Zanzibar waunda baraza la mitihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar waunda baraza la mitihani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Apr 5, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][/h]Posted on April 4, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
  Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Ramadhan Abdalla Shaaban,kuwa Waziri wa
  Ardhi.Makaazi,Maji na Nishati,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini
  Zanzibar jana,kabla Shaaban,alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
  Amali

  Wajumbe wa baraza la wawakilishi wamepitisha mswada wa sheria wa Kuunda baraza la Mitihani Zanzibar. awali Jina lililopendekezwa na waziri wa elimu wakati wakiwasilisha mswada ilikuwa ni Kuanzisha Bodi ya Vipimo na Tathmini ya Elimu Zanzibar. Waziri, pamoja na naibu wake Zahra Ali Hamad, pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Othman Masoud walijititajihidi kutetea jina la Bodi, lakini wajumbe wengi wa baraza khasa Backbenchers walifanikiwa kujenga hoja ya kuunda baraza la mithani Zanzibar ambalo majukumu yake hayatoingilia baraza la taifa la Mithani Tanzania (NECTA).
  Japokuwa Baadhi ya wajumbe akiwemo Mwakilishi wa Jimbo la Chonga (CUF) Abdallah Juma Aballah Chonga walipendekeza Zanzibar ianze kutunga mithani ya Form 4 na kuacha kutegemea NECTA, Majukumu ya ‘baraza la Mithani Zanzibar’ yatakuwa ni kusimamia mithani ya Zanzibar (Darasa la Saba, na Form 2) pamoja na kufuatilia maendeleo ya elimu Zanzibar. Wakichangia mswada huo Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu alisema wakati umefika kwa Zanzibar kuwa na chombo kinachojitegemea kitakachoshungulikia uratibu wa mitihani ya elimu ya juu hasa kwa kuzingatia umuhimu wa elimu nchini.
  Jussa alisema mswada huo ni mzuri licha ya kuwa na kasoro madogo madogo ambazo zinapaswa kurekebishwa na alisema chombo hicho ni muhimu sana kwa sababu ndiyo kitakachoratibu shunguli za mitihani ya kuanzia kidatu cha kwanza hadi cha kumi na mbili.
  Akizitaja kasoro hizo Jussa alisema kuna baadhi ya wadau ambao hawakushirikishwa katika mswaada huo na walipaswa kushirikishwa katika mchakato huo.
  “Suala hili sio la Muungano na imefika pahala Zanzibar ianzishe mambo yake wenyewe kwani msiba mkubwa tulipata wa kufelishwa wanafunzi kati ya 3303 waliofutiwa matokeo zaidi ya 1000 wanatokea Zanzibar lakini waziri ameshindwa kutoa kauli yoyote kuhusiana na suala hilo, Wananchi wanauliza jee serikali ipo makini katika hili? Alihoji Jussa.
  “Wananchi wa Zanzibar hivi sasa wanapoteza imani na wenzao wabara kutokana na mambo kama haya Mheshimiwa Spika.” alisema Jussa. Mwakilishi huyo aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba katiak suala la kuleta maelendeleo ya elimu nchini, serikali isione tabu kuzialika taasisi za elimu kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kusaidia kuinyanyua elimu ya Zanzibar. Na kusisitiza kwamba nchi yeyote yenye maendeleo basi wananchi wake wanakuwa na elimu.
  Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura (CCM) Hamza Hassan Juma naye alisema ili kufuta machozi ya wananchi wa Zanzibar ni kubadilisha jina la mswada huu na sio kuzungukazunguka katika kutoa majina ta tahmini na viwango bali ni kusema moja kwa moja baraza la mtihani Zanzibar “Mheshimiwa Spika dawa kubwa ni wazanzibari kuunda baraza letu la mitihani basi hakuna jengine. Maana hawa wenzetu wamezowea kutubeza nakumbuka tulipotaka kuanzisha vyuo vikuu hapa kila majina wakitwita lakini jee tuwaulize leo kuna vyuo vikuu hakuna? Alihoji Hamza.
  Alisema suala la kuundwa kwa baraza la mitihani Zanzibar haklina mjadala na wala halitaki kuzungukwa zungukwa kwani Zanzibar ina watalamu wake wa kila aina hivyo hakuna haja ya kuwa na kigugumizi katika hilo. Alisema katika suala hilo la elimu elimu ya form 4 Zanzibar kamwe haijakiuka katiba bali imetekeleza kwa vitendo azma yake ya kuinua kiwango cha elimu kwa wananchi wake, kwa kuwa rasilimali ya nchi yeyote ni elimu basi ni kurekebisha mitaala na sera za elimu.
  kufuatia malalamiko ya hivi karibuni ya wanafunzi kufutiwa mitihani, baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi walipendekeza zanzibar ijitegemee katika kutunga mithani yake na kuachana na NECTA, lakini waziri na mwanasheria mkuu wakajibu kuwa Zanzibar kujitoa ktk NECTA ni kinyume cha sheria, halafu haiwezi kuwa ni suluhisho la matatizo ya mithani.
  “Kwa kweli wanafunzi wetu wamefanya udanganyifu mkubwa. kamati ya baraza la wawakilshi ilikwenda Dar es saallam katika ofisi za NECTA na kuthibitisha hilo, na kamati ya wazee ambao watoto wao wamekumbwa na mkasa wa kufutiwa mithani pia wamethibitisha. hata kama tukiamuwa kutunga mithani wenyewe, tusiruhusu udanganyifu,” Shaabani alisema.
  Alisema upo ushahidi wa kutoka kwamba watoto walifanya udanganyifu na kwamba ni lazima wazazi pamoja na waalimu waungane kupiga vita udanganyifu ili kupata wanafunzi wankaoweza kuwa wataalamu siku za baadae. Waziri alisema, katika hesabu za jumla, kati ya wanafunzi 3303 waliyofutiwa matokeo ya mithani, 2076 ni kutoka shule za zanzibar. “watoto wamefanya kosa, lakini adhabu ya miaka mitatu bila kufanya mithani ni mingi. nitazungumza na waziri mwenzangu wa elimu tanzania bara kuangalia uwezekano wa kupunguza adhabu hiyo.”
  Amesema kuundwa kwa baraza la mitihani la Zanzibar sio suluhisho la kuepukwa kwa vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wanafunzi katika mitihani yao.
  “Mheshimiwa Spika hata kama Zanzibar itakuwa na Baraza lake la mitihani sio ufumbuzi wa tatizo hilo kwa sababu tatizo la udaganyifu wa mitihani ni la muda mrefu na vijana wetu wamepunguza kasi ya kusomea wanasubiri kuvuja mitihani ndio waanze kutafuta fedha wanunue” alisema Shaaban.
  Waziri alisema wanafunzi 1,200 waliofutiwa mitihani yao hapa Zanzibar ni kutokana na kuthibitika kuwa wamefanya udanganyifu katika mitihani hiyo.
  Alisema wanafunzi hao wamegundulika kuwa katika mtihani ya kiidato cha nne walifanya vitendo vya udaganyifu kwa kushirikiana na wasimamizi wa vituo wakati wa utahiniwa.
  Waziri huyo alisema Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lililazimika kufuta matokeo ya wanafunzi hao baada ya uchunguzi wa kina kufanyika jambo ambalo wizara yake nayo iliunda kamati maalumu ya kufuatilia suala hilo. Aidha Waziri Shaaban ambaye ameiaga wizara hiyo hapo jana alisema kwamba Wizara ya elimu ilichukuwa hatua kwa kulitaka baraza la mitihani la taifa Tanzania (NECTA) kuwasilisha ushahidi baada ya wanafunzi kufutiwa matokeo yao na serikali imelidhika na ushahidi wa Baraza hilo.
  Aliwaambiwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba katika suala la mitihani kwa wanafunzi wa kidatu cha nne uthibitisho umepatikana kwamba wanafunzi walifanya udanganyifu na hivyo suala la kufutiwa matokeo limetokana na kasoro hiyo iliyotokea kwa udanganyifu huo.
  Akitaja hatua za serikali katika suala hilo Waziri huyo alisema baada ya kutafakari kwa kina na kushauriana na wataalamu mbali mbali wa wizara yake serikali kupitia wizara ya elimu imeamua kuunda kamati ya kuchunguza kashfa hiyo ya udanganyifu na wasimamizi watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
  Akitaja hatua ambazo serikali iemchukua ni pamoja na Wizara ya elimu na mafunzo ya amali kuchukua jukumu kusambaza mitihani ya kidato cha nne na sita na kusimamiwa katika vituo vya wizara badala ya kazi hiyo kufanywa na watendaji wa mikoa hapa Zanzibar.
  Alisema licha ya kuwa wazazi wengi kuguswa na suala hilo lakini ni vyema wazazi hao wakachukua subra katiak jambo hilo kwani kuendelea kuwatetea wanafunzi ambao wamefanya vitendo vya udanganganyifu ni kutengeneza taifa dhaifu. Akizungumzia adhabu iliyotolewa na NECTA ya kuwazuwia wanafunzi kufanya mitihani miaka mitatu alisema adhabu hiyo ni kubwa na sasa wanapitia adhabu hiyo na kuangalia uwezekano wa kuweza kuipunguza kwani inaweza kuleta athari kubwa kwa wanafunzi.
  “Ni kweli adhabu waliopewa wanafunzi kufungiwa kwa miaka mitatu wasifanye mitihani, adhabu hiyo ni kubwa lakini seriakli zetu zote mbili ya Zanzibar na muungano tumeanza kujadiliana kuangalia upya adhabu hiyo namna ya kutafuta utaratibu mwengine” aliwaambia wajumbe wa baraza hilo.
  Mswada huo umepitishwa na wajumbe wa baraza la wawakilishi ambapo serikali imekubali kubadilisha jina la awali na kuitwa baraza la mitihani la Zanzibar ambapo awali jina lake lilikuwa Bodi ya vipimo na tathmini ya elimu Zanzibar jina ambalo lililalamikiwa na wajumbe wengi wa baraza hilo.
  Moja ya kazi za Baraza hilo ni kusimamia mitihani ya shule ya msingi na mitihani ya kidato cha pili Zanzibar ambapo Waziri Shaaban alisema mitihani ya kidato cha nne na sita itaendelea kusimamiwa kama kawaida na Baraza la mitihani la Taifa Tanzania (NECTA).
  Kwa mujibu wa mswada huo Baraza la mitihani la Zanzibar litafanya kazi ya kupima na kutathmini viwango vya ubora vya elimu ya maandalizi na msingi ili kuinua kiwango cha elimu cha Zanzibar. Waziri Shaaban alisema kwamba Wizara ya elimu na mafunzo ya Amali itaendelea kushirikiana na NECTA na Wizara yake haina mpango wa kujiondoa NECTA kwani wanafanya kazi pamoja.
  “Mheshimiwa Spika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar haina nia wala mpango wa ya kujitoa NECTA tutazidisha mashirikiano kwa kutumia uzowefu wao na utaalamu wao kuendeleza sekta ya elimu Zanzibar.”aliahidi Waziri Shaaban.
  Kabla ya kupitishwa mswada huo wajumbe wakichagia muswada huo walishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuanzisha Baraza lake la mitihani na kuchukuwa majukumu ya kusimamia mitihani yote badala ya kazi hiyo kufanywa na Baraza la Mitihani la taifa Tanzania NECTA ombi ambalo serikali imelikataa.
   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  pole pole jamaa wanatafuta njia

