Zanzibar yapiga marufuku kuuza (ku-export) mchele na sukari nje ya visiwa hivyo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa katazo la kusafirisha bidhaa za sukari na mchele nje ya Zanzibar kwenda nchi nyingine yoyote.

Taarifa hiyo rasmi ilitolewa na Ofisi ya Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda visiwani humo, Omar Said Shaaban, tarehe 30 Januari, 2023.

"Kwa kutekeleza mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 35(1) cha Sheria ya Biashara ya Zanzibar, namba 14 ya mwaka 2013, mimi OMAR SAID SHAABAN, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, naagiza katazo la kusafirisha Mchele na Sukari nje ya Zanzibar kwenda nchi yoyote, kuanzia tarehe 30 Januari, 2023," taarifa hiyo ilisema.

1675851841328.jpeg

Pia soma:
Zanzibar yaweka marufuku ya kuuza vyakula wakati wa Ramadhan
Bashe: Tumewalinda vya kutosha Wafanyabiashara wa Sukari, sasa wachague kuuza au kuacha, tunabadili Sheria

Marufuku nyingine Zanzibar Soma:

Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika
 
Heko serikali ya Mapinduzi kuhakikisha nchi ikinunua mchele na sukari kutoka nje ya nchi kwa fedha za kigeni hauuzwi tena kwa magendo nje ya Zanzibar.
 
Hapo wale wasafirishaji wa mchele kutoka Tanganyika wanaopeleka comoro itakuaje sasa.
 
Kule Tanganyika kijana wenu anasema waacheni wakulima wauze popote wanapoweza kuuza!.
Hao Viongozi Wenye Dhamana Ndiyo Wanaikwamisha Serikali Kwakuwa Hao Hao Ndiyo Wafanyabiashara Yaani Wanatupiga Mambo Mengi Wanazuia Yasifanikiwe. Tazama SGR Wanapiga Sound.
 
Yupo sahihi,hii inachochea hali ya kulima zaidi sababu ya uhakika wa soko.
Nzuri sana eeh?

Unauza mpaka akiba kisa hela tamu alafu mnunuzi anakuletea kwa bei mara mbili kuliko uliyomuuzia.


Maziwa ya brookside kama sijakosea yanazalishwa hapo Nairobi kutoka kiwanda cha familia ya Uhuru, lakini maziwa yanakusanywa kwa wingi kutokea Tanzania.

Baadaye tunakuja kuuziwa 1ltr karibu shs 8000 unaambiwa full cream, although mzee baba JPM alipiga stop huo usanii.

Wakati tuna viwanda hapa hapa homeland!.
 
Hahahaaa!! Kwa sababu hawalimi. Ila uku bara mkulima uza popote penye Faida kwako. Sisi tunalima
 
Back
Top Bottom