Haya kuna ile hadithi ya punda aliyetaka kwenda njia mbili,akaishia kufa.Sasa sijui hawa wenzetu wanataka nini?Wakija bara serikali mbili,wakiondoka serikali tatu.Mh!:shock:😕
Keissy aliwaambi nji nyeupee, jhakuna aliyetoka mjengo! Ungewauliza waikuwa wanasubiri nini, na je walihitaji nguvu za kutoka mjengoni kuelekea bandarini.Ni hatari sana Zanzibar ni nchi lakini wananchi wake sio raia ni wakaazi tu, Kuna haja Zanzibar kufanya Mapinduzi makubwa sana kujivua kutoka kwa watanganyika kwa nguvu zote ata kama hawatak. Ni aibu miaka 50 toka uhuru wazanzibar siyo raia ndani ya nchi yao
Mkuu Mwiba, asante kwa hii!.Baada ya Kuufyata sasa afyetuka baada ya kuzomewa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeshauriwa kuwa na uraia kwa watu wake pamoja na kuvipa hadhi vikosi vyake maalumu ili viweze kumiliki silaha za kivita chini ya mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
wakati umefika kwa vikosi vya SMZ kupewa hadhi ya kumiliki silaha za kivita badala ya kumiliki silaha za kawaida kama ilivyo sasa kwa mujibu wa sheria.
ni wakati mwafaka na unaofaa kwa SMZ kununua silaha kama mizinga, vifaru, helikopta za kivita na boti za kijeshi pamoja na silaha nzito kama RPG.
Huwezi kuwa na nchi bila ya kuwa na raia. Alitaka Wazanzibari kupewa uraia wao katika mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema ni jambo la kushangaza Wazanzibari kuitwa wakazi na si raia.
hatua ambayo itaipa hadhi nchi na kutambulika kitaifa na kimataifa.
Ndo maana limeshaanza kutiwa viraka ili litoshe...
Watanunua na nini hiyo mixinga wakati tunawalipia mishahara ya wafanyakazi SMZ na kuwalipia umeme!Baada ya Kuufyata sasa afyetuka baada ya kuzomewa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeshauriwa kuwa na uraia kwa watu wake pamoja na kuvipa hadhi vikosi vyake maalumu ili viweze kumiliki silaha za kivita chini ya mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Ushauri huo ulitolewa jana na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wakichangia makadirio na matumizi ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Vikosi Maalumu iliyowasilishwa na Waziri wake, Haji Omar Kheir, Chukwani mjini Unguja jana.
Akichangia bajeti hiyo, Mwakilishi wa Koani, Mussa Ali Hassan alisema wakati umefika kwa vikosi vya SMZ kupewa hadhi ya kumiliki silaha za kivita badala ya kumiliki silaha za kawaida kama ilivyo sasa kwa mujibu wa sheria.
Hassan alisema kuna vikosi vya SMZ ambavyo havina tofauti na askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambavyo vilishiriki kupambana na majeshi ya Idd Amini yalipovamia Tanzania mwaka 1978.
Alisema ni wakati mwafaka na unaofaa kwa SMZ kununua silaha kama mizinga, vifaru, helikopta za kivita na boti za kijeshi pamoja na silaha nzito kama RPG.
Wajumbe wengine, Amina Idd Mabrouk (Viti Maalumu), Jaku Hashim Ayoub(Muyuni), Raha Suleiman (Viti Maalumu), waliitaka Serikali kuangalia masilahi ya askari wa vikosi vya SMZ ikiwamo kuwapatia vitendea kazi pamoja na kuwajengea makazi bora.
Wawakilishi hao kwa nyakati tofauti walidai kuwa nyumba nyingi za makazi ya askari ni chakavu na hazistahili kukaliwa na askari ambao wanalinda nchi huku wananchi na viongozi wakiishi kwenye makazi bora.
Pia waliitaka SMZ kutambua umuhimu wa kuwalipa posho na marupurupu stahiki kwa muda wa kazi wa ziada askari wa vikosi vya SMZ pamoja na kuwaingiza katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).
Akizungumzia uraia, Mwakilishi wa Chambani, Mohamed Mbwana Hamad alisema: Huwezi kuwa na nchi bila ya kuwa na raia. Alitaka Wazanzibari kupewa uraia wao katika mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema ni jambo la kushangaza Wazanzibari kuitwa wakazi na si raia.
Alisema Wazanzibari wote wanatakiwa kupewa hadhi ya uraia na wageni ndiyo wanaostahili kuwa na vitambulisho vya ukaazi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, hatua ambayo itaipa hadhi nchi na kutambulika kitaifa na kimataifa.
Keissy aliwaambi nji nyeupee, jhakuna aliyetoka mjengo! Ungewauliza waikuwa wanasubiri nini, na je walihitaji nguvu za kutoka mjengoni kuelekea bandarini.
Ukishajua, then ...! Jadili hoja suala la vyama halina mantiki kwenye hii hoja
Kutoka bungeni na kielekea bandarini bado wazanzibar hawajajitoa kwenye himaya ya Tanganyika, kujitoa ni kuvunja muungano huu wa kidhalim ambapo Kessy na Lukuvi walienda makanisani wakasema haiwezekani Zanzibar kupatiwa mamlaka yao, kwa lugha nyengine Tanganyika hawataki Zanzibar iwe huru. Tanganyika ndio kikwazo hamtaki kutuacha munatungangania.
Kutoka bungeni na kielekea bandarini bado wazanzibar hawajajitoa kwenye himaya ya Tanganyika, kujitoa ni kuvunja muungano huu wa kidhalim ambapo Kessy na Lukuvi walienda makanisani wakasema haiwezekani Zanzibar kupatiwa mamlaka yao, kwa lugha nyengine Tanganyika hawataki Zanzibar iwe huru. Tanganyika ndio kikwazo hamtaki kutuacha munatungangania.
mbona mnafurahia kung'ang'aniwa.. mnapenda sana umeme wa bwelele.. tulia mpate vya bure..ila msilalame hiyo ndio impact ya vya bwelele..
Ni hatari sana Zanzibar ni nchi lakini wananchi wake sio raia ni wakaazi tu, Kuna haja Zanzibar kufanya Mapinduzi makubwa sana kujivua kutoka kwa watanganyika kwa nguvu zote ata kama hawatak. Ni aibu miaka 50 toka uhuru wazanzibar siyo raia ndani ya nchi yao