Zanzibar yagoma kulipa Sh40 bilioni Tanesco | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar yagoma kulipa Sh40 bilioni Tanesco

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by nngu007, Apr 6, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Waziri wa Ardhi, Maji, Makazi na Nishati wa Zanzibar , Ali Juma Shamuhuma

  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekataa kulipa deni la umeme la Sh 40 bilioni kwa TANESCO baada ya kupandishiwa kiwango.Waziri wa Ardhi, Maji, Makazi na Nishati wa Zanzibar , Ali Juma Shamuhuma alisema baada ya kiwango kuongezeka, serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatakiwa kulipa kwa asilimia 168 badala ya asilimia 21 kwa uniti.

  Shamhuna alikuwa akichangia katika majumuisho ya mjadala juu ya ripoti ya Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambapo Shamuhuna alisema, "hatukubali kulipa deni la Sh 40 bilioni kwa kiwango cha asilimia 168 asilani."

  Tanesco ilipandisha viwango vya malipo kwa wateja wake tangu mwaka jana kwa asilimia 21, kwa upande wa Tanzania bara ambapo kwa Zanzibar shirika hilo la umeme limepandishwa kwa asilimia 168 na kusababisha malalamiko makubwakutoka kwa wateja.Shamhuna alisema kuendelea kwa Tanesco kudai deni hilo kunakwenda kinyume na agizo la Rais Jakaya Kikwete kwamba pande zote mbili za Muungano zilipe viwango sawa vya asilimia 21.

  Waziri huyo ambaye alikuwa akichangia na kupigiwa makofi na wajumbe wengine alisema ili kuepukana na utegemezi wa umeme kutoka Tanesco ambao unaigharimu SMZ fedha nyingi, serikali umeanza kuchukua hatua za kuzungumza na wawekezaji wazoefu ili kuzalisha umeme kutokana na jua na gesi utakaojitegemea.

  Shamhuna aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba mradi kama huu umefanikiwa Dubai na Malaysia unaweza kuzalisha kati ya Megawati 50 na 100 ambao unatosheleza mahitaji ya sasa ya Zanzibar ya Megawati 50.  Hata hivyo, akizungumzia kuhusu madai ya baadhi ya Wajumbe wa baraza la Wawakilishi wanaotaka Zanzibar izalishe umeme kwa kutumia mawimbi ya bahari, Shamhuna alisema utafiti unaonyesha kuwa ni mradi mkubwa wenye gharama kubwa na pia haujafanikiwa katika nchi nyingi duniani.

  wakichangia mjadala huo wajumbe wengine wa baraza hilo wamesema suala hilo linahitaji kuangalia vyema na serikali ya muungano kwani haiwezekani serikali hiyo kukaa kimya na baadhi yao kutaka fedha hizo kutolipwa kwani haitowezekana
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Usishangae sana Mkuu, hawa Zenj siasa yao ya Nje/Muungano ni changu changu, chako chetu.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka wakati wa Nyerere walikuwa hawalipi hata kidogo
   
 4. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizo ndizo faida za muungano, mkijitenga kama mnavyolazimisha mtapata wapi jeuri ya kugoma kulipa?
   
 5. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  nyiye si mnasema mdebwedo!
   
 6. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nadhani kabla ya kuendelea kuwalaumu tungeangalia "uhalali na ukweli wa Zanzibar kutakiwa kulipa 168% wakati TBara ni 21%"
   
Loading...