Zanzibar wanafuga kuku wengi kuliko bara...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar wanafuga kuku wengi kuliko bara...?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mpaka Kieleweke, Aug 9, 2012.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Soma hotuba ya kambi ya upinzani hapa ujionee maajabu ya Tanzania; kwa wanaojua mahesabu wanaweza kufanya na kuonyesha hizo ni sawa na kuku ngapi ili kupata tani 100.


  4.0 Vibali vya Uagizaji wa Nyama ya Kuku toka Njeya Nchi

  Mheshimiwa Spika, taarifa ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2011 imeonyesha kuwa nchi yetu ina kuku takribani 58 milioni ambao wanafugwa hapa nchini mwetu.

  Mheshimiwa Spika, pamoja na kuku wote hao bado wizara hii inaendelea kutoa vibali ya kuagiza nyama ya kuku kutoka Brazili, jambo ambalo ni kinyume cha sheria zetu na matamko mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa na serikali hapa Bungeni mara kwa mara.

  Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 05.04.2012 Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Dr. E. J. Sekidio) alitoa kibali cha kuagiza nyama ya kuku kutoka nchini Brazili kwa kampuni ya Frostan Ltd, ya Jijini DSM kibali chenye namba 000551 cha kuagiza kiasi cha kilo27,100 au tani 27.1 ya nyama zakuku.

  Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 20.07.2012 Mkurugenzi Mkuu huyo huyoalitoa kibali kingine chenye namba 00000409 na code namba 0655 kwa kampuni ya MALIK FARAJ CO.LTD cha kuagiza nyama ya kuku kutoka Zanzibar kiasi cha katoni 10,000 zenye kilo 10 kwa kila katoni moja na hivyo ni sawa na kuagiza kilo 100,000 au tani 100 za nyama ya kuku kwa ajili ya migodi ya kuchimba madini ya Barrick.

  Kambi Rasmi ya upinzani inataka kupata majibu ya kina kuhusiana na vibali hivi na kama ni sahihi kuendelea kuagiza nyama ya kuku kutoka nje wakati wapo wafugaji wa kuku hapa nchini. Aidha, tunataka kujua nyama za kuku kiasi cha tani 100 zilizoagizwa kutoka Zanzibar ni kutoka nchi gani? Au ni kutoka Zanzibar? Na kama ni kutoka Zanzibar wanahitaji kibali cha kusafirisha nyama kuja bara?
   
 2. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kule Zanzibar ni. Free port ya vitu vingi na si kuku pekeyake. Na ndiyo maana TRA hawapendwi kama sumu Zanzibar. Ubaya zaidi tunaweza letewa kuku kutoka tusipokujua wakapitia Zanzibar na wakatusababishia madhara makubwa kwa afya zetu na mifugo yetu pia, mfano virus cya mafua ya ndege
   
 3. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  hii inataka kufanana na ile ya nguzo za Tanesco kutoka Africa kusini ,kumbe ni za mufindi!
   
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,897
  Likes Received: 2,317
  Trophy Points: 280
  Hata KILA Mazanzibari akifuga kuku 10 kila mmoja(kitu ambacho Wazenj hawakijui) bado wataagiza kuku toka Tangayika.
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  ila unaweza kuta ndio walaji duni wa kuku kuliko bara.....
   
 6. m

  mkataba Senior Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kushapigwa na akili zako na chuki binafsi dhidi ya Wazanzibari, utawaona hivohivo lakini chuki zako hazitosaidia kudumaza mawazo yao ya kudai nchi yao.
   
 7. m

  markj JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  hivi vitu ninanyovitumia hapa bara na vingi vina mazara kwetu! Na tbs wanavialalisha mbona hatuvitazami! Je hivi vinavyo tengenezwa hapa? Nyama tunayokula unaijua usalama wake? Hata huku ndo kubaya kabisa na vitu vinaingia kwa ushuru tena mkubwa na bado ni feki na vinamazara
   
 8. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,897
  Likes Received: 2,317
  Trophy Points: 280
  Hatuwezi kuwachukia Wazanzibari bwana , Zanzibar ni nchi atii!
  Twasubiri tu biashara ya kuuza kuku kwa dola nchini kwenu.
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,734
  Trophy Points: 280
  Ok wazenj wako juu!
   
