Zanzibar Wants Union Constitution Overhauled



kiatu chenyewe ni tanganyika na mguu ni zanzibar si walijifanya wanalazimisha muungano kwa nguvu saivi kila shepu tutafuata.....
 

mhaini na mlevi mwenyeo ulieshindwa kujua hao wanadai nn,,,,kwani si walijiunga kama nchi kamili au? Kama wanataka kutoka waachieni kwani hii ndoa ina ulazima gani hasa wa kuishikilia kwa nguvu zote kama hutakiwi tena ya nini muache,,,,,
 
Maalim Seif aliwahi kusema kabla ya uchaguzi mkuu October 2000:

"If we win I see no reason to stay in the Union. Zanzibaris have not benefited from it one bit. I would go to the mainland and start talks on a program to move toward full independence." - (interview with "Time" magazine, October 2000).


Halafu Wolfgang Dourado alisema yafwatayo:

"The millions and billions of aid and development money that comes into Tanzania, do your research into how much of it comes here. Nothing. We try to talk to them but it's a dialogue with the deaf and dumb." - ( interview with "Time" magazine, October 2000).

Kama Junius, Mzanzibari, alivyoandika katika mjadala mwingine hapa Jamii Forums: "Tushang'oa nanga."
 
kwani sasa hivi tunapata nini kutoka zanzibar ambacho kesho asubuhi tukikuta wameondoka tutakikosa?

hicho nini mnachokipata ndicho kinachowafanya hao viongozi wako waushikilie vizuri muungano na siku watakapoamuwa kuiwacha tu ndio utajua nini kilikuwa kinapatikana zanzibar kwenda kwenye muungano cz kwa wakati huo kitabakia huko huko zenji kuwanufaisha wenyewe wazenji,,,tanganyika daima
 

Well, tell us how much Znz contribute to run the Union government
Why more tha 500,000 znzbarian live in mainland
How much the Tanganyika gov lose through ''free port in znz'' which is a conduit for tax evasion.
Tell us how much tanganyika tax payers money have been used for island payroll.
Tell us who pay 80 MPs in union parliament.
Finally, with 500 billion budget who want to steal from this another Ilala municipal budget.
 
Hakuna faida kubwa ya kuigangania Zanzibar kubaki katika muungano,bado itakuwa katika jumuia ya Africa mashariki,na bado ni jirani zetu,kama majirani wetu wengi tena wakubwa waliotuzunguka kila pembe.
 
kwani muungano lazim!! Si na nyinyi mchukue tabganyika yenu!
na wao muwaache na zanzibar yao!!!
 
"kwa sababu mabadiliko ya katiba ya Zanzibar hivi sasa hayana nguvu bila kukubalika na Bunge la Muungano; sasa Bunge la Muungano litatakiwa kuridhia au kukataa. Likikataa Zanzibar watasema nini?"

Ni kweli hayana nguvu MKJJ... KAMA bunge la muungano likikataa ina maana zanzibar pia imekataa kwa sababu katika bunge la muungano kuna wawakilishi wa zanzibar ndani yake... hapo ndo mchezo mtamu wa politics utakapochezwa... pia option nyingine ni kujiondoa kwenye muungano kitu ambacho ni vigumu kwani maraisi wote huapa kuilinda katiba ya jamuhuri ya muungano wa tanzania na ilivyo sasa, mabadiliko hayo si mabadiliko kamili bali ni referendum isiyokuwa na nguvu za kisheria mpaka pale constitution mama ya muungano itakoporekebishwa...FULL STOP MASINONDA!!!

