Zanzibar Rais ni Nani Shein au Seif? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar Rais ni Nani Shein au Seif?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtu wa Pwani, Oct 12, 2010.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  naam wakuu

  nimeona polls mbali mbali tafiti mbali zikionesha nani atakuwa Rais wa Muungano ambazo bila shaka ni JK


  ila sijasikia si Redet, si wengine wakizungumzia kuhusu zanzibar

  sasa nani tutegemee atashinda na kua Rais wa Zanzibar?  ila kwa maoni yangu Dr shein ni chaguo la wazanzibar
   
 2. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Shein hana pesa ya Kuhonga REDET na SYNOVET
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Seif anasema yeye atafanya uchumi ukuwe kwa asilimia kumi kwa kuanzia na mwaka wa tano itafikia asilimia kumi na tano

  jamani wana uchumi huu si uongo wa mchana?
  chi gani duniani ilioweza kukuza uchumi wake kwa 15%
  n
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Haukusikia aliposema anahakikisha mafuta yaliopo Tundauwa yanachimbwa kwa kishindo ?? Huyo ni Seif kaka hana mchezo ,mambo yake ni papo kwa papo ,Kipindapinda upo ?
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kiseif seif nambie nchi gani na hata hizo zenye mafuta ambazo zinakua uchumi wake kwa 15%

  mwambie balahau atudanganya nchana
   
 6. M

  MLEKWA Senior Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nitakueleza ukweli mt uwa Pwani CCM inagiopa hizi polls kwa visiwan iwkani inajijua kuanzia mwaka 1995 CCM haina uwezo wa kushinda visiwani huu ndio ukweli kila mtu anaujua na CCM hawatokubali kwa hilo kufanyika hizi polls viiswani kwa kuhofia aibu.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280

  Mtu wa Pwani,

  ..Zenj wataanza kuchimba mafuta.

  ..pia wanapata umeme wa bure toka Tanganyika.

  ..watajiunga na OIC.

  ..watapewa 50% ya faida za BOT.

  ..bandari huru itaanza kufanya kazi na Zenj itakuwa kitovu cha biashara mashariki na kusini mwa Afrika.
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Sasa unashangaa nini?? No wonder unamshabikia JK sana...!! Hivi unafikiri kwa hali ilivyo sasa kama ni ZERO corruption unafikiri uchumi wa nchi kama zetu unaweza kukuwa kwa kiasi gani kwa miaka miwili tu ya kwanza. Sasa kama Chenge pekee yake amakomba mabilioni halafu anakwambia ni visenti tu, sasa jaribu kuimagine kuna akina Chenge wangapi TZ??? Pesa kama hizo pekee zikiokolewa unajuwa uchumi utapanda kwa kiasi gani??? Wewe mwenzetu inawezekana uko kwenye circle ya kina Karume ndiyo maana uko kihiyo!!!!
   
 9. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ziko nchi nyingi zina opportunities nyingi kuliko hizo ni nchi gani duniani narejea ilioweza kukuza uchumi wake kwa asilimia 15 seuze huyu anaeota kwa kusubiri kusaidiwa na nani kasema watapewa 50% ya BOT?

  ukweli siamini ila nataraji alikusudia kuwapiga kamba wale wanachama wake pale
   
 10. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  mbona Karume hata MaCUF wanamkubali

  na jitihada zote hajawahi kufikisha 15% tuzungumzeni realistic
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Kawambie waache kugawana pesa zetu, ndiyo utajuwa kuwa uwezo wetu ni kiasi gani. Unashangaa nini wakati uchumi tu wa Shelisheli yenye watu 80,000 ni mkubwa kuliko wa ZNZ yenye watu 1,000,000???
   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  bado hamtaki au mnataka kunizungusha ni nchi gani 15% uchumi wake umekuwa iwe na watu wengi au kidogo?

  au zanzibar itakuwa ya kwanza ?
   
 13. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtu wa pwani si ajabu zanzibar kua ya kwanza kwani hata muundo huu unaokuja wa serikali ni nchi ya kwanza.

  Uchumi wa china unakua kwa 20%

  halafu nyie ccm hamna ilani au sera? Maana badala ya kutangaza sera zenu munaanza kusema hili haliwezekani blaablaa...
   
 14. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wapi

  china hajafika hata 12% usianze uongo wa mchana
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sasa wewe unauliza maswali na majibu unatoa mwenyewe ukiambiwa otherwise unabisha, this is wht is called childish!!!!!
   
 16. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mtu wa Pwani sijuwi huwa unakunjwa nini halafu unakuja na hadithi za ajabu jamvini...wapi na lini Shein alikuwa ni chaguo la wazanzibari?
  Si ndiyo huyo watu walivunja chupa kule Bwawani waliposikia kachaguliwa?
  Nani alikuja kumpokea Shein kutoka Dodoma kuja Zanzibar...si watanganyika?
  Nani alimpigia kura huko Dodoma...si Watanganyika?
  Mtu wa pwani...mtafutie Shein mbeleko inayomfaa usimweke katika migongo ya wazanzibari, si chaguo lao... Shein anawajuwa waliomuweka na yupo hapo kulipa fadhila wakifanikiwa kumlazimisha atawale!!!
   
 17. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Junius fatalia ni jinsi gani mikutano ya Dr Shein inavyohudhuriwa na wazanzibari wengi kuliko wa maalim


  angalia uone jinsi sera za shein zinavyorejesha matumaini kwa wazanzibari
   
 18. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Shein ana sera za sasa na si CCM!!!

  Kwa taarifa yako, huko visiwani ni Seif tu mtake msitake. Karume alishaona hilo ndiyo sababu akakubali mseto. CCM hawawezi kuchakachua matokeo kotekoete yaani bara na visiwani hivyo nguvu zote zinahamishiwa bara.
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Je unaelewa kuwa Karume alikuwa ni CUF ,je unaelewa kuwa Kikwete alikuwa CYF na inasemekana bado wana imani na Chama hicho.

  Halafu Zanzibar ni kisiwa kidogo sana hivyo wakifanikiwa kufukua matangi 1000 kwa siku basi baada ya mwaka watakuwa kwa wananchi wake hawana haja ya kufanya kazi na magari yao yatakuwa yakijazwa petroli bure ,nyie huko Tanganyika waacheni akina chenge wawachague.
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Oct 13, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Mtu wa Pwani,

  ..wa-Zenj wako makini sana na masuala ya uchaguzi.

  .si rahisi Redet kupeleka michezo ya kitoto kwa wa-Zenj.

  ..kuhusu kukua kwa uchumi wa Zenj nadhani potential hiyo ipo. Zenj ni eneo dogo sana na kuna fursa kama za utalii, uvuvi, kilimo, biashara na viwanda. wa-Zenj wakiwa makini wanaweza kupiga hatua kubwa tu za kiuchumi.

  ..kitu ambacho ningeshauri kiongozi yeyote yule wa Zenj kukishughulikia kwa haraka sana ni kupunguza ukubwa wa serikali na baraza la wawakilishi. linganisha idadi wa wawakilishi iliyokuwepo mwaka 1964 na hii iliyopo sasa hivi. naamini huo ni mzigo mkubwa sana kwa wananchi wa Zenj.
   
Loading...