 10. majorbuyoya

  majorbuyoya JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,815
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  unataka kusema huyo jamaa chuki zake haziwezi kuwadumaza wazanzibari mawazo yao kwa mara ya pili? maana kila mtu anajua kuwa wazenji tayari mawazo yao yashadumaa especially kwa kulalamikia mambo yasiyo na msingi.
   
 11. Mkaguzi

  Mkaguzi JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hii ni rushwa dhahiri. Ukienda wizarani pale wanakuambia hairuhusiwi kuimport kuku sasa vibali vilitolewaje? waziri na kajibu kisanii sana
   
 12. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  ni ngumu, hizo statistics wanapata wapi?Wapo watu kibao wana kuku kibao tuu hakuna nayehesabu,ila hawa jamaa wanakuja na data zao kimeo.Tatizo ni distribution ya hizo kuku huku bara na consumer kuwa wengi sana.Zenji ni wachache na wana pia mazao ya bahari, huku wengine wakiwa na pato dogo sana kiasi cha kuwafanya wasiwe watumiaji wazuri wa kuku kama si wafugaji.

  Hao jama wanaoingiza kuku wana uwanja mpana kama wanaleta kuku ambao ni genetically modified na wanatoak katika nchi ambazo watu wanawafyatua kama kuzalisha nyanya.Bei itakuwa chini sana na pengine wanapewa bei sawa na bure kama kuna mkono wa watafiti ambao hawajapata pa kufanyia huo utafiti.
   
 13. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Zanzibar wanaagiza kuku wao kutoka Brazil nasikia...
   
 14. Mkaguzi

  Mkaguzi JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wote hao wanatoka Brazil lakini wizara ilishasema imesimamisha uagizaji wa kuku kutoka nje ya nchi sasa hivi vibali vilitolewa vipi tena. Pia kama umepata bahati ya kuona hao kuku huwa wanauza 4000 - 5000 na mostly ni majunk. This will definitely killl our Poultry Farming in TZ which has recently employed a lot of Tanzanians.Serikali inatakiwa kulitizama hili swala kwa jicho la tatu na waache Kudanganyika na vijirushwa mbuzi. Huyo Dr Sekidio aweke uzalendo mbele na sio masilahi binafsi.
  Waziri nae anasubiri hadi yasemwe Bungeni ndo anatuambia kibali kilikua feki??? what a nonses
   
 15. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Kama mh.alisema kwa usahihi,natilia mashaka hivyo vibali kwenye red,kibali cha tarehe 05/04/2012 ni na.0000551 na cha tarehe 20/07/2012 ni na.0000409,wapi na wapi hizo serial numbers?
   
 16. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,093
  Likes Received: 1,477
  Trophy Points: 280
  Wazanzibar wengi wanachukia TRA kwa sababu imegundua janja yao ya kupitisha mizigo kinyemela halafu wanaingizia bara kuna kipindi wakati Nahodha akiwa waziri kiongozi alikuwa na mazungumzo na mabalozi wa Tanzania nje ya nchi na moja ya mambo waliyomuulizia ni kuhusu kuifanya Zanzibar kuwa free port alichowajibu hata Zanzibar ikiwa Free port bado soko lao kubwa linategemea bara.Kwa taarifa hiyo utaona Wazanzibar ndio wanatuhujumu kwa kiasi kikubwa na kwa sababu juzi wamepiga marufuku chakula kuletwa bara nategemea pia watapiga marufuku na hao kuku wasiletwe kwani kama walivyosema serikali yao inajitahidi kuleta chakula kwa bei nafuu lakini wafanyabiashara wanakivusha huku
   
 17. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  dawa ni kuuvunja muungano.
   
 18. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu rodrick alexander enzi za mzee Ruksa waZanzibar walitugeuza sisi wabara soko lao ndiyo maana leo unasikia kelele nyingi za kutaka rais ajaye atoke Zanzibar ili watunyonye tena.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...