Pakacha, awali ya yote tuchanganye R na L (balubalu na barubaru).
Sijali natoka wapi bali najali naishi wapi na kupata dairy bread yangu.
Ahali yangu ninapochambua jambo siangalii kuwa natoka wapi. Hilo sio tatizo kwangu ila nia ni kufikisha maoni yangu kwa jamii.
Pili , nilitumia tu kifupi cha wapemba na waunguja nikiwa na maana kuna visiwa viwili yaani Pemba na Unguja. Kumbuka kuwa kila penye viwili lazima kuwe na uvutano. ( Mfano Simba na Yanga. Kila mpenzi wa soka huko Tanzania ni lazima awe mpenzi wa timu moja katika hizi ima Simba au Yanga kisha ndio atakuwa na timu nyingine let say Mtibwa, malindi, miembeni au hata African sports au coastal union.
sasa tukizama kwenye historia ya visiwa vyetu utaona kulikuwa na vyama hasimu viwili tokea enzi hizo na kila chama kilikuwa na ngome yake kwenye kisiwa kimoja. na hata hivi leo utaona the same kuna vyama vikuu viwili na kila chama kina dominate kisiwa kimoja.
Sasa pamoja na kuwa na tofauti ya kisiasa lakini watu hawa wanafungamanishwa na DINI moja yaani UISLAMU..
nakushauri usome vizuri sana Historia ya visiwa hivyo bila jazba na kwa nia ya kuelewa utaona hao niliyokudokolea kidogo.