Angalia nchi nyingine zenye population ndogo - sio kigezo peke hicho. List of countries by population - Wikipedia, the free encyclopedia
Ukifuata katiba, Zanzibar sio nchi ila ni sehemu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hili sio geni wala la kutugwa - na wala hamna mtu anayepinga hili. Swala la hapa, ni hali halisi inayoendelea - tanganyika imefanikiwa kujivuta na kuwa tanzania bara - na kubebwa na mikoa yake 25, na tunaitwa tanzania bara - mara nyingi Tanzania tu.Petu Hapa
labda utuambie kipi hujaelewa mwenzetu kwenye hayo majibu ya wadau hapo juu tukusaidie kufafanua mkuu
NB zingatia post ya chigwiye
Unajua Zanzibar kuwa au kutokuwa nchi inategemea wewe binafsi unatafsiri neno "nchi" katika context gani. Kama ukitafsiri neno nchi katika context ya kisiasa kwa kanuni za Umoja wa Mataifa, basi Zanzibar si nchi. Kama ukitafsiri neno nchi kwa mintilafu ya kimsaafu kama Biblia na Kurani, basi Zanzibar ni nchi, maana Mwenyezi Mungu aliumba mbingu na nchi - na nchi haikuwa na mipaka. Na pia kama unataka kutafsiri nchi katika misingi ya Katiba ya JMT basi si Zanzibari wala Tanganyika zilizo nchi. Na pia kama unataka kuangalia mambo katika context ya kiu-Zanzibari na Kiu-Zanzibara basi Zanzibar ni nchi. Sasa chaguo ni lako na sisi wenye akili hatuhitaji kubishana na wewe juu ya hili!
zanzibar ni kisiwa cha utalii
Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ina mamlaka ya kujiamulia mambo yake ya ndani kama uvuvi, kilimo, maji ya kunywa nk! Hivyo kimataifa Zanzibar haina mamlaka wala haki ya kijiwakilisha. Zanzibar haiwezi kuwa na jeshi lake la ulinzi vinginevyo itahesabiwa imeasi na adhabu ya muasi inafahamika. Rais wa Zanzibar hawezi kuwa amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama.
Kwa nini kung'ang'ania kujua kama Zanzibar ni nchi au kitu kingine? Ni vizuri kuainisha faida na hasara za muungano ulioipelekea Tanganyika kupoteza uhalali wake na Zanzibar kubakia kujidai na kutafuta makuu zaidi.Muungano tunaweza kuuongelea kwa hisia tofauti na tukasema yote tunayotaka kusema. Lakini sasa naona kuna haya maneno maneno ya kusema Zanzibar si nchi. Je hii dhana ni sahihi ? kutoka kipengele kipi cha katiba? Ama ni kwa hisia hisia zetu tu? Iwapo ni hisia tu, ni haki kweli kuvua utambulisho wa eneo kikejeli kejeli kweli. Na kama sio nchi, Zanzibar ni nini sasa? Mkoa? wilaya ama ni kitu gani?
Kwa nini kung'ang'ania kujua kama Zanzibar ni nchi au kitu kingine? Ni vizuri kuainisha faida na hasara za muungano ulioipelekea Tanganyika kupoteza uhalali wake na Zanzibar kubakia kujidai na kutafuta makuu zaidi.