Kwahiyo familia yenye mtoto mmoja hiyo sio familia? Ila familia yenye watoto wengi ndio familia?
Itambulike Serikali ya zanzibar ni serikali - na wala sio kwa kejeli wala kufanya mzaha - Zanzibar inahistoria yake - sio ya kimkoa wala wilaya. Hakuna wilaya yoyote ama mkoa uliofanya kikao cha muungano ili wajiite tanganyika. historia yetu na mipaka yetu ya kikoloni ndio imejenga utanganyika, na historia hiyo ndio inayoitofautisha zanzibar - na kujenga muungano. Hatuwezi kudharau vitu hivi, kirahisi rahisi tu. Kufunika funika tu kwa kuwa tunapenda muungano.
Ndani ya katiba yetu, tunatambua kabisa zanzibar sio mkoa wala wilaya - kwa ukosefu wa maneno ama uoga wa kujitawala tumeita Tanzania Zanzibar - na ikasemwa kwamba Rais atashauriana kwanza na "Rais wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika Mikoa, Wilaya au maeneo mengineyo" katiba. Kwahiyo, zanzibar yenyewe sio mkoa wala wilaya !
Ha ha ha ha ha! Utalii wenyewe wa Zanzibar uko wapi? Watalii wenyewe wanaungaunga kutoka Bara. Muungano ukifa na utalii wasahau - hiyo ndio habari japo chungu masikioni. Sana sana hilo ni shamba la karafuu tu.
:juggle:KATIBA YA SASA YA ZANZIBAR
Ibara ya 3 na 4 ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar inasema hivi:canada:
"Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar."
Vilevile, Ibara ya 4 ya sheria ya mabadiliko ya katiba inasisitiza, "Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."
Ibara mpya ya 26(1) inayounda "Afisi" ya rais wa Zanzibar inamtaja rais wa Zanzibar kama "… Mkuu wa nchi ya Zanzibar…"
Ibara mpya ya 2A ya Katiba ya Zanzibar inampa rais wa visiwa hivyo mamlaka ya kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu wa sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
Ibara mpya ya 24(3) ya katiba ya Zanzibar inasema, kutokana na maombi yanayopelekwa mahakamani kuhusu masuala ya haki za binadamu, uamuzi wa mahakama Kuu ya Zanzibar "… utakuwa ni wa mwisho na hautokatiwa rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa ya Tanzania."
HAKUNA TANZANIA BILA YA ZANZIBAR
ZANZIBAR ILIFANYA MISTAKE KUUNGANA NA TANGANYIKA NDIO KUKAUNDWA JINA LA TANZANIA KAMA MUUNGANO HUU USINGELITOKEA BASI KUNGEKUWA HAKUNA JINA LA TANZANIA DUNIANI!!!!!!!!
MAURITIUS , SEYCHELLES, COMORO, VISIWA HIVYO VYOTE NI NCHI KAMILI NA NI MAJIRANI WA ZANZIBAR KATIKA BAHARI YA HINDI NA ZANZIBAR NI KUBWA KI ENEO KULIKO VISIWA VYOTE HIVYO NA POPULATION YA WATU WA ZANZIBAR NI KUBWA KULIKO VISIWA HIVYO!!!!!!!!!!!
WATANGANYIKA TUWACHE TABIA YA KUWAONEA NA KUWATISHA WAZANZIBARI KWA SABABU TUKO NA JESHI, DINI HAISEMI HIVYO TUWACHIE NA NCHI YAO WAFANYE MAMBO YAO KIVYAO KAMA VISIWA VYENGINE TU DUNIANI VYOTE VIKO NA FREEDOM YAO!!!!!!!!
Zanzibar ikiwasilishwa katika UN umoja wa mataifa 1963
KAMA WEWE NI MTANGANYIKA HALISI BASI IJUE HISTORIA YA NCHI YAKO KULIKO KUBERULIWA BERULIWA
TUU NA MAJACUC:focus:
Historia zinaonyesha visiwa na nchi nyingi zinaomba uhuru wao, Sudani ya kusini imefanya hivyo. Ila gharama ya uhuru katika Tanzania itakuwa nini nini? Kama tunaangalia hilo, basi tujadili kwa mapana bila kutoa dharau kwa Zanzibarukiona kijana analazimisha kuitwa familia tofauti na familia ya baba yake na hajaoa wala hana mtoto ujue huyo ni chizi.
anamtukana baba yake,
zanzibar haiwezi kuwa nchi na wote watakaoleta chokochoko tunawafungulia kesi ya uhaini.
Mwaka 1987 utumwa ulifugwa Zanzibar chini ya Sultan Hamoud Muhammed kwa matakwa ya waingereza. Mwaka Dec, 1963 ilipata uhuru wake toka kwa muingereza. Mapinduzi 1964 kama tunavyofamu muungano wetukihistoria zanzibar ni soko, bidhaa nyingi ilokuwa inauzwa hapo na waarabu ni wanyamwezi na wamakonde, kama kuna mtu anajua lini hili soko liligeuka kuwa nchi anijuze!
Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ina mamlaka ya kujiamulia mambo yake ya ndani kama uvuvi, kilimo, maji ya kunywa nk! Hivyo kimataifa Zanzibar haina mamlaka wala haki ya kijiwakilisha. Zanzibar haiwezi kuwa na jeshi lake la ulinzi vinginevyo itahesabiwa imeasi na adhabu ya muasi inafahamika. Rais wa Zanzibar hawezi kuwa amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama.