Zanzibar: Msaidizi wa Injinia wa Meli ya MV Mapinduzi ajinyonga meli ikiwa safarini

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Msaidizi wa Injinia wa MV Mapinduzi amejinyonga wakati meli hiyo ikiwa njiani kutoka Unguja kuelekea Pemba, hali iliyosababisha meli hiyo kukatiza safari na kurudi unguja.

Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi Thobias Sedeyoka amethibitisha.

======

Mhandisi msaidizi katika meli ya Mv Mapinduzi, Haji Abdalla Khatib (55) amefariki dunia baada ya kujinyonga wakati meli hiyo ilipokua inatoka Unguja kwenda Pemba.

Tukio hilo limetokea leo Jumatatu Julai 22, 2019, Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, Mustafa Aboud Jume amesema baada ya kupata taarifa hiyo walilazimika kusitisha safari na kuamuru meli hiyo irudi Unguja.
Amesema Khatib amejinyonga katika chumba cha Injini, sehemu aliyokuwa anafanyia kazi na kwamba, hadi sasa bado hawafahamu sababu za kujinyonga kwake.

“Marehemu alikuwa fundi umeme wa miaka mingi tangu enzi za meli ya ukombozi, hivyo ni mtu muhimu sana,” amesema.

Amesema pamoja na hayo, uchunguzi wa kifo hicho umefanyika na tayari jeshi la polisi linaanza kazi zake mara moja kwa lengo la kubaini sababu zilizomfanya injinia huyo kujitoa uhai wake.
IMG-20190722-WA0020.jpg

Msaidizi wa Injinia wa MV Mapinduzi amejinyonga wakati meli hiyo ikiwa njiani kutoka Unguja kuelekea Pemba, hali iliyosababisha meli hiyo kukatiza safari na kurudi unguja.

Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi Thobias Sedeyoka amethibitisha.
Duh! Yakhee huko zenji pemba wenzetu vipi mbona na nyie mwataka kufanana na wale jamaa zetu wa iringa yakhee..? Juzi juzi tu hapa bosi polisi kajinyonga, leo tena mwingine kajitundika jamani huko zenji wenzetu kuna ninii!!
 
Marehemu alikua na hasira mbaya
 
Injinia wa Meli ya MV Mapinduzi Ajinyonga Wakati Meli Ikiwa Safarini

Mtu mmoja anayetajwa kuwa Injinia wa Meli ya MV Mapinduzi inayofanya safari zake Unguja na Pemba, Haji Abdallah Khatib, amejinyonga wakati Meli hiyo ikiwa safarini kutoka Unguja kwenda Pemba.

Mkurugenzi wa Shirika la Meli na Uwakala Zanzibar Salum Ahmada Vuai, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo ameeleza kuwa mtu huyo alikuwa kwenye chumba cha mashine na alikuwa peke yake.

''NI kweli amejinyonga lakini ni mapema sana kujua chanzo lakini Meli imelazimika kukatisha safari yake na kurejea Unguja kwaajili ya uchunguzi zaidi'', amesema Vuai.

Awali Kamanda wa Polisi wa Mjini Magharibi Thobias Sedeyoka, aliiambia EATV&EA Radio Digital kuwa athari ya tukio hilo inakwenda kwa abiria wengine ambao leo ni siku ya kwanza ya wiki na walikuwa wanakwenda kwenye majukumu yao lakini wanalazimika kurudi.

''Bado tunaongea na mamlaka husika ili kujua lakini tu kama mnavyofahamu leo ni Jumatatu watu wanakwenda kwenye shughuli zao huo Pemba lakini sasa wanarudi Unguja ili tuupate mwili na tufanye uchunguzi kisha tutawajulisha zaidi'', ameeleza.
 
Back
Top Bottom