Zanzibar wajiandaa kudai Referendum for Independence + Devolution Max

Zanzibar wajiandaa kudai Referendum for Independence + Devolution Max

ugwenousangi

Member
Joined
Sep 11, 2012
Posts
98
Reaction score
29
Wakuu habari za ndani kabisa kutoka Visiwani ni kuwa tayari watu wa kule washaanza na Plan B wakati Dodoma bado ngoma mbichi.

Kuna watu wa Intelligentsia (sio inteligensia) ambao wana asili ya Pemba na Unguja (wamo CCM, CUF, waaio na vyama) wanajiita "Zanzibar First " na ni wasomi, wana influence, wana pesa, wako cultured, wako socially aware, wako exposed na dunia inavyokwenda na wana linkages na network na wenzao toka nchi mbali mbali dunian wameandaa "White Paper" au tuseme Blue Print ya future ya Znz na hoja zao kuu mbili ni

1.wapewe referendum for independence ili waamue kama wawe huru au waendelee kuongozwa toka Dar/Dodoma

2. Kura zao zikiwa NO wanataka Znz ipewe kitu kinachoitwa DEVOLUTION MAX ambayo watajotawala kwa kilakitu kasoro DEFENCE na FOREIGN AFFAIRS

White paper yao inaelezea jinsi gani watakavyo jitawala, kiuchumi, kijamii na kisiasa na wamejikita zaidi kwenye uchumi.

Inavyoonekana wanasiasa wote wa CUF na CCM ambao wanakula kuku kwa system iliopo watapata taabu sana kwani hawa jamaaa wamejiandaa kisawa sawa sasa cha kujiuliza je hawa jamaa wanajaribu kuwapindua viongozi walipo au vipi?

Nikipewa rukhsa na aliteninitumia hii doc naweza kuiweka hapa kwa faida ya wote.

Stay tuned...
 
Haya sasa. Km hii ni kweli kwa maana ya sasa inaweza kuwa kweli lkn huko tuendako hili haliepukiki. Katiba mpya ilitakiwa kumaliza kila kitu lkn naona maintarahamwe wapokwa fahamu kabisa kuhusu hili
 
inawezekana n kweli ndo mana jana mwanasheria mkuu wa zanzibar ame vote NO
 
nyie tanganyika mnaponzwa na kitu gani kuingangania zanzibar kiasi icho??? km si njaa na choyo, kama visiwa mnavyo tele, kama bahari mnayo, kama ardhi mnayo, sioni mnachohitaji kutoka zanzibar

Tatizo ndo mana mnaendeshwa wengi wenu ni wanafiki na mamluki mfano bunge la katiba posho na mishahara inatoka Tanganyika,no free lunch
 
kama ni kweli tanganyika itafufukia zanzibar
 
Hilo haliepukiki!! CCM walitakiwa kuutumia vizuri mwanya wa katiba mpya kutatua kero za wananchi, badala yake wameongeza kero kwa wananchi!!

Katiba ni maridhiano, ilitakiwa wakae na upande wa Z'bar kufikia muafaka sahihi juu ya mustakabali wa Nchi hizi mbili. Lakini pia walitakiwa kuijumuisha Tume ya Warioba ktk mchakato mzima ili wasaidiane kutafuta maridhiano ya nini Wananchi wanataka, SIO KURAZIMISHA MAMBO!! Hii liwake jua ama mvua inyeshe tuendako ni lazima MACHAFUKO YATOKEE!!
 
tunaomba iwe kweli,zisiwe porojo.shikirieni hapo hapo wznz.nafasi hii adhimu,haitojirudia.
 
Wakijitenga watanganyika tutawafukuza wazenji wote wahamiaji huku bara wakiwemo mawaziri waliojenga huku na wapemba.
Itakua ni kinyume cha sheria za kimataifa,pia usisahau ukanda wa pwani wote ni milki ya zanzibar,dar,tanga,pwani,mtwara,lindi.
 
Wakijitenga watanganyika tutawafukuza wazenji wote wahamiaji huku bara wakiwemo mawaziri waliojenga huku na wapemba.

Jitahidi kuficha hisia zako. Nchi zinapojitenga huwa kunatolewa muda e.g 6months ili raia wapate wasaa wa kuchagua ,either kukana uraia wa nchi zao e.g Patel. ama wafate taratibu za uhamiaji .
 
Yawezekana kabisa!!!!

Wakiamua chao haswa Wapemba, wanajua jinsi ya kwenda!!!
"Watachomana ndevu" mpaka kieleweke!!!!
 
Wakuu habari za ndani kabisa kutoka Visiwani ni kuwa tayari watu wa kule washaanza na Plan B wakati Dodoma bado ngoma mbichi.

Kuna watu wa Intelligentsia (sio inteligensia) ambao wana asili ya Pemba na Unguja (wamo CCM, CUF, waaio na vyama) wanajiita "Zanzibar First " na ni wasomi, wana influence, wana pesa, wako cultured, wako socially aware, wako exposed na dunia inavyokwenda na wana linkages na network na wenzao toka nchi mbali mbali dunian wameandaa "White Paper" au tuseme Blue Print ya future ya Znz na hoja zao kuu mbili ni

1.wapewe referendum for independence ili waamue kama wawe huru au waendelee kuongozwa toka Dar/Dodoma

2. Kura zao zikiwa NO wanataka Znz ipewe kitu kinachoitwa DEVOLUTION MAX ambayo watajotawala kwa kilakitu kasoro DEFENCE na FOREIGN AFFAIRS

White paper yao inaelezea jinsi gani watakavyo jitawala, kiuchumi, kijamii na kisiasa na wamejikita zaidi kwenye uchumi.

Inavyoonekana wanasiasa wote wa CUF na CCM ambao wanakula kuku kwa system iliopo watapata taabu sana kwani hawa jamaaa wamejiandaa kisawa sawa sasa cha kujiuliza je hawa jamaa wanajaribu kuwapindua viongozi walipo au vipi?

Nikipewa rukhsa na aliteninitumia hii doc naweza kuiweka hapa kwa faida ya wote.

Stay tuned...
Mkuu Ugweno Usangi, asante kwa hii, kiukweli siogopeshwi na hatua hii, mabadiliko ya 10 ya katiba ya Zanzibar, yameweke sheria ya referendum, ningeogopa sana kama Zanzibar wangeamua kupiga kura ya YES or No kuhusu muungano!.

Pasco
 
Mkoa wa zanzibar hauwezi kujiendesha kama nchi..bajeti yao yote inatokana na mapato ya bara
 
Back
Top Bottom