Nafikri ndo maana Kikwete alisema hiyo GNU si ya milele itakuwa reviewed baada ya miaka fulani... sasa sijui hayo ya Zanzibar kuwa nchi au la yametokea wapi maana referendum ilitakiwa kuwa kukubali au kukataa GNU... MENGINEYO YAMECHAKACHULIWA TU katika hiyo referendum... PIA inawezekana kwamba wanzibar hawajui nafasi yao katika muungano ndio maana wanapelekeshwa na zanzibar politisions... ni wazi kuwa zanzibar ni nchi ndani ya muungano kama ilivyo Tanganyika lakini both Tanganyika na zanzibar hazitambuliki KIMATAIFA kama inchi zenye legal personality kimataifa when it comes to issues SAY of entering treaties and enforcement of binding intenational laws.
Ni JMT pekee (Tanganyika +Zanzibar) ndio ina uwezo kimataifa... hawa wazanzibar wanataka kuchokoza nyuki maana wanafanya watu wengine kama hamnazo vile....

Inanifanya mimi nifikirie kwamba labda hawakubaliani na makubaliano yaliyofikiwa mwaka 1964 kati ya karume na Nyerere waliokuwa wanaziwakilisha nchi zao na kama ndio hivyo basi ina maana kwamba hawayakubali mapinduzi ya watu wa zanzibar yaliyomuweka Karume Madarakini PIA...

Kingine cha kunishangaza ni kwamba katika bunge la muungano wamo wabunge wanaoiwakilisha zanzibar... Kwa nini wabunge wa zanzibar hawakuja na hoja binafsi za hiyo referendum ambayo pia ingehusisha vipengele vya muungano? sina jibu labda walikuwa tu wako pale kudaka tonge mdomoni...

Na CCM wenyewe ndio wamelikologa kwa sababu sidhani kama walitegemea haya mambo ya zanzibar kutambuliwa kama nchi au sehemu ya muungano yangejitokeza... Nadhani walichokuwa wanafikiria ni GNU pekee iliyotokana na mazungumzo kayi ya Seif na Karume...
Karume pia amekosea kwani ameenda kinyume na kiapo chake cha ku-defend constitution ya zanzibar na ile ya muungano aliyoapa kuilinda.. sasa iweje leo akubali mabadiliko ya zanzibar kuwa nchi wakati tayari anajua kwamba zanzibar na Tanganyika ndo zinaunda Tanzania... ina maana pia kwamba Zanzibar hawalitaki jina hili la Tanzania ndo maana wana-insist wao kuwa ni nchi....

Pia nafikiri wamesaidia kuwafanya watanganyika waamuke kwani kama mabadiliko hayo ya zanzibar yakipelekwa kwenye bunge la muungano ni wazi pia kwamba mabadiliko mengine pia yatajitokeza tofauti na hayo wanayoyaomba wazanzibari...

Na kwa sisi tuliozaliwa katika nchi inaitwa Tanzania nafasi yetu iko wapi tunapokwenda Zanzibar kama nchi... hebu waache kutunganganyia mambo... wazee wazima lakini vihivyo wa kufanya mambo kwa kukurupuka...
 
Mwisho kama hawataki.. basi wajitoe.. sioni sababu yoyote ya kuwang'ang'ania ili hali ni kwa faida yao...
 

Huyu Hamza Hassan Juma simwelewi hata kidogo, hivi unaweza kuimarisha Muungano kwa kuvunja Katiba inayounda huo Muungano? Ibara ya 61 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (toleo la 2005) inasema kwamba "Wakuu wa Mikoa wa Tanzania Zanzibar watateuliwa na Rais wa Zanzibar baada ya kushauriana na Rais (wa Jamhuri ya Muungano)." Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar, 1984 yanadai kwamba Rais wa Zanzibar atateua Wakuu wa Mikoa bila kushauriana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Sasa kama marais hawa wawili kila mtu atafanya mambo yake Muungano utakuwepo? Kuungana si kufanya vitu kwa pamoja? By the way, Wazanzibari wanaulalamikia sana Muungano, sasa ni kichekesho kudai kwamba wanachukua hatua za "kuimarisha Muungano." Ridiculous indeed!
 

kwa sababu anataka kuchanganya siasa za blah blah na constitutional law
 
Hakuna awezaye kuzuia kurudi kwa Tanganyika yetu sasa, na wazanzibar wanatusaidia jambo hili litimie haraka zaidi.
 
