukristo tu, kwani hata kama wewe ni mwanaume halafu mwanaume mwenzie akaja kukuchumbia akuoe maaskofu, mapadre na wachungaji watawafungisha ndoa tu. na huo ndo utulivu wa ukweli kwa mujibu wako lakini. to hell.
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,292
  Likes Received: 22,067
  Trophy Points: 280
  UAMSHO wana harufu ya ugaidi
   
 14. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  akili ni nywele kila mtu ana zake....dini ni imani kila mtu anayo ya kwake...
   
 15. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kinaitwa Amani hiyo ni janja ya nyani tu!
   
 16. Fatal5

  Fatal5 Senior Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  TANZANIA SERIKALI INAUA WAISLAMU - YouTube
   
 17. Fatal5

  Fatal5 Senior Member

  #17
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  TANZANIA SERIKALI INAUA WAISLAMU - YouTube
   
 18. Fatal5

  Fatal5 Senior Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
 19. Fatal5

  Fatal5 Senior Member

  #19
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  TANZANIA SERIKALI INAUA WAISLAMU - YouTube
   
 20. Fatal5

  Fatal5 Senior Member

  #20
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
Loading...