  swali
  kwani ktk mambo ya muungano je mambo ya utungaji wa mitihani yalikuwa ni ya muungano?
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Waunde baraza litakalo sahihisha 1+1 = 4!!!! Wote wapate div. 1
   
 4. ma2mbo

  ma2mbo JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  baraza la mitihani ni suala la muungano..ivo kuunda baraza lao ni kuvunja katiba..
   
 5. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  go go znz
   
 6. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  I say........long overdue
   
 7. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Wakitunga baraza lao ndio watajimaliza kielimu..mambo yote yatakuwa mdebwedo tu!
   
 8. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Punde tu tutaanza kusikia waunguja wanapendelewa zaidi kwenye mitihani kuliko wapemba (or vice versa!) na hilo baraza la mitihani zanzibar!
   
 9. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Sasa sisi watanganyika tufanyeje na hii post yako?
   
 10. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kama kuna
  viongozi wanao
  shabikia ***** huu
  wa kusema eti mwa
  nafunzi kafanya
  udanganyifu basi
  wanaupupu vi
  chwani mwao.
   
 11. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii habari haituhusu sisi watanganyika.
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Maumivu ya kichwa huanza taratibu na then kinakolea
   
 13. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Na zile nafasi za upendeleo vyuo vya juu ( div 4)wazikatae.
  Pesa za elimu ya juu nazo wazikatae
   
 14. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kila mzanzibari ni Mtanzania na sio kila Mtanzania ni mzanzibari. kwa mantiki hio mzanzibari ana kila haki kama mtanzania mwenziwe Mtanganyika kwenye Tanzania, lakini sio kila Mtanganyika ana haki Zote zanzibar
   
 15. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nahisi kama wengi tunajadili hili suala kwa jazba bila ya kusoma kile kilichoandikwa.
  Kwa tathmini yangu ya haraka haraka, kuna wawakilishi kutoka pande zote mbili (angalia hao kwenye nyekundu) ambao hata katiba wala sheria hawazijui. Bahati nzuri, Waziri wa Elimu na Mwanasheria Mkuu wameokoa jahazi, na uthibitisho wa hilo upo kwenye madondoo mbali mbali niliyoyaacha.

  Tukija kwenye kitendo cha kuundwa kwa baraza la mitihani ambalo litashughulikia mitihani ya Zanzibar (Std. 7 na F.II) pamoja na kusimamia kiwango cha elimu Zanzibar, kuna ubaya gani?

  Kwa kueleweshwa tu, mitihani ya darasa la saba TBara inasimamiwa na chombo gani? Ikiwa chombo hicho hakipo, kuna ubaya wowote kwa TZBara kukiunda? Kama kipo, kinaingilia suala la elimu ya juu Tanzania?
   
 16. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Afadhali wakaulizane maswali ya taarabu hawa kupe wa kipemba
   
 17. h

  hamada Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 25, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wacha kujipendekeza, hii post haiwafai hwa jamaaa ona sasa kejeli zao, mbuzi weeee.
   
 18. h

  hamada Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 25, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kitu cha mamako kichogo cha Tanganyika weee! kafundishwe adabu mwanaharamu wee, unawajua wapemba?
   
 19. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka mwishoni mwa miaka ya 80 na hadi miaka ya 90 tulikuwa kila kitu tunapekeleka kwa kufuata balance, uundwaji wa timu ya taifa enzi hizo ni lazima ubalance, wabara wangapi na wa visiwani wa ngapi, bwana Jusa huwa simwelewi kabisa, anaposema, "waliofutiwa mitihani ni wanafunzi 3303 na kati yao 1000 ni wazanziba na waziri wa Elimu hajatoa msimamo wowote" Hivi hapo hoja ni nini? kufutiwa mitihani au wazanzibar waliofutiwa ni wengi kuliko wa bara, swali rahisi kwake ni hili, alipaswa kujiuliza kwanini wamefutiwa mitihani, sio wa wapi wamefutiwa mitihani, tukifika hapo kwenye mawazo ya huyu Mshirazi tutaanza kujiuliza, mbona magereza wazinzibar hawapo?


  Waheshima hawa wa Zanzibar kama kweli wanataka kujiondoa kwenye baraza la mitihani kwa nia njema, binafsi sinatatizo na hilo, lakini wasiwasi wangu unakua hapo kwenye hoja zenyewe, inaelekea wanataka mfumo wa quantinty and not quality.
   
Loading...