Balozi yakubu afika ZIPA kujitambulisha

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
817
514
Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanziabar (ZIPA) imekutana na Balozi wa Tanzania Nchini Comoro Balozi Said Yakubu aliyefika Ofisi za ZIPA Maruhubi Kujitambulisha

Balozi huyo ambae ameambatana na watendaji kutoka Idara ya Mambo ya Nje Tanzania amesema kuteuliwa kwake kuwa Balozi wa Comoro ni muendelezo wa historia ya kiuchumi iliyoanzishwa na waasisi wa Nchi mbili hizi Comoro na Tanzania

Amesema Tanzania inafaidika na biashara ya mazao ya nafaka na kilimo inayopanua wigo wa kiuchumi kwa wananchi wake hivyo ZIPA haina budi kuziendeleza fursa hizo za Uwekezaji katika nyanja nyingine ikiwemo usafiri, miundomninu na Nyumba za makaazi

Nae kaimu Mkurugenzi Mtendaji ZIPA Ndg. Vuai Yahya Lada amesema Balozi za Tanzania nje ya Nchi zina mchango mkubwa kwenye Uwekezaji kutokana na makongamano na mikutano inayoandaliwa na balozi hizo kwani huzaa Wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini.
 

Attachments

  • 20240514_175508_InSave_0.jpg
    20240514_175508_InSave_0.jpg
    72.3 KB · Views: 2
  • 20240514_175508_InSave_1.jpg
    20240514_175508_InSave_1.jpg
    170.8 KB · Views: 2
  • 20240514_175508_InSave_2.jpg
    20240514_175508_InSave_2.jpg
    130.3 KB · Views: 3
  • 20240514_175508_InSave_3.jpg
    20240514_175508_InSave_3.jpg
    109.2 KB · Views: 3
  • 20240514_175508_InSave_5.jpg
    20240514_175508_InSave_5.jpg
    69 KB · Views: 3
  • 20240514_175508_InSave_4.jpg
    20240514_175508_InSave_4.jpg
    141.8 KB · Views: 2
  • 20240514_175247_InSave_5.jpg
    20240514_175247_InSave_5.jpg
    69 KB · Views: 2
Back
Top Bottom