Mzee Mwanakijiji kashaandika sana hapa JF. Tatizo la Wazanzibar ni Wazanzibar wenyewe.
Wakitaka kuvunja Muungano, basi wataweza kwa muda mfupi sana.
Ila hata huyo mwenye domo la maneno machafu AKA Jussa, ni NATO kupindukia (No Action Talking Only).
Huyu na matusi yake, Bunge likianza anakimbilia DODOMA kuchukua Posho. Si agome basi tumuone?
Baniani mbaya ila kiatu chake kizuri. Tumewachoka bana.
Nendeni salama. Waondooeni viongozi wenu wote Bungeni na Serikalini, mchezo umekwisha.
Wanaume wa Makamo kufanya mambo kama Kibinti kigori, si vizuri sana na mnawaaibisha hata Wanenu.
Chukueni uamuzi DUME na Susieni Bunge na Serikali ya Muungano na Taasisi zake zote - MTAKUWA HURU.