huwezi kuliziba juana ungo huwezi kuliziba jua huwezi kuliziba


kumekucha sasa ni wakati wa kukubali kuzungumza tukubali kukaa na kuzunguimza tena kwa amani hadi mapovu ya mdomo yajae na tukubaliane nini cha kufanya
 
I guess 'Dr' Karume had something up his sleeve all along, something to do with the kind of legacy that he would like to leave behind and at least be remembered for; his timing is interesting- anajua suala hili litaleta mvutano, but who cares? atakuwa ameshatoka madarakani!

I don't think we need to spend so much energy kuwashikilia hawa jamaa zetu waendelee kukaa kwenye Muungano; hata hivyo ni muhimu wafuate taratibu zinazokubalika kikatiba ili kutimiza matakwa yao.

Sasa naanza kuona mantiki ya kwa nini baadhi ya watu wamekuwa wakisisitiza sana umuhimu wa kuwa na Constitutional Conference...
 
Kosa kubwa ambalo mimi naliona ni kitendo cha kuacha zanzibar iendelee kuwa na rais, wawakilishi huku tanganyika ikiwa imemezwa ndani ya muungano hapo ndipo walipochemka japo inawezekana walikuwa na nia njema lakini kihalisia haikutakiwa iwe hivyo....
Wangefuata hata maneno ya kwenye msahafu wa biblia kwamba ..mtu atawaacha wazazi wake ataambatana na mwenzake mpaka kifo kiwatenganishe lakini muungano wetu haukujengwa ktk misingi hiyo ndiyo maana kila siku unasikia serikali tatu wengine moja kwa sababu tangu mwanzo tanganyika ndiyo ilikubali kuwaacha wazazi wake na kuambatana na muungano.......tunaendelea kutwanga maji kwenye kinu bila sababbu na wakati tunajua fika kuwa haiwezekani...........kama kuna sababu za msingi ambazo ni lazima kkuwe na muungano basi mabavu yatumike kuondoa upuuzi wa wazanzibar wachache kufanya mambo haya makubwa kwa matakwa binafsi isipokuwa lichukuliwe jukumu la kuondoa katiba ya zanzibar ili tuwe na katiba moja na serikali moja na wala sio tatu km wengine wanavyoshauri.............
mwanzo wa haya ni mwisho wa muungano
 


Mnasingizia bure Mwinyi na kuondoa DIRA na MIIKO. Hayo yote tumevuruga sisi wananchi na sio Mwinyi.

Hata hivyo Mwinyi anatakiwa aubembeleze sana huu muungano, sasa ukivunjika , AS PER HUDI mpaka kufa si atamiss?? Ama itakua je hapo?

Nafikiri Kikwete na Mkapa nao wanaweza miss hiyo huduma.

Tungetengana nafikiri ni obvious zanzibar watakua zanzibar sisi tutajiita tu JAMHURI YA TANZANIA. Wataumia hao.

Harafu tukitengena nafikiri maendeleo ndo yatakuja kwa kasi. Mimi nafikiri tutengane tu.
 
Muungano ulipoanzishwa upande wa Bara ndio uliopendekeza na sasa katika mabadiliko ni zamu ya Zanzibar kupendekeza. Ni uungwana kuwa Bara nayo ikubali mabadiliko moja kwa moja kama alivyofanya Karume kwa Nyerere. Usifutuke hiyo ndiyo demokrasia!
 

Kaiba ipi iliyovunjwa? Tueleze kipi kigeni katika mabadiliko hayo? Kuwa Zanzibar ni moja ya nchi mbili za Muungano huu? Kuwa Rais wa Zanzibar kuwa na mamlaka ya vyombo vya serikali ya Zanzibar (mikoa)? Ni nani anaelipia uendeshaji wa Mikoa ya Zanzibar?
TATIZO LENU NI LILE LILE chenu chetu na chetu ni chetu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…