Zanzibar na Comoro zina mahusiano Maalumu

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
817
514
ZANZIBAR NA COMORO INA MAHUSIANO MAALUM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar na Comoro zina Mahusiano maalum ya kuchanganya damu wa kindugu hivyo ameridhia kufunguliwa kwa Konseli Mkuu wa Comoro hapa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo alipokutana na Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Comoro Mhe. Saidi Yakubu aliyefika kumuaga baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Zanzibar tarehe 14 Mei, 2024.

Rais Dk. Mwinyi pia amemtaka Balozi Yakubu kuangalia fursa zilizopo za kuuza bidhaa mbalimbali kutoka nchini na kuzisimamia hati za makubaliano ya pamoja na kamati ya ushirikiano wa kudumu ikiwemo katika sekta ya afya, elimu, utamaduni, biashara, usafirishaji na habari kupitia shirika la utangazaji Zanzibar (ZBC).

Aidha Rais Dk. Mwinyi amesema Shirika la Meli la Zanzibar lina mpango wa kuagiza meli mbili mpya, ameleeza pia MV. Mapinduzi imeshafanyiwa ukarabati na hivi karibuni itaanza safari zake kutoka Zanzibar kwenda Comoro.

Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi amebainisha kuwa Zanzibar imejipanga kwa utalii wa matibabu kwa kuifanya hospitali mpya ya Lumumba kuwa kituo cha kupokea wagonjwa kutoka nje hasa nchi ya Comoro pindi itakapokamilika na kuanza kutoa huduma.

Naye Balozi Yakubu amemuahidi Rais Dk. Mwinyi kudumisha uhusiano wa kindugu uliopo kati ya Zanzibar na Comoro pamoja na kuendeleza hati za makubaliano ya pamoja na kamati ya ushirikiano ya kudumu.

IMG-20240514-WA0016.jpg
IMG-20240514-WA0014.jpg
IMG-20240514-WA0015.jpg
 
ZANZIBAR NA COMORO ZINA MAHUSIANO MAALUM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar na Comoro zina Mahusiano maalum ya kuchanganya damu wa kindugu hivyo ameridhia kufunguliwa kwa Ofisi ya Konseli Mkuu wa Comoro hapa Zanzibar.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Comoro Mhe.Saidi Yakubu aliyefika kumuaga baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Ikulu Zanzibar tarehe 14 Mei 2024.

Rais Dk.Mwinyi pia amemtaka Balozi Yakubu kuangalia fursa zilizopo za kuuza bidhaa mbalimbali kutoka nchini na kuzisimamia hati za makubaliano ya pamoja na kamati ya ushirikiano wa kudumu ikiwemo katika sekta ya afya, elimu, utamaduni, biashara, usafirishaji na habari kupitia shirika la utangazaji Zanzibar (ZBC).

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Shirika la Meli la Zanzibar lina mpango wa kuagiza meli mbili mpya, ameleeza pia MV.Mapinduzi imeshafanyiwa ukarabati na hivi karibuni itaanza safari zake kutoka Zanzibar kwenda Comoro.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amebainisha kuwa Zanzibar imejipanga kwa utalii wa matibabu kwa kuifanya hospitali mpya ya Lumumba kuwa kituo cha kupokea wagonjwa kutoka nje hasa nchi ya Comoro pindi itakapokamilika na kuanza kutoa huduma.

Naye Balozi Yakubu amemuahidi Rais Dk.Mwinyi kudumisha uhusiano wa kindugu uliopo kati ya Zanzibar na Comoro pamoja na kuendeleza hati za makubaliano ya pamoja na kamati ya ushirikiano ya kudumu.
 

Attachments

  • IMG-20240514-WA0482.jpg
    IMG-20240514-WA0482.jpg
    593.6 KB · Views: 2
  • IMG-20240514-WA0484.jpg
    IMG-20240514-WA0484.jpg
    611 KB · Views: 2
  • IMG-20240514-WA0481.jpg
    IMG-20240514-WA0481.jpg
    777.1 KB · Views: 2
  • IMG-20240514-WA0485.jpg
    IMG-20240514-WA0485.jpg
    766.8 KB · Views: 1
  • IMG-20240514-WA0483.jpg
    IMG-20240514-WA0483.jpg
    546.6 KB · Views: 2
  • IMG-20240514-WA0480.jpg
    IMG-20240514-WA0480.jpg
    575.5 KB · Views: 3
Alete wapiga kura kutoka Comoro wampigie Kura na CCM yake labda waTanganyika wameanza kushituka wanataka nchi yao
 
Ukisoma habari hiyo utadhani Rais Mwinyi ni Rais wa Tanzania au Zanzibar Ndiyo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hongera sana Zanzibar.
 
Back
Top Bottom